Naomba ushauri maana simuamini

cpampya

Member
May 4, 2020
16
25
Imenilazimu kufungua akaunti mpya kwa sababu nyingi kidogo. Moja kwa moja kwenye matatizo yanayonisibu, huyu bwana niko naye muda wa miaka karibu minne sasa ila tunakaa mikoa tofauti mimi niko Dar na yeye yuko mkoa mmoja Kusini Mangaribi, naendaga kumtembelea nikipata nafasi na nikiwa huko tunaishi kama mke na mume kabisa.

Yeye kuja mjini mpaka alazimishwe anasema ni kazi inambana yaani nikiangalia maisha yangu na plan zangu za miaka ijayo naona kabisa hapa hakuna cha maana ninachofanya.

Mbali na kutokuwa na imani nae kwenye mahusiano simwoni kama ni mtu mwenye uelekeo wa kufanikiwa, chochote anachopata ni pombe tu. Ananiambiaga plani zake nyingi za maendeleo napata matumaini labda ameanza kupata hamu ya kufanikiwa ila hakuna kitu.

Kila nikamuuliza analalamika kuwa wanawake tuna tamaa, sina tamaa ila nataka na sisi tufike mbali. Marafiki zake wengi wanajielewa na wana kazi nzuri tu, yeye kutwa ni kujisifia tu kuwa anafahamiana na huyu au huyu na kwamba amesoma Dar chuo cha mabrazameni na masistadu ila nikimwambia aniconnect nipate kazi huku Dar anaanza kulalamika nirudi mkoani atanilipa hiyo hela ambayo ningepata nikiajiriwa.

Nikiangalia kweli amejenga hapo mkoani ila pia kuna opportunity nyingi zaidi Dar kwanini anang’ang’ania mkoani? Na ameshawahi kusoma na kuishi Dar muda mrefu kwahiyo sio mgeni.

Lingine nikiangalia umri wangu unaenda na yeye wala haeleweki, tayari ana mtoto na mwanamke mwingine na hana interest ya responsibility na huyo mtoto. Nahisi ndiyo alivyo yaani wale wanaume wa kuzalisha watu tu bila mbele wala nyuma.

Kwenye kutomuamini kimapenzi ni kwasababu kila mara anaongea na maex wake nakusema flani bado ananipenda au flani anajuta kuachana na mimi. Yaani ananiboa sana kama wanampenda si aende kwa wao asinipotezee muda. Kuna wakati rafiki yangu aliajiriwa kwenye ofisi flani hapo mkoani nilitaka nimtume kwa siri baa jamaa anazoenda nione kama atamtongoza ila nikaona ni ujinga. Hii ingekuwa njia nzuri ya kumkamata na kuachana nae ila pia nahisi sitakuwa nimetenda haki, nakosa amani jamani sijui nifanyeje?

Na mambo mengi sana nayofikiria ila niishie hapa kwa leo.
 
Dada yangu,
Nakushauri achana na huyo mwanaume mbona wanaume wapo wengi na watakaokupenda......kukaa na mwanaume kwa muda mrefu siyo kigezo tosha cha kujiaminisha kama atakuoa maana kama angekuwa hana mtoto ungesema atanioa maana hana mtoto lkn tayar unamtoto nabhuwezi jua mawasiliano yake na mama wa huyo mtoto waliozaa nae

Pia kama mwanaume anakupenda hatoweza kukuhadidhia mambo ya wanawake zake waliopita hapo anatumia kama gia ili akuumize moyo ili umuache lin anaona hujiongezi ndio maana anazidi kuziongelea...

Huo ni ushauri tu Dada yangu
 
Mshkaji anataka ujue kua umepata bahati kua na uhusiano naye, tabia ambayo ni ya kitoto na ya ajabu kidogo.

Anawezaje kukutangazia juu ya kupendwa na X wake? Au X kutamani arudiane naye?

Pia to be fair hata wewe unaonyesha una insecurities zako na anaziexploit ili kukutumia anavyoona inafaa. Mojawapo ya insecurity yako ni hauamini kama utapata mtu baada ya huyu bwana.

Ungekua unajiamini, kwa hizo tabia zake wewe hata huu uzi haukutakiwa kuanzisha ungekua ushafanya uamuzi zamani, ila umekuja hapa tukuencourage kumuacha and then akija kukubembeleza useme JF ndiyo imesababisha.
 
Kama huna kazi Dar jaribu kwenda huko mkoani ukae nae kwa muda mrefu ujaribu kuongea nae kwa kituo. Kuna wanaume wanahitaji mtu wa kuwahimiza kufanya mambo ya kimaendeleo. Pengine hata hiyo pombe anaiendekeza sana kwa sababu ya upweke. Ila tabia yake ya kuongelea ma ex mimi pia sijapenda... nachukia mwanaume ambaye kila muda anaongelea na ex iwe kwa uzuri au kwa ubaya....inaboa kishenzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa ushauri.kweli nikitafakari jinsi hali itakavyokuwa miaka ijayo najiona kabisa nikiwa mlezi wa familia huku nikiendelea kumvumilia.najua hii itaishia kunijengea chuki na kushindwa kumweshimu.

Pia mwanaume akishajikita kwenye pombe....Sahau kuhusu maendeleo yaani wewe utafanya mwenyewe maendeleo lkn yeye pesa yake ni pombe na marafiki ndio maana kila malengo mnayopanga hayatimizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usije ukarogwa kubeba na mimba yake aseee,..

