Naomba ushauri kwenye sakata hili

Red pen

Member
Mar 4, 2019
51
36
Salaam,

Mimi ni mjasiriamali mdogo mdogo wa vitenge hasa kutoka Tunduma, katika kuhangaika wa kunifungia mzigo nishajikusanya nikaanza kufanya utafiti nikakutana na sister mmoja anasema yupo Kigoma anaweza kunifungia mzigo Kwa uaminifu mkubwa ila yeye hayuko Tunduma.

Basi, nikaanza mawasiliano nae nikampatia aina ya vitenge ninavyohitaji akasema angeliweza kunifungia mzigo ma kesho autume nilipo.

Nikamtumia Hela, tangu nimemtumia hajaniblock nikimpigia hapokei anafanya kutuma meseji tu, whassap anasoma meseji zangu hajibu, nikajaribisha kumtumia ujumbe na kujifanya Niko nahitaji vitenge kama mteja tofauti nilishangaa ananiambia kwanini namtafuta kwenye Simu nyingine?

Je, inamaana hauzi bidhaa hizo?! Kwa maana kama angelikuwa anauza basi angeligundua ni mteja mpya. Kuna siku alinipigia Simu kuwa mzigo umeshatumwa ila Kuna tatizo nikamuuliza tatizo Gani?

Akadai mzigo huo umefungiwa na mzigo wa mteja wake ambaye hajalipia Kwaiyo nisubilie ampate ili tuchukue mzigo baada ya siku mbili nikamwambia anitumie namba ya mzigo wangu utakaokuwa umeongezeka nitalipia basi alikataa kunitumia akadai nimtumie Hela kwanza Kisha ndio anitumie namba ya mzigo!

Nikakataa, kesho yake ananiambia mzigo utarudishwa Kigoma ili atoe mzigo usiokuwa wangu Kisha autume tena!! Jamani ni wiki mbili Sasa natuma ujumbe kuuliza mzigo wangu ananijibu Kwa ukali kuwa nitulie atanitumia Hadi Sasa hajibu chochote!

Nilimtumia 262,000 naomba msaada kwa namna Gani naweza kupata haki yangu?

Anadai yeye sio tapeli lakini mpaka Sasa hivi nahisi hakuna cha vitenge ila nahitaji nirudishie pesa yangu jamani😭😭😭😭.

Niende wapi nipate msaada ili akamatwe na arudishe Hela yangu maana vielelezo vyote vipo.

Msaada please!
 
Pole sana mkuu ila ukweli ni kwamba wabongo wengi ni washamba na matapeli sana hasa kwenye biashara za umbali na Tayari ulishafanya makosa kutuma hela na pia kwenye biashara usiwahi kumwamini mtu japo wapo watu wachache sana wazuri ila kwa maelezo yako tu huyo ni tapeli hyo ela umepigwa mzeee
 
def_xcode msaada please! Asante
Mkuu ungekuwa kigoma labda ungeweza washirikisha polisi wakamtrack ukamkamata ila umesema hauko kigoma, na polisi wetu navyowajua hawafuatilii jambo bila pesa. Kimsingi unaweza kutumia zaidi ya ulichopoteza.

Pole sana mkuu kuna muda mtu unatapeliwa unakubaliana na hali tu, unaweka hiyo pesa kwenye bad debtors maana unaweza kuendelea kuhangaika na pesa ambayo hutoipata na ukapoteza muda.

Huyo hauzi vitenge ndio maana ulipomtafuta kwa simu nyingine moja kwa moja alijua ni wewe.
 
Pole sana mkuu ila ukweli ni kwamba wabongo wengi ni washamba na matapeli sana hasa kwenye biashara za umbali na Tayari ulishafanya makosa kutuma ela na pia kweny biashara usiwahi kumwamini mtu japo wapo watu wachache sana wazuri ila kwa maelezo yako tu huyo ni tapeli hyo ela umepigwa mzeee
Huyu sister Kwa jinsi nilivyompata ilikuwa anaamasisha watu wasimtumie mtu Fulani aliyekuwa anatapeli watu huko Tunduma akawa anadai hata nae anauza ila si Kwa Bei hizo. Basi nikamuona ni mtu mwaminifu, na akawa anadai huyo sister mwingine alikwenda kwake kama mteja na alipomtumia picha za vitenge basi akaanza kutapeli watu. Alikuwa anadai watu wasimtumie kwani yule ni tapeli. Ndipo kuona atakuwa salama nikamtumia yeye na Sasa Hadi Sasa hivi anazingua
 
Yes! Nahisi kichwa kuuma wadau Hela ngumu, Kila evidence zipo Hadi sauti zake tulivyokuwa tukiwasilana meseji n.k nilimpatia Fb kwenye grup la Tunduma vitenge
Imeniuma sana wewe kupoteza hela, haswa haya maswala ya mizigo ya biashara. Ameprove failure sana.
Nenda polisi andika RB. Ila also. Kama unaweza nipa details ulimpataje huyo, i can give a lea
 
Yes! Nahisi kichwa kuuma wadau Hela ngumu, Kila evidence zipo Hadi sauti zake tulivyokuwa tukiwasilana meseji n.k nilimpatia Fb kwenye grup la Tunduma vitenge
Imeniuma sana wewe kupoteza hela, haswa haya maswala ya mizigo ya biashara. Ameprove failure sana.
Nenda polisi andika RB. Ila also. Kama unaweza nipa details ulimpataje huyo, i can give a lea
 
Mkuu ungekuwa kigoma labda ungeweza washirikisha polisi wakamtrack ukamkamata ila umesema hauko kigoma, na polisi wetu navyowajua hawafuatilii jambo bila pesa. Kimsingi unaweza kutumia zaidi ya ulichopoteza.

Pole sana mkuu kuna muda mtu unatapeliwa unakubaliana na hali tu, unaweka hiyo pesa kwenye bad debtors maana unaweza kuendelea kuhangaika na pesa ambayo hutoipata na ukapoteza muda.

Huyo hauzi vitenge ndio maana ulipomtafuta kwa simu nyingine moja kwa moja alijua ni wewe.
Ndo hapo Sasa! Hadi nikamuuliza Kwan hauna wateja wengine?
 
Nenda kituo Cha polisi toa gharam mtrack alipo, inawezekana hata kigoma hayupo! Hakuna biashara ngumu Kama ya mtandaoni hasa kwa mtu amabaye hujafika hata kuona ofisi yake!!. Kiufupi huyo hafanyi biashara hiyo ya vitenge n tapeli Kama walivyo CCM tu.
 
Kekundu!!, Kekundu!! Kekunduu!!....
Ilisikika kwaya moja...
Ni umaaaku!!!! Kutuma pesa kwa mtu mmejuana kwa simu tu!....

Usikute aliemtumia hela ni mtu wanakaa nae mtaa mmoja... Kampanga jamaa kwa kutumia mtu wa hapo hapo.... Kama wafanyavyo askari polisi a. K. A Pongozzzz
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom