Naomba ushauri juu ya mimba isiyo na baba

Naomba ushauri juu ya mimba isiyo na baba

Naboti

Senior Member
Joined
Apr 17, 2015
Posts
188
Reaction score
48
Habarini wenzangu,

Jamani mimi nimekutana na maswaibu makubwa sana hata sijajua namna ya kuyasuluhisha ndani ya moyo wangu.Nimekuwa nikisumbuana na mume wangu muda mrefu tokea tunaoana ila nimeendelea kumvumilia hadi tumezaa nae mtoto mmoja ambae kwa sasa ana miaka minne.

Wiki iliyopita sijajua mwenzangu kachanganyikiwa nini kaanza kunipiga wiki nzima bila sababu ya msingi kila akirudi anakuta nimelala na mtoto anaanza kunipiga hadi majirani wanakuja kuamulia siku ya nne alivyoanza tu kunipiga nikakimbia na kutorokea kwa wazazi kwa vile sio mbali sana na hapo tunapoishi na mume wangu kesi imeenda kwenye dawati la jinsia na wakanishauri nisimpeleke mahakamani kwa sababu kwa kosa lake hilo la kunipiga kila siku bila hata sababu angeshtakiwa kufungwa kuanzia mwaka mmoja hadi mitatu.

Niko bado kwenye kuona namna gani aadhibiwe mtu huyu na pia tulikuwa tumeshachokana sana.Cha ajabu leo nimeona siku zangu zimepitiliza kama wiki hivi ikanibidi nikanunue kipima mimba ili nipime kama ninayo au la, nilivyopima nikajikuta ninayo.

Uwiii mimi kwa mateso niliyoyapata kwa mwanaume huyu toka anioe sipendi kabisa kurudiana nae sasa kwa hali hii ya ujauzito wake nilionao nitafanyeje wadau yaani nimepanic nimekuwa kama kichaa maana akija kujua nina ishu yake hawezi kuniacha atanikomalia wakati mwanaume ni mtesaji kama polisi magereza.

Nakaribisha ushauri kwa pande zote maana nimedata. Nawaza je nitoe na sijui huwa wanatoaje mimba? Au je nilee mimba? Na nikiulizwa baba wa mtoto nani nikimtaja mume wangu atanirudia wakati ndo kwanza tumeachana.
 
Nilipenda xana nikupe ushaur ila kwa kaul yako ya askar magereza imenikera huwa hawamtesi mtu mpaka awe anamakosa na kafungwa
 
Nashindwa kuamini mwanaume anatoka kazini anafika tuu anaanza kukupiga bila hata kosa? Inawezekana huyo mtu amekuoa bila wewe kumjua kwa undani sana. Kama mmeachana basi wewe zaa tuuu na leo mwanao na maisha yanasonga mbele.

Nani alikwambia kuwa eti u can't live without your hus, kuna maana gani ya kuishi kwenye ndoa ambayao haina Furaha do u think mtafika uzeeni kama wazazi wenu? Kuna wengine watakuja kusema oooh eti mtoto akilelea na mzazi mmoja siyo vyema.

Who said this? Maisha bila Furaha ni shida kubwa sna ndo maana watu mnapata pressure na mnakufa mapema. Kwa ushauri wangu wewe ukiamua kusepa wewe sepa na life inasonga.
 
Hata polisi wamemuuliza kuwa kama hatumii viroba basi anatumia madawa ya kulevya lakini vyote alikataa
 
Huna nia ya kunipa ushauri We Kondoakwetu hiyo sio sababu
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: pnk
Ananipiga na mzigo anakula kama hivi sasa matokeo hayooo wakati tumeshatengana
 
Pole dada hawa wanaume wanatupa wkt mgumu bure,km unakipato chako cha uhakika na unaona unaweza kuendesha maisha yk vzr basi zaa huyu mtoto umlee mwenyewe kumbuka atakuja kukusaidia ww mwenyewe hapo baadae,huyo shetani mpotezee,maisha gan ya kupigana bl sbb asije akakutia kilema cha maisha bure.
 
Asante kwa ushauri mzuri nimeupenda sana.
 
1. Ulipaswa uende polisi....au mpaka akupige na kukuua????

2. Mueleze ni mjamzito

3. Kuwa mjamzito hakukufanyi ishindwe kuishi maisha yako unahitaji support ya watu wako wa karibu

4. Mapenzi yakiisha heri kila mmoja atafute ustaarabu wake kupigana mwisho akutoe kilema kisa na mkasa? Na mwambie kama ana nguvu sana ashike jembe akalime

Mwisho.hakuna mtoto asiye na baba
 
Lea mimba na mjulishe. Halafu embu weka mambo wazi hakuna sehemu umemkera? Maana mtu kuja tu na kuanza kushusha kichapo bila sababu kila siku ni shida kuelewa, au labda ashakuwa chizi?
 
Pole dada hawa wanaume wanatupa wkt mgumu bure,km unakipato chako cha uhakika na unaona unaweza kuendesha maisha yk vzr basi zaa huyu mtoto umlee mwenyewe kumbuka atakuja kukusaidia ww mwenyewe hapo baadae,huyo shetani mpotezee,maisha gan ya kupigana bl sbb asije akakutia kilema cha maisha bure.


Ni kweli kabisa, nashukuru sana
 
Kwani we mbona limekuchoma?Na ww askari magereza?

Lol..mimi limenichekesha 'polisi magereza'...ndo nimemsikia kwako.

Back to topic: POLE! Lea mimba...zaa mtoto mtunze. Kuhusu kuachana au kurudiana ni maamuzi yako.
 
Back
Top Bottom