Naomba ushauri kuhusu hili

kagarara

Senior Member
Nov 23, 2010
118
9
Mm natarajia kuhtim masomo yangu kwenye chuo kimojawapo hapa tanzania, lakini akilini mwangu nina mawazo makuu mawili; kupata ajira na kuoa. Nimemweleza mpenzi wangu kuhusu mipango ya harusi yangu akaniambia yy yuko tayari kwa ndoa pale tu nitakapoona inafaa. Kwa wadau wa jf wenye uzoefu katika masuala ya ndoa, je baada ya kuhitimu huo mwezi wa nane ni mwaka gani(baada ya muda gani) ambao mnanishauri tufunge hiyo ndoa yetu takatifu na huyu mchumba wangu?
 
Mi nafikir muda sahihi wa wewe kuoa ule ambao wewe mwenyewe unaona uko tayari.
 
Inaelekea wewe mwenyewe ujielewi?jihoji
kwanza wewe unataka nini then amua
nivigumu sana kupata ushauri sahihi.
 
Wewe utakapoona uko tayari kukabiliana na majukumu ya kifamilia!
 
Inaelekea wewe mwenyewe ujielewi?jihoji
kwanza wewe unataka nini then amua
nivigumu sana kupata ushauri sahihi.

ndiyo mkuu, lakini ndo maana nauliza ushauri ili niweze kuchcnganya na akili na mawazo yangu!
 
hakuna muda muafaka wa kuoa!umri ukitimia na ukampata unayeamini mnawezana waweza funga ndoa!kila la kheri mkuu
 
labda huyo dada anaona hujajiandaa,hakuna haraka kama unataka mambo mazuri...maliza shule,tafuta kazi kwanza ndio umuoe-ukimuoa mapema kabla hujapata kazi,majukumu ya nyumbani yatawafanya mstruggle hivyo kuweka strain kny mapenzi yenu.na kama mtoto ataingia hapo kati mapema kabla hujapata kazi ndio kabisaaa itakuwa mushkeli.
 
Mi nafikir muda sahihi wa wewe kuoa ule ambao wewe mwenyewe unaona uko tayari.

naongezea kuwa wakati ukiendelea kumalizia masomo yako, muombe Mungu akusaidie ktk last minute choice, japo huwa kifupi, lakini mengi hutokea kipindi hicho.

but as a woman, sijafurahishwa na msichana mwenzangu kusema kuwa yeye yuko tayari wakjati wowote wewe utakapoona nafaa. sijafurahi kwa sababu naona kashindwa kukupa msaada hata wa mawazo ktika kipindi hiki mnapojipanga na maisha yenu wawili, nadhani kauli zake hizo ndio zimepelekea wewe kuja huku JF kuomba ushauri kwani hakika amekuacha peke yako uamue siku na saa ya harusi. mke mwema lazima pia awe mshauri mwema. mambo mengi sana huharibika maishani kwa mtu kukosa ushauri. sasa wewe bado u-mwanafunzi na huenda mambo ya kipato bado si shwari ila yeye anasema yuko tayari wakati wowote, akimaanisha hata leo. so yeye anaangalliaje majukumu ya ndoa ikiwa utaamua kufunga naye ndoa kesho asubuhi? na mkipata mtoto mtamtunzaje wakati mnasoma, nk.

so nakushauri pamoja na ushauri wa hapa, endelea kumshawishi mwenzio ashirirki katika kutafakari maisha yenu na mfike mahali muwe mnashauriana pamoja badala ya yeye kukuachia peke yako eti "yeye yuko tayari wakati wowote utakaooona unafaa" hii kauli haiashiiriikukupenda bali inaashiria kukuachia mzigo wa tafakari katika mambo nyeti na magumu kuamua kama haya. na inaweza kuwa mzigo mkubwa sana kwenye ndoa yenu siku za usoni. but nawatakieni kila la heri
 
Nawashukuru sana wana jf kwa ushauri wenu mzuri mnaoendelea kunipatia. Nina imani utanisaidia sana.
 
anzaa kazi, paata kwako, then omba michango kama kawaida then oa,
ila angalia kamamupenzi anakupima maana jibnu lake linabidi liwe pia mjijenge wote kimaisha i mean pamoja as ckako chake na chake chako
 
Mi nafikir muda sahihi wa wewe kuoa ule ambao wewe mwenyewe unaona uko tayari.

nimekubali kwa asilimia zote.
Watu walikuwa wanaoana hawana hata godoro sio siku
hizi hadi tujenge tununue gari, tufungue biashara, tutiane na mimba ndio ndoa itangazwe.
 
Mkuuu jiweke kwanza sawa kimaisha.......Usikimbilie kuowa maana baada ya miezi 5 utaanza kujuta...take ur time weka maisha sawa ndio uoe huo ndio ushauri wangu!!
 
Back
Top Bottom