Naomba ushauri: Kuna mtu kamtongoza mke wangu

Sms na kukataa kukupa namba, ni ushahidi tosha kuwa mwl akikaza atamkula tu
Au pengine kashaliwa....

Aangalie vizuri tarehe za hizo sms pengine hizo za kumkataa ticha ni za kipindi Cha nyuma na ndio ambazo zimeachwa kwenye simu Kama camouflage.

Zile za kumsifia ticha kuwa anamkuna vizuri na miahadi ya kubanduliwa tena ndio hizo ambazo zimefutwa kwa kisingizio Cha simu yake ni ndogo haihifadhi sms nyingi.

Tafuta mchepu au kama unae endelea kumpa backup kiasi flani inasaidia kupunguza mawivu ya kijingajinga.
 
Bro ushauri wangu , hapo" KUNA SHIDA HAPO

MAJADIRIANO YA NN KATI YA JAMAA NA MKE WAKO KAMA MKE ANGEKUWA NA MSIMAMO BAC HATA ZILE SMS ZA KUKATAA USINGEKUTA

ALARM SOOON "ANALIWAA"


TUKATAE TYU NDOA
Kuna ka ukweli hapa.!
Kwa nn mke afute sms za inbox halafu aache sent?
Kuna uwezekano alishaanza kuliwa kitambo sema alihisi mumewe atakuja kustukia na sms zao za kutongozana alishazifuta zamani so akacheza dili na ticha ili ajifanye amemtumia text za kumkataa sa hivi ionekane hivyo na ndio maana hataki hata kutoa namba ya ticha na anakuwa mkali eti naye aliwahi kukukamata na text za wanawake kwa dalili hizo mke keshaliwa na kama hajaliwa basi yuko tayar kuliwa 99%
 
Mke mpaka sasa hajaliwa na huyo mwalimu kwa maelezo uliyotoa. Ila kwa ujinga wako ataliwa sasa. Simama kama mwanaume
 
Huwa nashangaa sana..yaani mwanaume mzima unaogopa kushika cm ya mkeo..eti nitapata presha...stupidy.

Shika cm kagua..ukikuta usaliti piga chini...it is over kwanini uwe na wasi wasi
Dah.! We jamaa una msimamo kama wangu kabisa...ungekuwa karibu ningekuagizia mzinga wa konyagi na chapati sita na supu ya pumbu umeongea point sana!
 
Kosa haliihukumiwi kwa kosa ...we simamia msimamo wako either asiende Tena kazin kwake au akupe namba ya jamaa upate uhakika ndio aende

Kumpigia simu mwanaume mwenzio inahitaji moyo sana yeaendelee na mishe zingine japo kuna kila dalili ya uyo wife kuja kuuza mechi......!!!! Mwanamke kama hajakuelewa huwa hawatakagi kujua chochote kuhusu wewe ila huyu mke wa bwashee tayari anaelekea kiblaa
 
Duuh mtihani huoo ila mwanamke wako ana msimamo maana hapo alikuwa anatongozwaa ila na wew acha kufatilia simu ya mkeooo... hakuna mwanamke asieliwaaa aiseee.
 
Uko stressed wakati hajagegedwa akigegedwa utajinyonga.

R.I.P in advance.
Huwezi kusema moja kwa moja kuwa hajaliwa maana hizo sms zinaweza zikaachwa za kuzugia in case of any ziokoe jahazi. Hapo inawezekana kabisa jamaa anakula zigo hizo jamaa kategeshewa tu zimpe contractions
 
1.Kwanini aache meseji za sent... Halafu afute za inbox?... Huyu mwanamke mjanja sana ndugu yangu,,, basi kama vipi angeacha zote izikute kama hakuna kinachoendelea..
2.Kwanini hataki kukupa namba yake??

INAWEZEKANA...Ashaliwa...au anaelekea kuliwa...Be careful ndugu yangu...
 
