Naomba ushauri kuhusu Biashara ya Bajaji

Kwa bajaji mpya kama dereva mzuri, Barbara ya lami kila service maximum 35,000@kwa kila bajaji. Na hii inafanyika kila baada ya siku 14 (once in 2weeks).
Naliandika hili Kaka. Kuna mtu alisema tuzipeleke kariakoo. Lakin shauri tuliloafikiana pale ni bora tukomae na kule kule Kwa mana pale zilipo bajaj zinakwepwa Kwa sabb sio tvs
 
Bila shaka kuna mahali panavuja, mimi naona ukinunua used ndio huwa zinasumbua service. Lakini mpya atleast 2years zikiwa barabarani ndio matengenezo ya gharama huanza
Yan hizi nimepewa samari ndan ya miez 6 ngoma ikaanza kuwa ngumu. Kuna watu mpaka leo Wana majarida kituo cha polisi wanadaiwa.
 
yani mkuu vijana mda mwingine hatuna exposures
Mimi ninayo moja na inamwaka na miezi miwili sasa lakini matengenezo makubwa niliyofanya yaligharima 50,000 niliwepa lakini mara kwa mara huwa yanachezea 28,00 hadi 34,000 kwa kila siku 14. Na vitu vya kurekebisha mara nyingi huwa ni grease,oil, plug, rubber bush

Madereva rough rough fukuza usiwe na huruma. Mimi mpaka sasa nimebadilisha mara nne.
 
Naliandika hili Kaka. Kuna mtu alisema tuzipeleke kariakoo. Lakin shauri tuliloafikiana pale ni bora tukomae na kule kule Kwa mana pale zilipo bajaj zinakwepwa Kwa sabb sio tvs
Kwa Dar sjajua soko lipoje, huku mikoani abiria hawachagui brand, wanapanda yoyote itakayokuwa mbele yao. Na hizo brand zingine mimi sjawahi Miliki mi nipo n TVS
 
Kwa Dar sjajua soko lipoje, huku mikoani abiria hawachagui brand, wanapanda yoyote itakayokuwa mbele yao. Na hizo brand zingine mimi sjawahi Miliki mi nipo n TVS
Shida madereva wanadai kama sio tvs sijui ni Kama gari manual
 
Vijana wameua kwa maksudi kabisaa,, yani bajaji ununue mpya, ndani ya mwaka hazitamaniki??? Mmhhhh au barabara mbovu,,huko kuna barabara nyingi za vumbi.... Njoo upige kazi..zakhem darlive pale kwenda kkoo.. fasta unapata pesa mzuri.
Mkuu kuna kipande cha barabara kutoka mbande kwenda msongola ambacho ni kibovu sana juzi nimepita hapo yaani hapafai kwa bajaji. Sasa kama wako huko lazima watapata changamoto bajaji kuharibika hataka.
 
Kwa mpango wa mkataba umekufa Kwa Hali iliyopo. Bajaji Kuna siku hazikufanya kazi na mpaka Sasa mkataba umevunjika. Mkataba ulikuwa miaka 2 kila siku elf 20.bajaj sas zinaleta hesabu ya elf 15 na Hali mbaya. Zimechoka kammaa uji na matengenezo kila wiki

Kikao cha dharura hapa mwisho kimefamywa na mm nlikuwepo hizi hela za mikopo ya vijana. Nimecheka Sana hesabu zao hawa jamaa. Mm nataka nifanye kitu genuine kwanza wamalize mkataba tuziuze tugawane hela
Hizi pesa za mikopo ya halmashauri kwa nini zinakuwa na urasimu sana?
 
Habari!

Natafuta Bajaji ya kufanyia kazi
Nipo teyari kwa mkataba au kawaida kuleta hesabu
Nina uzoefu pamoja na uaminifu wa hali juu.

Nina Leseni na kitambulisho cha taifa (NIDA)
Namba: 0674074563
Nipo teyari kufanya kazi sehemu yoyote kwa Dar

Nipo Temeke Dar es salaam
 
Back
Top Bottom