Naomba ushauri kwenu ninyi wastaafu

makundubhyali

JF-Expert Member
May 26, 2013
2,389
882
Wakuu mimi nimefikisha 55 ya ajira yangu serikalini. Naona kama nimechoka na kazi ya ajira na natamani kustaafu mapema shida ni kutojua changamoto za wastaafu.

Mfuko wangu wa akiba ya wastaafu wameniambia nitalipwa milion themanini na tano kwa mkupuo na kila mwezi nitakuwa nalipwa laki nne.

Kwa ujumla tayari nimejenga nyumba ya kuishi niliponunua shamba kijijini kama ekari 30 ,na pia ninazo nyumba kadhaa za nimepangisha mjini.

Hofu yangu inatokana na wenzangu waliostaafu hapa kazini na baadhi yao walikuwa na uwezo mkubwa kazini lakini wanaishi kwa dhiki kubwa na mara kwa mara wanakuja hapa kazini kupiga mzinga utafikiri bado wako kazini.

Kwa mstaafu yeyote mwenye uzofu wa maisha ya ustaafu anipe ushauri kabla sijaamua kuachia ngazi ya ajira
 
Heri yako umesubiri ufike hata hiyo 55 wengine tulikimbia kabla na maisha yanaendelea... Mkuu hata usipostaafu leo jua siku moja utastaafu tuuu.... Hivyo ni vizuri kuamua moja...

Binafsi naishi poa tu na nilijiwekeza kiasi so maisha yanaendelea.

Hao wanaowapiga vizinga hawakujipanga.
 
Wakuu mimi nimefikisha 55 ya ajira yangu serikalini. Naona kama nimechoka na kazi ya ajira na natamani kustaafu mapema shida ni kutojua changamoto za wastaafu. Mfuko wangu wa akiba ya wastaafu wameniambia nitalipwa milion themanini na tano kwa mkupuo na kila mwezi nitakuwa nalipwa laki nne. Kwa ujumla tayari nimejenga nyumba ya kuishi niliponunua shamba kijijini kama ekari 30 ,na pia ninazo nyumba kadhaa za nimepangisha mjini. Hofu yangu inatokana na wenzangu waliostaafu hapa kazini na baadhi yao walikuwa na uwezo mkubwa kazini lakini wanaishi kwa dhiki kubwa na mara kwa mara wanakuja hapa kazini kupiga mzinga utafikiri bado wako kazini. Kwa mstaafu yeyote mwenye uzofu wa maisha ya ustaafu anipe ushauri kabla sijaamua kuachia ngazi ya ajira
Mkuu nani nina wazo kama la kwako. Nampongeza Lusungo amejaribu kumpa ushauri wa kutia moyo , ila hawa wengine ambao naona wanazungumzia umri badala ya ushauri sioni kama hilo ni hitaji la mleta mada.
 
Ha ha ha jamani mpeni mwenzenu ushauri sio kumfanyia mizaha kama hii.
Naona hawa si wastaafu ndo maana kwani nimetumia lugha gani tofauti au wazee wana maandishi tofauti na vijana ? hata hivyo wakitoa ufafanuzi zaidi litakuwa jambo jema ili nipate kujitambua.
 
Ha ha ha jamani mpeni mwenzenu ushauri sio kumfanyia mizaha kama hii.
Naona hawa si wastaafu ndo maana kwani nimetumia lugha gani tofauti au wazee wana maandishi tofauti na vijana ? hata hivyo wakitoa ufafanuzi zaidi litakuwa jambo jema ili nipate kujitambua.
Heri yako umesubiri ufike hata hiyo 55 wengine tulikimbia kabla na maisha yanaendelea... Mkuu hata usipostaafu leo jua siku moja utastaafu tuuu.... Hivyo ni vizuri kuamua moja...

Binafsi naishi poa tu na nilijiwekeza kiasi so maisha yanaendelea.

Hao wanaowapiga vizinga hawakujipanga.
Asante sana mkuu kwa ushauri.
 
Sina hakika but Enzi zile za JK akiwa bado raisi kulikua na ile sharia ambayo mama Gaudensia Kabaka alikua anataka ipite ya kulazimisha kwamba lazima tufikishe miaka 60 ndio tulipwe stahiki zetu zote kwenye hiyo mifko ya jamii; sina hakika kama ilipita ile au bado ipo pending, nakushauri hebu rudi tena kwenye huo mfuko wako and then waulize kama watakata pesa zako au vipi. Vinginevyo mzee wangu nakupongeza kwa uwekezaji ulioufanya mapema.
 
