Naomba Ushauri Juu Ya Hali Hii Ya Wife

naombeni msininione binafsi,aa... ila kuishi na ndugu wa mume ni lawama maana waweza kujitoa kwa roho yako yote lakini hawaridhiki,mi niliishi na shem angu mwaka jana akiwa form two alikua jeuri,kiburi aambiwe kitu na kaka yake lakini sio mimi,nimeumwa mimi ye alikua likizo basi hata anisaidie chochote hamna anaenda kuzurura,lakini angekua mdogo wangu hapo angenisaidia,ila kiukweli tunamkaribisha shetani mana hamuwezi kujinafasi na mume wako
nachoshauri ni kuwasaidia wakiwa kwa wazazi wao au wapelekwe bording au hostel uwahudumie huko
 
Naishi na mke wangu vizuri tu siku nyingi, lakini familia yangu ni kubwa kiasi kwamba kila baada ya muda fulani napata mgeni wa kuja kututembelea. Kama ni mwanaume kidogo afadhali hata watasalimiana na atamuhudumia at least kiroho safi, mbaya zaidi ni wa jinsia ya kike. Hata kama anajua kabisa ni ndugu japo wa mbali kidogo anakuwa mzito sana kumuhudumia kwa vikwazo kibao mara oooh naumwa/sijisikii vizuri/n.k. ilihali sura ikionyesha dhahiri kwamba hajafurahia ujio wa huyo mtu.

Sasa nimepata bahati ya kuwapata watoto wawili wa kike wa kaka zangu, kutoka kijijini ili waje kujiendeleza kielimu, mmoja ni mdogo yuko darasa la II na mwingine amemaliza la saba nataka angalau apate kozi za kujiendeleza hapa mjini. Sasa wife ananambia ye ataki kuwaona la sivyo ataondoka, na nnavyoandika hapa, ameamua kuondoka kweli leo hii. Lakini siku mbili baada ya hawa watoto kufika kwangu, na mdogo wake pia ambaye amekuja kusoma chuo naye alifika kwangu na anaishi kwangu na anasoma chuo kwa gharama zangu!

Hivi ni kweli niachie hawa watoto warudi nyumbani ili nikae na mke na shemeji yangu ndani, au nimwachie mke aende sababu njia zote za kujaribu kumwelimisha mke wangu juu ya jukumu na umuhimu wangu kuwasaidia watoto hawa amezikataa, hataki kabisa kuongea juu yao.

Naomba ushauri wenu.

Umemuoa wewe au mmemuoa ukoo mzima?
 
Huyo wa darasa la saba naweza kufahamu kuja kujiendeleza lakini huyo wa la pili mmmmh bora mrudishe. Kijijini hakuna shule jamani, pili ni mdogo atakosa mapenzi ya wazee. Tatu huyo mkeo kama keshaanza kunung'unika atakuja mtesa huyo mtoto.

He is too young for all that, msaada haukatazwi lakini mbo ya kuishi na extended family hizi za bongo pasua kichwa.
 
ahaaaaaaaaaaaa! Ticha ndo umetema vitu hizooooo design za kifisadi kama mtoto Nata??????????? Daaaaah! I cant believe this!!!!!!!!!!!

me nikahisi mtu kaiba PaSsWorD yake jman, Lol
 
Fuata ushauri wa mke wako kaka,achana na watoto wa ndugu zako. Familia ni BABA,MAMA NA WATOTO.Hata huyo mdogo wake anayesoma CHUO fukuza. Kama ni kusaidia watoto wa kaka yako wasaidie wakiwa huko huko kwao,sio unawaleta kwako. Chukua hiyo usisikilize kelele za watu.
Utapata shida sana mkeo akiondoka na ndo mwanzo wa kuharibika kwa ndoa na familia yako kwa ujumla.
 
naombeni msininione binafsi,aa... ila kuishi na ndugu wa mume ni lawama maana waweza kujitoa kwa roho yako yote lakini hawaridhiki,mi niliishi na shem angu mwaka jana akiwa form two alikua jeuri,kiburi aambiwe kitu na kaka yake lakini sio mimi,nimeumwa mimi ye alikua likizo basi hata anisaidie chochote hamna anaenda kuzurura,lakini angekua mdogo wangu hapo angenisaidia,ila kiukweli tunamkaribisha shetani mana hamuwezi kujinafasi na mume wako
nachoshauri ni kuwasaidia wakiwa kwa wazazi wao au wapelekwe bording au hostel uwahudumie huko

swadaktaaaaaa.....
Mke ni rahisi kucontrol ndugu zake lakini ukitaka kucontrol nduhu za mume huchelewi kuiywa mchoyo,tania mbaya na mengine mengi.....tena watasambaziana maneno ukoo mzima..hayo ndo wanayoyakataa wanawake wengi...