Mimi ni mtumishi wa idara X, lakini pia ni mjasiriamali, hapo nyuma mke wangu alikuwa anashinda ktk duka letu dogo lakini kwa sababu za kiafya (anasumbuliwa na maumivu ya Mara kwa Mara ya mgongo) ili tulazimu apumzike nyumbani halafu hapa dukani nitafute mfanyakazi, na pia tuwe na binti wa kazi, huyu binti wa kazi pamoja na majukumu ya nyumbani lakini pia alikuwa anaenda kuuza barafu ktk shule iliyojirani ili tujipatie kipato zaidi, maisha yameendelea.

Katika nyumba ambayo kuna Hilo duka langu walihitaji kufanya marekebisho ya nyumba hivo ilitulazimu kusimama biashara Kama kwa miezi miwili hivi, takribani Kama mwezi 1.5 uliopita binti wa kazi alipata dharura akaenda kwao, na ndio ikawa 1 kwa 1. Hivo kwa vile wife alikuwa tu home basi mwanzoni alianza kwenda kuuza barafu mwenyewe ktk shule ile ya jirani. SHIDA NI KAMA ILIANZIA HAPO. Kwani Mara kadhaa nilisikia akiongea na mwalimu wa hiyo shule kumuuliza Kama wanafunzi wanaenda shule, Kuna wakati pia yule mwalimu alimwambia wife kuwa yeye awe anapeleka tu barafu halafu pesa anafata badae, nikamwambia wife hapana, Sasa juzi kutwa usiku mida ya saa 3 nimerudi home sa wife akasahau simu yake jikoni nikasema nimpelekee, akili ikanituka ktk sms, ktk inbox kukawa na sms za kawaida, ila ktk sent items kukawa na sms zifuatazo:

1. Haunitakii mema, unataka watoto wangu walelewe na mama wa kambo?
2. Hizo ni porojo kama porojo nyingine, ishi na mkeo nami niishi na mume wangu.
3. Haiwezekani kwani utaniharibia ndoa yangu.

Ghafla nikakutana na wife akanipokonya simu Ile kw maneno kuwa mbona nashika simu yake, nikamjibu kuwa mi nilikuwa nakuletea.. Nikaachana naye nikaenda kuoga, badae wakati narudi kulala nikamuhoji akasema ni kweli Kuna mwalimu alimtongoza lakini yeye wife akamkataa, na pia akasema kuwa Kuna siku alimpigia simu huyo dada wa kazi (Maria) kuhusu taarifa za yule mwalimu na akajibiwa kuwa n mtu ambaye Yuko ktk familia, nikajiuliza n kwa nn alimuuliza Maria kuhusu taarifa za yule mwalimu, lengo n kwamba afahamu nn kuhusu huyo mwalimu.

Katika maongezi akasema kuwa yeye wife hakumkubalia yule mwalimu na hata sms zinajieleza, nikahoji suala la kutokukuta inbox za yule mwalimu akasema kuwa simu yake n ndogo hivo hakuona umuhimu wa zile sms hivo akaamuwa kuzifuta, kesho yake asbh nikiwa kazini nikamtumia text kuwa anitumie namba ya simu ya yule mwalimu sa akachelewa kuituma ikabidi nimpigie, akasema kuwa hawezi kuituma kwani hataki matatizo zaidi yahusuyo suala Hilo, na akagoma, jioni nimerudi home nikamwambia tena suala la namba akasema kuwa ameshaifuta na hata sms hazipo Tena, nikakosa jibu. Leo asbh nilimwambia kuwa hataenda tena kuuza barafu ktk Ile shule, mchana Kaja dukani akawa anasema mbona n Mara nyingi tu alikuwa akinkuta mm na sms za wanawake wengine, sikutaka kulijibia hilo,... NIKO STRESSED NA SUALA HILI ninaomba ushauri marafiki

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Sema Mwalimu atapewa tu akikomaa. Sasa hivi anapewa mwingine humjui. 🤣🤣
 
Back
Top Bottom