Nakushauri usistaafu kwa umri wamiaka 55. Kwanza utakapostaafu kwa miaka 60 mkupuo wa fedha utakaoupata utakuwa hata zaidi ya shillingi 130millioni na pensheni kwa mwaka itakuwa zaidi ya laki nne. Usidhani kuwa huku mitaani kuna raha hasa wakati huu wa awamu ya tano, huku mitaani kuna taabu sana. Hiyo miaka mitano iliyobaki kwa kipato chako unaweza kujenga tena nyumba mbili za kupangisha mjini. Hapo bado una heshima siku unarudi mitaani heshima imekwisha kabisa.
 
Nashukuru kwa pongezi zako , Mimi mfuko wangu ni LAPF na hauna hilo sharti unaruhusiwa wakati wowote kustaafu kwa hiyari na kulipwa mafao yako muda wowote kuanzia miaka 55 na kuendelea mpaka 60.
 
Nakushauri usistaafu kwa umri wamiaka 55. Kwanza utakapostaafu kwa miaka 60 mkupuo wa fedha utakaoupata utakuwa hata zaidi ya shillingi 130millioni na pensheni kwa mwaka itakuwa zaidi ya laki nne. Usidhani kuwa huku mitaani kuna raha hasa wakati huu wa awamu ya tano, huku mitaani kuna taabu sana. Hiyo miaka mitano iliyobaki kwa kipato chako unaweza kujenga tena nyumba mbili za kupangisha mjini. Hapo bado una heshima siku unarudi mitaani heshima imekwisha kabisa.
Nashukuru kwa input zako ingawaje nimecheka sana kuhusu kujenga nyumba mbili mpya. Kwa ujumla sasa hivi hali si nzuri kwani semina , washa na kongamano zilizo nyingi ambazo si nje ya kituo chako cha kazi posho sahau kabisa. Hata hivyo mawazo yako nitayazingatia.
 
Ml
Nakushauri usistaafu kwa umri wamiaka 55. Kwanza utakapostaafu kwa miaka 60 mkupuo wa fedha utakaoupata utakuwa hata zaidi ya shillingi 130millioni na pensheni kwa mwaka itakuwa zaidi ya laki nne. Usidhani kuwa huku mitaani kuna raha hasa wakati huu wa awamu ya tano, huku mitaani kuna taabu sana. Hiyo miaka mitano iliyobaki kwa kipato chako unaweza kujenga tena nyumba mbili za kupangisha mjini. Hapo bado una heshima siku unarudi mitaani heshima imekwisha kabisa.
Mleta uzi, zingatia sana ushauri wa huyu bwana, binafsi nimeupenda. Najua mwili wako (mleta uzi) utakua umechoka but please, ni ushauri mzuri hasa hapo kwenye uwekezaji zaidi.
 
Hiyo pesa unayolipwa kwa mkupua 10 % fungua ofisi ya kisanii,inayohusiana na kazi uifanyayo.iliyo baki weka Fixed Deposit Account.
Halafu wewe ishi kwa hiyo laki 4 kila mwezi........MUHIMU KULIKO VYOTE.....****Endelea kuamka asubuhi mapema kwenda kwenye kiofisi chako ch kuzugia.
 
Wakuu mimi nimefikisha 55 ya ajira yangu serikalini. Naona kama nimechoka na kazi ya ajira na natamani kustaafu mapema shida ni kutojua changamoto za wastaafu.

Mfuko wangu wa akiba ya wastaafu wameniambia nitalipwa milion themanini na tano kwa mkupuo na kila mwezi nitakuwa nalipwa laki nne.

Kwa ujumla tayari nimejenga nyumba ya kuishi niliponunua shamba kijijini kama ekari 30 ,na pia ninazo nyumba kadhaa za nimepangisha mjini.

Hofu yangu inatokana na wenzangu waliostaafu hapa kazini na baadhi yao walikuwa na uwezo mkubwa kazini lakini wanaishi kwa dhiki kubwa na mara kwa mara wanakuja hapa kazini kupiga mzinga utafikiri bado wako kazini.

Kwa mstaafu yeyote mwenye uzofu wa maisha ya ustaafu anipe ushauri kabla sijaamua kuachia ngazi ya ajira
Million themanini na pension ya 400000 kila mwezi si haba .Cha muhimu ujitayarishe mapema kabla ya kupokea hiyo fedha.jaribu kutembelea ofisi za mifuko ya pension utapata ushauri nasaha mzuri.jaribu kujipa muda ili ubuni sehemu ya ku invest..Vizuri wakati ukipata fedha ziweka Fixed account akili yako itulie na wakati huo unapata faida.
 
yani mkuu tegemea pm za wadada wa mjini nyingi zenye sio za nchiii hii wakijibebishaa mana siyo kwa upendaji pesa ule
 
Back
Top Bottom