Lakini miaka hii kukaa na watu chungu nzima ya nini? Ndugu wa mke na wa mume kama kuna uwezekano wa kuwasaidia huko waliko wasaidiwe huko huko... Au waende boarding la sivyo maneno maneno na mifarakano ndipo inapoanzia.
 
Naomba Unisikilize kwa makini,
Katika dunia hii mara nyingi binadamu tunapata riziki kwa sababu maalumu,tunapata riziki amabzo so zetu.wakati mwingine unaweza pata fedha kumbe fedha hizo ni kwa sababu ya watu flani ambao wamekuwa wakimwomba Mungu awasaidie kujikwamua,na sasa mungu ameangalia mahala pa kupitishia/Kujibu maombi yao akaaona apitishie kwako.Sasa basi unajukumu la kufikisha kile ambacho umetumwa na mungu,na baada ya kufikisha utalipwa na yeye kwa kile utakachokiua umefanya,

lakini pia,umekua unaweza kumudu gharama zote hizo kwa msaada wa Mungu,inafikia siku sasa Mungu anaitaji kuona wewe unamrudishia nini Mungu.Katika hali hiyo tegemea shetani hafurahishwi na mahusiano mazuri yaliopo katiu yako na Mungu kwakua mungu anakuwezesha na wewe unamtolea kwa njia ya kuwasaidia wasiokua na uwezo.kwa sasabuhiyo basi shetani lazima ajaribu kuingilia kati ili kuvuruga na shetani kaaamua kumtumia wakala wake.

Sasa basi, uwamuzi unao wewe,...ushauri wangu ni kwamba yakupasa kua mtu mwenye msimamo wa kukata shetani kukupelekesha,najua sheji anakubip,wewe usimpigie, akitest wewe fanya kweli,usimtafute,usimfate,piga kimya,amin unachofanya wala si unachopelekwa kama remote,

Ndugu yangu ukiyumba tu ndio umasikini umekukuta

start with capital M in when u mention God the creator..................ujumbe mzuri!
 
Tatizo kubwa hapo ninaloweza kuliona ni mke wako kuogopa mzigo wa ulezi.

Kulea mtoto wa darasa la pili, na mwengine aliyepo katika umri ambao watoto wengi huwa wakaidi, si jambo dogo na inawezekana ikawa hilo linalomuogopesha japo kuwa hajachukua njia sahihi kufikisha ujumbe wake (kama hajakueleza hili)

Mkilizungumza suala hilo linaweza kukusaidia kidogo
 
Well said Gaijin,naomba kura yako miss chit chat
Tatizo kubwa hapo ninaloweza kuliona ni mke wako kuogopa mzigo wa ulezi.

Kulea mtoto wa darasa la pili, na mwengine aliyepo katika umri ambao watoto wengi huwa wakaidi, si jambo dogo na inawezekana ikawa hilo linalomuogopesha japo kuwa hajachukua njia sahihi kufikisha ujumbe wake (kama hajakueleza hili)

Mkilizungumza suala hilo linaweza kukusaidia kidogo
 
Last edited by a moderator:
Mmmmh, yaani kabisa nimesoma, nimeanza kazi
Nina wadogo zangu? BAdo wanahitaji shule eti niwaache kuwasaidia kisa kuogopa extended family sijui mume ana nini
Phheeeewwww! Niwaache ili baadae waje kuwa tegemezi?

Au niwaache afu kwenye ukoo niwe nimetoka alone???
Unaenda kwa nduguyo hana hata shati kisa ulishindwa kumsomesha na uwezo ulikuwa nao?

To hell!

