Naomba ushauri kuhusu Mizani ya kupima dhahabu

GONZZ EPACLEM

JF-Expert Member
Dec 3, 2016
312
239
Habari wanajukwaa,

Niende moja kwa moja, nipo katika maeneo ya wachimba dhahabu na nimevutiwa sana na biashara hii kiasi kwamba natamani nijitose katika ulimwengu wa biashara ya dhahabu kwa namna ya ununuzi wa dhahabu mbichi (yaani ile ambayo haijayeyushwa), kiasi fulani nimeielewa hii biashara.

Sasa kabla sijaingia rasimi, kuna vitendea kazi kwa maana ya mzani (GOLD SCALE) inahitajika na fedha kiasi ya kuanzia, hivyo, nini kusudi la kuandika uzi huu, ni kwamba humu ndani JF kuna wabobezi wa biashara hii na ombi langu kutoka kwao ni wanisaidie aina gani ya mizani ambayo ni portable na ina ubora zaidi katika kupima dhahabu na inayokubalika kwa wachimbaji wadogo wadogo.

Asanteni na karibu kwa maoni yenu
 
Mzani pekee ni TANITA
Huu ndo wakubalika na umezoeleka kwa watu. Mweusi
Unauzwa 230,000 Mwanza
 
TANITA,
bei yake 130,000/ chukua huo ,ambao unapima desimali moja utakupa faida zaidi

mzani huu una aminika kwa wachimbaji wadogo wadogo
 
🙏Asnte
Ila nashindwa kuelewa hii mizani ya Tanita,mbona bei zake tofauti tofauti sana?
Nimeagiza huu mzani dar lakini bahati mbaya nimekutana na bei tofauti ili hali inapima uzito sawa
Kuna hizi bei
1. 120k kwa dar
2. 260k kwa dar

Kwa mwanza ni 230k,
Naomba ufafanuzi plz wa hizi bei
 
Ila nashindwa kuelewa hii mizani ya Tanita,mbona bei zake tofauti tofauti sana?
Nimeagiza huu mzani dar lakini bahati mbaya nimekutana na bei tofauti ili hali inapima uzito sawa
Kuna hizi bei
1. 120k kwa dar
2. 260k kwa dar

Kwa mwanza ni 230k,
Naomba ufafanuzi plz wa hizi bei
huo wa 260K,unapima units kama g,ounce,carat,grain na kadharika

unapima kuanzia 0.01g na other units

huo wa 130K unapima only gram (units) na 0.1 g kipimo cha chini

fanya uchaguzi wako
 
Back
Top Bottom