Naomba ushauri kuhusu ujenzi wa fensi/uzio wa tofali

Udochi

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
761
1,006
Mafundi na wazoefu wa ujenzi, kujenga fensi kwenye kiwanja cha 400 sqm nahitaji tofali za blocks ngapi?

Na hela ya ufundi niandae kiasi gani?

Kiwanja ni tambarare.

Naomba mwongozo.
 
Ili upate idadi ya tofali lazima ujue mzingo(circumference) ukitumia eneo kama hiyo 400sqm inaweza kua ni 20X20=400sqm mzingo itakua ni (20+20)x2=80m au 25X16=400sqm na mzingo (25+16)x2=82m au 40x10=400sqm na mzingo ni (40+10)x2=100m nk. So vipimo vyote hapo juu vitakupa majibu tofauti Weka vipimo vyake halisi vya urefu na upana nikuchakatia fasta.
 
Iliupate idadi ya tofali lazima ujue mzingo(circumference) ukitumia eneo kama hiyo 400sqm inaweza kua ni 20X20=400sqm mzingo itakua ni (20+20)x2=80m au 25X16=400sqm na mzingo (25+16)x2=82m au 40x10=400sqm na mzingo ni (40+10)x2=100m nk. So vipimo vyote hapo juu vitakupa majibu tofauti Weka vipimo vyake halisi vya urefu na upana nikuchakatia fasta.
Mkuu mimi mwenye mzingo wa mita 114 nitahitaji tofali ngapi?

Urefu kwa urefu wa mita 30 na upana wa mita 27

Sent from my vivo 1938 using JamiiForums mobile app
 
Unajenga ukuta wenye kimo (height) ya mita ngapi? Unaweka tofali tupu, au kuna sehemu unaacha nafasi kwaajili ya conceete louvres au magrill ya chuma?

Otherwise, makadirio ya chini ni tofali 2500. Makadirio ya juu ni tofali 3000.
 
Mkuu mimi mwenye mzingo wa mita 114 nitahitaji tofali ngapi?

Urefu kwa urefu wa mita 30 na upana wa mita 27

Sent from my vivo 1938 using JamiiForums mobile app
Kama ni ukuta tu(solid wall) bila louvres au magril tegemea kutumia tofali 3,500 hii ni kwa ukuta wa mita 3 juu kutoka usawa wa ardhi. Yani msingi/kiuno 0.5m na ukuta wenyewe ni 2.5m

Chini hapo ni moja ya kazi zangu mt meru hospital ni ukuta wenye urefu wa mita 360 hivi. Tembelea Instagram yangu ujenzi08 au Facebook ujenzi. Karibuni

FB_IMG_1648818291625.jpg
 
Tofali za nchi 5 zinafaa?
 
Ili upate idadi ya tofali lazima ujue mzingo(circumference) ukitumia eneo kama hiyo 400sqm inaweza kua ni 20X20=400sqm mzingo itakua ni (20+20)x2=80m au 25X16=400sqm na mzingo (25+16)x2=82m au 40x10=400sqm na mzingo ni (40+10)x2=100m nk. So vipimo vyote hapo juu vitakupa majibu tofauti Weka vipimo vyake halisi vya urefu na upana nikuchakatia fasta.
Vipi hapa kwenye sq 1054 ambapo ni 40 x 26...urefu wa ukuta uwe standard
 
Nikifikiriaga wingi wa matofali ya fence, naishia kujenga kwanza fence mpaka nyumba iishe. Fence inakula matofali mengi kuliko nyumba yenyewe!
 
Kiwanja changu ni squaremeter 367,
Mita 21×17.5,
Nimetumia tofali 2,300 kukamilisha uzio wa kozi 8.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom