Naomba ushauri katika suala hili la kuandika makala

Innocenzo

Member
Jul 29, 2017
21
4
Habari zenu ndugu.Hivi karibuni nimegundua nina uwezo(sijui tuseme kipaji) cha kuandika makala. Ninaandika makala za aina mbalimbali,zikiwemo za elimu,uongozi bora,biashara na hata michezo.

Hivyo basi naandika uzi huu kuomba ushauri ni jinsi gani ntaweza kutumia makala zangu kuelimisha jamii huku nikijiingizia kipato,ili nianze kujiajiri ili nitakapomaliza chuo kikuu niwe na mahali pa kuanzia maisha na sio kusubiri kuajiriwa.

Pia kama kuna yeyote ambaye anafahamiana na watu kama vile wahariri na waandishi wa magazeti au mahali pengine popote ntakapoweza kusambaza makala zangu kwa jamii,tafadhali nionganishe nae.
 
Back
Top Bottom