Pia mwanaume akishajikita kwenye pombe....Sahau kuhusu maendeleo yaani wewe utafanya mwenyewe maendeleo lkn yeye pesa yake ni pombe na marafiki ndio maana kila malengo mnayopanga hayatimizi
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo ndo unapokosea...huyo mzee wake anahusikaje kwenye mahusiano yenu...kuwa na adabu kwa wazazi...Hii nayo ni sababu kubwa inayonikatisha tamaa.mzee wake nae tabia ni hiyohiyo nahisi itajirudia kwa huyu bwana.
Hatari sana...... Marafiki zake wengi wanajielewa na wana kazi nzuri ...
Nikiangalia kweli amejenga hapo mkoani ila pia kuna opportunity nyingi zaidi Dar kwanini anang’ang’ania mkoani? ...
Mshkaji anataka ujue kua umepata bahati kua na uhusiano naye, tabia ambayo ni ya kitoto na ya ajabu kidogo.
Anawezaje kukutangazia juu ya kupendwa na X wake? Au X kutamani arudiane naye?
Pia to be fair hata wewe unaonyesha una insecurities zako na anaziexploit ili kukutumia anavyoona inafaa. Mojawapo ya insecurity yako ni hauamini kama utapata mtu baada ya huyu bwana.
Ungekua unajiamini, kwa hizo tabia zake wewe hata huu uzi haukutakiwa kuanzisha ungekua ushafanya uamuzi zamani, ila umekuja hapa tukuencourage kumuacha and then akija kukubembeleza useme JF ndiyo imesababisha.
Kama huna kazi Dar jaribu kwenda huko mkoani ukae nae kwa muda mrefu ujaribu kuongea nae kwa kituo. Kuna wanaume wanahitaji mtu wa kuwahimiza kufanya mambo ya kimaendeleo. Pengine hata hiyo pombe anaiendekeza sana kwa sababu ya upweke. Ila tabia yake ya kuongelea ma ex mimi pia sijapenda... nachukia mwanaume ambaye kila muda anaongelea na ex iwe kwa uzuri au kwa ubaya....inaboa kishenzi
Sent using Jamii Forums mobile app
Usije ukarogwa kubeba na mimba yake aseee,..
Ni hiviii,kuna wadada baadhi kukaa bila mahusiano mnaona kama mmepungukiwa hivii au mtaonekana mna kasoro mpo radhi kukumbatia bomu for the sake of uonekane uko kwa mahusiano,,ole wenuu tena OLE wenu,maisha yalivyo mafupi bado ukawe na mahusiano au ndoa isoeleweka ni bora uwe single for GOD...
Hebu anza upya,tena anza na MUNGU uone kama huto meet your soul mate,.acha kung'an'gania stress,.loh!!!!