Kuna watu fulani fulani wanafanikiwa karibu familia nzima sababu ya kusaidiana, sio kumsaidia mtu pesa bali kumpa njia ya kujipatia kipato.

Mfano, wahindi wa TZ hawatupani, hata wachaga baadhi yao unakuta kaka kamwajiri mdogo wake dukani. Nenda baada ya miaka miwili yule mdogo naye ana kibanda chake, hawa ni katika biashara.

Wanaoamini katika elimu pia, hauwezi kuwa na degree ukasema nimpunguzie kidogo ndugu yangu, awe na certificate afu mie niwe na advanced diploma, elimu haigawanyiki kihivyo, lazima akae darasani na asome.

SI kila jambo la kuiga, iga kwa akili na manufaa ya uwapendao
 
Inavyoonesha Mkeo Hajakataa Kuwapa Msaada Hao Nduguzo,Tatizo Hawi Huru Iwapo Nduguzo Mtaishi Nao!
Kama Kuna Uwezekano Wa Kuwahudumia Nduguzo,Waki Mbali Na Nyumba Yako!..Basi Waondoe Nyumbani Na Endelea Kuwasomesha Wakiwa Mbali!
Msikilize Mkeo Banah!
 
anatikisa kiberiti huyo..we mwambie unakubaliana naye aende kwao halafu usiongee sana..najua ni ngumu ila kaza moyo mkuu. amini nakuambia hamalizi hata wiki atakutafuta mikono nyuma anataka kurudi. pole sana!
Naishi na mke wangu vizuri tu siku nyingi, lakini familia yangu ni kubwa kiasi kwamba kila baada ya muda fulani napata mgeni wa kuja kututembelea. Kama ni mwanaume kidogo afadhali hata watasalimiana na atamuhudumia at least kiroho safi, mbaya zaidi ni wa jinsia ya kike. Hata kama anajua kabisa ni ndugu japo wa mbali kidogo anakuwa mzito sana kumuhudumia kwa vikwazo kibao mara oooh naumwa/sijisikii vizuri/n.k. ilihali sura ikionyesha dhahiri kwamba hajafurahia ujio wa huyo mtu.

Sasa nimepata bahati ya kuwapata watoto wawili wa kike wa kaka zangu, kutoka kijijini ili waje kujiendeleza kielimu, mmoja ni mdogo yuko darasa la II na mwingine amemaliza la saba nataka angalau apate kozi za kujiendeleza hapa mjini. Sasa wife ananambia ye ataki kuwaona la sivyo ataondoka, na nnavyoandika hapa, ameamua kuondoka kweli leo hii. Lakini siku mbili baada ya hawa watoto kufika kwangu, na mdogo wake pia ambaye amekuja kusoma chuo naye alifika kwangu na anaishi kwangu na anasoma chuo kwa gharama zangu!

Hivi ni kweli niachie hawa watoto warudi nyumbani ili nikae na mke na shemeji yangu ndani, au nimwachie mke aende sababu njia zote za kujaribu kumwelimisha mke wangu juu ya jukumu na umuhimu wangu kuwasaidia watoto hawa amezikataa, hataki kabisa kuongea juu yao.

Naomba ushauri wenu.
 
Nimesoma maoni ya wengi, there's mixing feelings lakini ukweli utabaki kuwa kwa maisha yetu ya Kiafrika hatuwezi kukimbia extended family. Wengi wetu tumepitia kwenye mikono ya watu wengi na tumekaa kwa kaka, dada, shemeji, mjomba, nk kabla ya kuanza kujitegemea na kuwa na mafanikio tuliyonayo sasa. Itakuwa ni upumbavu kama wewe baada ya kufanikiwa hautaki kuangalia nyuma na kutoa msaada kama ambavyo na wewe ulivosaidiwa mpaka ukafanikiwa. Wazo la kuwasaidia huko waliko ni wazo zuri, lakini tuwe wakweli elimu ya leo kijijini ni mbovu sana, kwa hiyo kama mtu una nafasi na una nia ya kumsaidia ndugu yako ni bora uanze angali mdogo kw kumpeleka kwenye shule nzuri, provided uwezo unao. Hivi ndiyo tunavyoishi kiafrika. By the way, ni faraja sana kama mwisho wa siku hao uliowasadia wakafanikiwa na kuwa na maisha mazuri, jamani wema hauozi. Kuna familia wamezaliwa zaidi ya 10, lakini wote wamepata elimu nzuri na wana kazi za maana ukifuatilia utagundua kuwa wazazi hata hawakuwa na uwezo wowote wa kuwapa elimu watoto wote, lakini kwa kuwa mkubwa alipata elimu na akatambua umuhimu wa kuwavuta ndugu zake, mwisho wa siku wote wamafanikiwa na wanaishi maisha mazuri ya kuheshimiana na kusadiana kwa shida na raha.
Kwa ushauri kama una nafasi ya kuwasaidia, pls wasaidia kwa kadri ya uwezo wako na mke wako anapaswa ajue kuwa your doing for good.
 
