Mkuu ninavyosikia kwa umri huo ile tarehe uliyofikisha miaka 55 ulitakiwa uwe ueshajaza fomu za kustaafu kabisa, lakini sasa hivi kama hizo tarehe zimepita ni lazima usubiri tu tarehe yako ya miaka 60. Huwa wanasema ukivuka tu hiyo 55 hakuna tena nafasi ya kusatafu hapa katikati. Wewe piga kazi tu maana uraiani nako hakufai sana. Kuna jamaa yangu alilipwa mafao milioni 200 na pension ya zaidi ya laki 9 kila mwezi (yeye alikuwa mkuu wa idara), ha! Hata miaka mitano haikuisha akawa kwenye mawe mapaka ikabidi aukimbie mji kwenda kujificha kijijini kwao nasikia siku hizi analima alizeti kwa jembe la mkono. Kustaafu bila mipango ni changamoto sana, ingawa hautafia kazini!! Anza sasa kupangilia mambo yako mpaka hiyo miaka 60 kuwa na nyumba tu haitoshi je, una akili za kusimamia hizo mambo? Maana jamaa yangu huyo alikuwa na alikuwa amejenga, ana mashine ya kukoboa na kusaga, akanunua gari kali ya kwendea kanisani, akanunua hiace 2, akawa anakunywa maji ya chupa (akaachana na maji ya kudownload). Lakini alifirisika mpaka akauza na nyumba! (AKILI KIONGOZI).