Ni hiviii,kuna wadada baadhi kukaa bila mahusiano mnaona kama mmepungukiwa hivii au mtaonekana mna kasoro mpo radhi kukumbatia bomu for the sake of uonekane uko kwa mahusiano,,ole wenuu tena OLE wenu,maisha yalivyo mafupi bado ukawe na mahusiano au ndoa isoeleweka ni bora uwe single for GOD...

Hebu anza upya,tena anza na MUNGU uone kama huto meet your soul mate,.acha kung'an'gania stress,.loh!!!!
 
Miaka minne ?. Na bado huoni kilicho mbele yenu.

Mmmhhhh anyway, ukifikisha miaka 30+ ndio atakutamkia kua Hakuhitaji.

Ushauri wangu...

Kwanza usimuache bila kumwambia.

Kaa uongee naye, mwambie ni miaka minne sasa ,kama kujua na mmejuana , lkn hakuweki wazi, hujui hatima yako, Umri unakwenda, ...mchana laivu mwambie sasa nahitaji uniweke huru na akupe hitimisho kamili ambalo litathibitishwa na matendo nasio porojoporojo za maneno n.k

Mchana laivu... Kuna wanaume ovyo sana, atakutombaa miaka zaidi ya saba.. Usikute amekutoresha na mimba kabisa...alafu mwisho anakuacha ,anaoa mwingine

MTU wa ivo unapaswa uepukane naye kabisa.

Akikuzengua ,nitafute maana namm nipo Dar hahahaha !!.Sijaoa ,Ila Nina mtoto mmoja Nampenda sana, na ukitaka nikuache, basi usimpe raha mwanangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii nayo ni sababu kubwa inayonikatisha tamaa.mzee wake nae tabia ni hiyohiyo nahisi itajirudia kwa huyu bwana.
Hapo ndo unapokosea...huyo mzee wake anahusikaje kwenye mahusiano yenu...kuwa na adabu kwa wazazi...

"corona ipo tuchukue tahadhari"
 
Sasa wewe mwenyewe huna kazi kumbe halafu unalalamika mwenzio hajafanikiwa kama wenzake? Kwanini usifanikiwe wewe kama mafanikio ni marahisi hivyo.

Ungekuwa mdogo wangu usingeolewa na huyo mwanaume. Hakuna mtu hapo.
 
... Marafiki zake wengi wanajielewa na wana kazi nzuri ...

Nikiangalia kweli amejenga hapo mkoani ila pia kuna opportunity nyingi zaidi Dar kwanini anang’ang’ania mkoani? ...
Hatari sana...

"corona ipo tuchukue tahadhari"
 
Inawezekana nina insecurities za kibinadamu kabisa na huenda ndio zimeniweka kwake muda wote huu.lakini sio insecurities za kufanya nidhani sitapata mtu bora zaidi yake la hasha.nadhani huruma inachangia pia kwasababu baada tu ya kumaliza chuo ndio alipoanza stori za maex wake.pia hata tukipishana jambo dogo anasema au kwasababu nimempita kielimu hivyo natamani mambo makubwa.huruma inanifanya nijaribu kumprove kuwa sio tamaa wala tofauti za kielimu ila ni tabia zake na kutoona mafanikio mbele yetu.

Sitaweza kusema kuwa jf ndio imesababisha kuachana.kwangu imekuwa kama njia ya kutoa dukuduku langu kabla ya kumface.kwanza sijui kama hata anafuatilia mambo ya jf yeye ni pombe na kulalamika kuhusu kazi na maex muda wote.

Mshkaji anataka ujue kua umepata bahati kua na uhusiano naye, tabia ambayo ni ya kitoto na ya ajabu kidogo.

Anawezaje kukutangazia juu ya kupendwa na X wake? Au X kutamani arudiane naye?

Pia to be fair hata wewe unaonyesha una insecurities zako na anaziexploit ili kukutumia anavyoona inafaa. Mojawapo ya insecurity yako ni hauamini kama utapata mtu baada ya huyu bwana.

Ungekua unajiamini, kwa hizo tabia zake wewe hata huu uzi haukutakiwa kuanzisha ungekua ushafanya uamuzi zamani, ila umekuja hapa tukuencourage kumuacha and then akija kukubembeleza useme JF ndiyo imesababisha.
 
Nmepata kazi ya kujishikiliza ambayo inawezekana ikawa ya kudumu sasa nikianza safari za mkoani kila siku si nitaonekana siko siriaz?pia sitaki kujiaminisha kuwa nitambadilisha na kumfanya aanze kupenda maendeleo sasa hiv

Kama huna kazi Dar jaribu kwenda huko mkoani ukae nae kwa muda mrefu ujaribu kuongea nae kwa kituo. Kuna wanaume wanahitaji mtu wa kuwahimiza kufanya mambo ya kimaendeleo. Pengine hata hiyo pombe anaiendekeza sana kwa sababu ya upweke. Ila tabia yake ya kuongelea ma ex mimi pia sijapenda... nachukia mwanaume ambaye kila muda anaongelea na ex iwe kwa uzuri au kwa ubaya....inaboa kishenzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa ushauri.sirudi nyuma

Back
Top Bottom