Naomba ushauri kuhusu huyu mwanamke

Naomba ushauri kuhusu huyu mwanamke

Mwenye uzi ni mwajiliwa wa serikali, ukute anakadegree harafu anashindwa kuhendo mambo madogo kama hayo. Nikiwa kama mwajiri wako nakufuta kazi kuanzia sasa.
 
Kama una ujasiri wa kuendelea naye fanya hivyo lakini kuwa makini sana asije akatoa tena mimba yako.
 
wanaume duniani waaelekea kuisha wanabaki wale wenye vichululu.
 
Mwishoni mwa mwaka 2019 nilikuwa kwenye mahusiano hot ya kimapenzi yenye ndoto za kuja kuishi pamoja na huyu mwanadada

Mimi nikiwa mwajiriwa wa serikali yeye akiwa kwenye taasisi za ukopeshaji ,baadae akahamishwa na taasisi yake kwenda mkoa jirani,hata hivyo mapenzi yetu yalikuwa ya moto

Miezi michache baadae akaanza kuonyesha dalili za kutaka kiniacha,mara hajibu sms kwa wakati,hapokei sim,baadae nikachoka moyo binafsi ila nikafanya uchunguzi nikagundua ana mahusiano mengine na mtu mwingne nikaamua kuachana naye rasimi

Miezi 3 iliyopita nikiwa bize na harakati zangu,kuchek whasap nikakuta sms yake ikinijulia hali nami nikajibu fresh,baada ya siku tatu akanipigia sim akiniomba msamaha na maelezo kibao,sikumwelewa akamtumia rafiki yangu wa karibu akalialia akanishawishi basi nikamwambia nipe muda,kadri siku zinavyoenda mawasiliano yakawa ya karibu zaidi

Basi kwa kuwa moyo wangu ulikuwa unampenda huyo mwanamke ikabidi nianze kurudisha mahusiano

Lakini baada ya mwezi mmoja kupita nikaingia whasap kuperuzi nikakuta status yake ina watoto mapacha,nikamuuliza vipi wanao au akanijibu ndio nilijifungua mwezi uliopita

Alivyoniambia hivyo moyo wangu uliuma hatari sikumtafuta tena wala sikupokea simu yake wala sikujibu sms zake

Sms aliyonitumia ya mwisho ikasema hivi" Nilijua hunipendi tangu awali,huna mapenzi ya dhati,ungekuwa unanipenda upendo wako ungedhihirika kwenye kipindi hiki kigumu cha maisha yangu ,kumbuka hawa ni malaika tu hawana kosa ,ndio nimefanya makosa makosa kwani wewe huwezi ukafanya makosa ya kuzaa nje? "

Ila kimoyo moyo nami pia nimezaa nje mtoto mmoja

Wadau naomba ushauri
Hadi umefikia kuomba ushauri maana yake bado unampenda rudiana nae.

...........Ila ningekuwa mimi hakuna kurudi nyuma wala sihitaji ushauri.
 
Hv n kwa nn wadada wakiacha mtu hupenda kurudi. Huwa wana pima upepo au !!!!!!!!

Anyway
Na mm niliachwa mwezi sept baada ya mda alirudi, ila ukweli n kwamba mwanamke akikuacha ujue hakupendi kaa nae mbali na mm nilimzia gear hewani

Kheri yetu wanaume tutasema mm naona sijatulia bado nna mambo mengi ila sio mademu
hua wanataka kupunguza na kumantain body count!. ili asijione ametumika sana kwa watu wengi! mile age zisome kidgo
 
Mwambie malaika wanajuana mpaka kiongozi mkuu. Na wako verified, hao wake ni watoto na akubali kuwa ni single mother.
 
ndio ila idadi ya wanaume wanaomtumia atakua ameimantain haijaongezeka, hvo atakua anajiona yy wa thamani( sio malaya ) kuliko yule aliepitiwa na wengi
Aahhh kina dd wana ujinga sanakwa head zao 🤣🤣
 
Mimi kama mwanamke achana na huyo mpuuzi. Hakupendi hata lepe. Anakutaka wakati huu wa shida tu.a apambane na hali yake.
Ila kuna watu vichaaa
 
Back
Top Bottom