Mtoto wa darasa la pili anakunyima uhuru mama mwenye nyumba??

Nikupe mfano: Nimezaliwa na kukulia Tandale kwa mfuga mbwa, nimetoka kwa manati na kuolewa.
Mdogo wangu yuko darasa la pili, nahitaji asome, kwa sasa naishi Arusha, je unadhani mazingira ya kwa mfugwa mbwa yanafaa sana?? Risk zikoje??

Unamsaidia mtu akiwa mbali kama mazingira ya huko yanaruhusu kusaidika, hata pale mazingira hayaruhusu umwache tu?? Haiingii akilini

Ee Mungu, nisaidie kuwaelewa wanadamu

Inavyoonesha Mkeo Hajakataa Kuwapa Msaada Hao Nduguzo,Tatizo Hawi Huru Iwapo Nduguzo Mtaishi Nao!
Kama Kuna Uwezekano Wa Kuwahudumia Nduguzo,Waki Mbali Na Nyumba Yako!..Basi Waondoe Nyumbani Na Endelea Kuwasomesha Wakiwa Mbali!
Msikilize Mkeo Banah!
 
baadhi ya wanawake ni kama watoto, anapima kina cha maji.

Ila angalia pia kakulia mazingira gani, kama kwao alizoea kuishi wao wa familia yao tu, basi lazima aone mzigo kuishi na nduguzo.

hilo neno pia ,mazingira aliyokulia labda yamechangia yeye kuwa hivyo pia ya kutozoea kuishi na familia kubwa ya nduguzo
 
Jamani nawashukuruni nyote, kwa michango yenu ya mawazo kwa sababu nimepata upeo sasa, kiasi kwamba kuna uwezekano wa kuamua kusaidia au ukaacha au ukasaidia mtu akiwa mbali au karibu lakini pia ukamfuata Mke na kutowasikiliza ndugu au ukawa na msimamo wako binafsi bila kujali wengine watasema nini provided uko katika right way. Mawazo yangu yaliyobakia kichwani hayatofautiani kabisa na yale ya akina na Micha, Kongosho, jamiif na wengineo wengi.
Nawashukuru sana na kwakuwa nilijisikia kama mtu aliyekosa wa kuongea naye kama rafiki wa karibu wa kuweza kunishauri vizuri hadi nilipo leta habari hii hapa, nahisi kama mzigo uliokuwepo ndani ya nafsi yangu nimeutua kwani hii ni true story na imetokea juzi Jumatano nikawa kama nimepoteza ramani vile! Nitatoa feedback kwenu iwapo itatokea vinginevyo.

ILA NAHISI KWA MAISHA YA WATANZANIA WALIO WENGI BADO TUNAISHI KATIKA HALI YA EXTENDED FAMILY, HATA KAMA HATUKAI NA NDUGU KARIBU LAKINI BADO WANATUNYOOSHEA MIKONO KUANZIA SHIDA NDOGO NDOGO KAMA MSOSI (KILIMO KINAPOPATA MATATIZO mfano. UKAME/MAFURIKO), ELIMU, MAKAZI, n.k.
SASA KAMA NTAPATA NAFASI YA KUONANA NAYE HAMUONI KUWA NI VEMA KUMUONYESHA HIZI KOMENTS MAANA WENGINE WAMEWEKA VITU KAMA CASE STUDIES ZA MAISHA HALISI AMBAO WAO WAMEYAPITIA ILI NAYE AWEZE KUELEWA MAONI YENU NI YAPI JUU YA HILI?
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom