Naomba ushauri maana simuamini

Naomba ushauri maana simuamini

Imenilazimu kufungua akaunti mpya kwa sababu nyingi kidogo. Moja kwa moja kwenye matatizo yanayonisibu, huyu bwana niko naye muda wa miaka karibu minne sasa ila tunakaa mikoa tofauti mimi niko Dar na yeye yuko mkoa mmoja Kusini Mangaribi, naendaga kumtembelea nikipata nafasi na nikiwa huko tunaishi kama mke na mume kabisa.

Yeye kuja mjini mpaka alazimishwe anasema ni kazi inambana yaani nikiangalia maisha yangu na plan zangu za miaka ijayo naona kabisa hapa hakuna cha maana ninachofanya.

Mbali na kutokuwa na imani nae kwenye mahusiano simwoni kama ni mtu mwenye uelekeo wa kufanikiwa, chochote anachopata ni pombe tu. Ananiambiaga plani zake nyingi za maendeleo napata matumaini labda ameanza kupata hamu ya kufanikiwa ila hakuna kitu.

Kila nikamuuliza analalamika kuwa wanawake tuna tamaa, sina tamaa ila nataka na sisi tufike mbali. Marafiki zake wengi wanajielewa na wana kazi nzuri tu, yeye kutwa ni kujisifia tu kuwa anafahamiana na huyu au huyu na kwamba amesoma Dar chuo cha mabrazameni na masistadu ila nikimwambia aniconnect nipate kazi huku Dar anaanza kulalamika nirudi mkoani atanilipa hiyo hela ambayo ningepata nikiajiriwa.

Nikiangalia kweli amejenga hapo mkoani ila pia kuna opportunity nyingi zaidi Dar kwanini anang’ang’ania mkoani? Na ameshawahi kusoma na kuishi Dar muda mrefu kwahiyo sio mgeni.

Lingine nikiangalia umri wangu unaenda na yeye wala haeleweki, tayari ana mtoto na mwanamke mwingine na hana interest ya responsibility na huyo mtoto. Nahisi ndiyo alivyo yaani wale wanaume wa kuzalisha watu tu bila mbele wala nyuma.

Kwenye kutomuamini kimapenzi ni kwasababu kila mara anaongea na maex wake nakusema flani bado ananipenda au flani anajuta kuachana na mimi. Yaani ananiboa sana kama wanampenda si aende kwa wao asinipotezee muda. Kuna wakati rafiki yangu aliajiriwa kwenye ofisi flani hapo mkoani nilitaka nimtume kwa siri baa jamaa anazoenda nione kama atamtongoza ila nikaona ni ujinga. Hii ingekuwa njia nzuri ya kumkamata na kuachana nae ila pia nahisi sitakuwa nimetenda haki, nakosa amani jamani sijui nifanyeje?

Na mambo mengi sana nayofikiria ila niishie hapa kwa leo.
Pole

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo muda uliotumia kutafakar unatisha kabsaa kuanza upya maisha yako as long as unajua nn unahitaj usikubal mtu akucheleweshe mae na ktk kumuacha mtu usimuonee huruma bcoz he won't change hata mkiachana akirud akwambie amechange its nothing tabia ni ngozi haibadliki kabsaaa kuna wanaume ni mizigo ya mama zao usikubal akawa mzgo wako kama wanavyotuona sisi kua kuna wakat tunawarudsha nyuma same applies to them kuna wanaume ukiwa nao bora uwe single kulko kubeba mizigo ya mama zao one thing hajakuoa ,haufahamik popote,so its a grt chance kumove on na maisha yako uyo anakusaidia kukusogezea umr tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unataka kuniambia kuwa pamoja na kuona viashiria vyote hivyo hujaandaa plan B na plan C na plan D?..

Hebu shtuka, kuwa nae na pia angalia wanaume wengine wanaofaa jaribu kuwa nao. Wape nafas wanaume wengine.

Huyo usimuambie kitu, utamuambia mambo yakiwa sawa ukikamilisha plan zako na Bwana mwingine.

Ndio plan zenyewe na wanawake wengi wanafanya,
By the way. Una kila sababu na tumia umbali uliopo kama opportunity .


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom