Naomba Ushauri Juu Ya Hali Hii Ya Wife | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba Ushauri Juu Ya Hali Hii Ya Wife

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by BOTOPLAM, Oct 31, 2012.

 1. B

  BOTOPLAM Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naishi na mke wangu vizuri tu siku nyingi, lakini familia yangu ni kubwa kiasi kwamba kila baada ya muda fulani napata mgeni wa kuja kututembelea. Kama ni mwanaume kidogo afadhali hata watasalimiana na atamuhudumia at least kiroho safi, mbaya zaidi ni wa jinsia ya kike. Hata kama anajua kabisa ni ndugu japo wa mbali kidogo anakuwa mzito sana kumuhudumia kwa vikwazo kibao mara oooh naumwa/sijisikii vizuri/n.k. ilihali sura ikionyesha dhahiri kwamba hajafurahia ujio wa huyo mtu.

  Sasa nimepata bahati ya kuwapata watoto wawili wa kike wa kaka zangu, kutoka kijijini ili waje kujiendeleza kielimu, mmoja ni mdogo yuko darasa la II na mwingine amemaliza la saba nataka angalau apate kozi za kujiendeleza hapa mjini. Sasa wife ananambia ye ataki kuwaona la sivyo ataondoka, na nnavyoandika hapa, ameamua kuondoka kweli leo hii. Lakini siku mbili baada ya hawa watoto kufika kwangu, na mdogo wake pia ambaye amekuja kusoma chuo naye alifika kwangu na anaishi kwangu na anasoma chuo kwa gharama zangu!

  Hivi ni kweli niachie hawa watoto warudi nyumbani ili nikae na mke na shemeji yangu ndani, au nimwachie mke aende sababu njia zote za kujaribu kumwelimisha mke wangu juu ya jukumu na umuhimu wangu kuwasaidia watoto hawa amezikataa, hataki kabisa kuongea juu yao.

  Naomba ushauri wenu.
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mwache aondoke mchoyo huyo,Iweje ampende ndugu yake wakwako awakatae, HUO NI UBINAFSI......mwambie akiondoka amwache huyo mdogo wake wa kike azibe pengo lake
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  baadhi ya wanawake ni kama watoto, anapima kina cha maji.

  Ila angalia pia kakulia mazingira gani, kama kwao alizoea kuishi wao wa familia yao tu, basi lazima aone mzigo kuishi na nduguzo.
   
 4. m

  mbukoi JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 253
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mwache aondoke kwani anaonekana kusumbuliwa na uchoyo,ujinga na ubinafsi.mke ni msaidizi wako kaka anapaswa kuyaelewa na kuyakubali majukumu uliyonayo na kukusaidia kuyatimiza kwa usahii.akienda kwao hata mwezi na ukaonyesha kutokujali sana atarudi akiwa na adabu zote but usimuache mpe ka midterm break.
   
 5. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Naomba Unisikilize kwa makini,
  Katika dunia hii mara nyingi binadamu tunapata riziki kwa sababu maalumu,tunapata riziki amabzo so zetu.wakati mwingine unaweza pata fedha kumbe fedha hizo ni kwa sababu ya watu flani ambao wamekuwa wakimwomba Mungu awasaidie kujikwamua,na sasa mungu ameangalia mahala pa kupitishia/Kujibu maombi yao akaaona apitishie kwako.Sasa basi unajukumu la kufikisha kile ambacho umetumwa na mungu,na baada ya kufikisha utalipwa na yeye kwa kile utakachokiua umefanya,

  lakini pia,umekua unaweza kumudu gharama zote hizo kwa msaada wa Mungu,inafikia siku sasa Mungu anaitaji kuona wewe unamrudishia nini Mungu.Katika hali hiyo tegemea shetani hafurahishwi na mahusiano mazuri yaliopo katiu yako na Mungu kwakua mungu anakuwezesha na wewe unamtolea kwa njia ya kuwasaidia wasiokua na uwezo.kwa sasabuhiyo basi shetani lazima ajaribu kuingilia kati ili kuvuruga na shetani kaaamua kumtumia wakala wake.

  Sasa basi, uwamuzi unao wewe,...ushauri wangu ni kwamba yakupasa kua mtu mwenye msimamo wa kukata shetani kukupelekesha,najua sheji anakubip,wewe usimpigie, akitest wewe fanya kweli,usimtafute,usimfate,piga kimya,amin unachofanya wala si unachopelekwa kama remote,

  Ndugu yangu ukiyumba tu ndio umasikini umekukuta
   
 6. Swts

  Swts JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 3,072
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Me mijanamike mingine sijui ipoje yan jamani. Me mbona sina roho hiyo,yani napenda wageni na nikiwa mwenyewe nakosa raha. But mi naamini i ni tabia nyingine ambayo mtu anayondani, wengi kwa ksingzio cha wivu, but ukweli ni Roho mbaya,unafiki na uchoyo. We muache akae ukoo,kikimuwasha atarudi.
  Kumbuka dunian wote wapitaji, tafuta paspot ya mahali pema kivyako kwan kila mtu atahesabiwa fungu lake siku ya mwisho, asikutaftie laana kwa watoto ambao hawajamkosea kitu,em Atoke zake, nin banaa, me sipendi mijitu kununa,roho za y! Aaaaagh
   
 7. m

  msemakwelii JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 217
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bro cjakuelewa kwani hamkujadiliana kama mke na mume kabla ya hao watoto kuja, maana familia zetu ni za kubebana kimtindo mtindo ili mradi kila mmoja anapata kidogo cha kumsaidia maishani, Kama familia lazima muwe na misimamo ya familia nawe kama kichwa cha familia lazima uwe na msimamo wako, lazima uonyeshe kuwa ndiwe Mzee wa Boma, Akileta kutikisa kiberiti muonyeshe kuwa kimejaa, kama Vipi Basi Muwe na mstakabali wa familia kila ndg asaidiwe aliko na ndg zake pia wachape lapa, then mwendo mdundo
   
 8. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Huyo mchawi tu
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Achana naye mwache aende mwanakwenda kama analingia kiungo chake cha uzazi mwambie vipo vingi sana au siku mpitishe kona baa aone mademu wanauza mbunye wakaree kuliko yeye ndio atatuliza kipago....
   
 10. mbota

  mbota JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 742
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 60
  mke wako ni wa maana sana na ndio maana ulimuamini na kumuoa. ILA SASA mke wako asikutenganishe na familia yako amekuja amekukuta naa familia means hao watoto ambao hawajui lolote maana ni wadogo hasa huyo wa std 2 na unamoyo wakuwasaidia mm nakushauri uwasaidie mkuu MUNGU ATAKUPIGANIA KATKA HILO JARIBU LA WIFE ATAJAELEWA TU ILA AJUE AFRICAN FAMILY IS EXTENDED FAMILY TYPE NOT NUCLEAR AT ALL
   
 11. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ukitaka kujua kuwa mkeo ni bomu basi mwambie alete ndugu zake. Hapo utamjua vilivyo. Hapa tatizo ni malezi hata saa nyingine atokako. Maana hapa Bongo kuna vikabila vinajulikana kwa uchoyo na roho mbaya. Kama umeoa huko mwanangu umekula wa chuya. You still have the choice. Ajirekebishe au aonje suspension. Mpe msimamo wako uone kama atafuata au la. Ni umaskini wa moyo tu mwanangu unaomsumbua huyo mkeo.
   
 12. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kaka huyo mwanamke atawanyanyasa sana hao nduguzako pindi ukiwa hauko,tena mkumlazimisha ndio watakuwa mahousegal/boy hapo ndani inabidi uwe na msimamo sana pia uwe karibu sana nao kuongea nakuwauliza pia kuzisoma nyakati woga walionao etc.hii dunia tunapita tu wengi wanashindwa kuelewa kwa kweli .sometime chukua maamuzi ya lowassa fukuza wote na muandikishane kuwa hamna ndugu kukaa hapo home kabisa tuone atafanyaje pumbaf kabisa .mimi nina wifi yanu anaroho mbaya sana hapendi ndugu wa mume ukienda kwake hata useme unaumwa hakupi hata maji na dawa,lol nimeacha kabisa kwenda kwao .
   
 13. T

  Tetra JF-Expert Member

  #13
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  "Nitakwenda nyumbani,nitakwenda nyumbani" Ndiyo tishio wanalotumia wanawake wengi wenye ndoa ili kuwafanya waume zao watende jinsi watakavyo wao.Wanatumia maneno hayo kama silaha tu au njia ya kufanya mapatano.Ni kama biashara kwao.
  Wanawake wanaotumia lugha hii hawatambui kwamba wanajidhuru wenyewe kwanza.Wanadhihirisha utoto wao.HAWANA UKOMAVU WA MAISHA.
  Ushauri:
  Mpe muda aende akatulize akili,kuhangaika kumfuatilia au kumpigia simu au kumbembeleza sana ni kumpa jibu kwamba yeye yu sahihi.
  Sina maana muachane La! Muache akae kwao ale huko alale huko atajua thamani ya kuwa kwake.
  SIMAMA KAMA MWANAUME KAMILI NA SIO NUSU MWANAUME.
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mwambie uko tayari waondoke woote
  pamoja na ndugu yake
  au wakae wote
   
 15. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #15
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,122
  Trophy Points: 280
  We baba utakufa na pressure bureeeeee ukiendekeza hiyo vita baridi!!!!!!!!!!!! Dawa ya baba Lara 1 akimleta ndugu yake anamwambia kabisaaaa mama lara 1 hapendi wageni mnavombana ndani mwake, wewe jielewe fanya lililokuleta usiingie kwenye kumi na nane zakeeee! Maisha si mchezo we kaza roho fanya yako ujikomboe!!!!!!!!! UKIMKOROFISHAAAA MI SIMOOOOOOOO!!!! USINITEGEMEE KABISA KATIKA SAFU YA UTETEZI WAKO!!!! We waache wakae hivo hivo jiweke pembeni waangalie wakimalizana wenyewe kwa wenyewe, baadae watazoeana!!!!!!!!!

  Basi wakuja akiambiwa hivo anakaa kwa adabu, full kupiga cargo, hadi mama lara anaanza kumwambia usirudi kijijini banaa mambo gani ya kushika mbolea, kaa jirembe uolewe huku town. LASIVO WATU WA KIJIJINI WANA TABIA YA KUJISAHAAU NA KUJIONA WANA HAKI SAWA NA MAZA HOUSE JST BECAUSE NI NDUGU ZAKO!!!!!
   
 16. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #16
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mke wa roho hiyo mbaya anaweza kuku ua wewe au hata hao ndugu zako apate alichofata MALI.

  Mie nahisi kuna kitu anafanya sasa anakuwa hana raha wa upande wako wakiwepo as wanaweza kumuaribia, ukimchunguza kiundani utakuta maajabu yake mengi usiyoyajua.

  Ni kweli sio haki wewe kumsaidia na ndugu zake na wewe kutosaidia ndugu zako. Pia labda hamna watoto na hiyo inampa wivu wa watoto wa kaka yako.

  Angalia sana tena sana, as akirudi cha kufuata ni kuanza maneno ya uongo juu ya watiti hao hata kusema wameiba kuwa makini sana hapa as anaweza kukugombanisha na ndugu zako ili mradi ashinde yeye na kupata anachopata kwako.

  Ni tabia mbaya ila angeongea nawe kama anaona ni mzigo mkubwa kusaidia kulea hao, ungeweza saidia kwa namna nyingine bila kuaribu uhusiano na kuacha kuwa na roho ya kutosaidia nduguzo.

  Ana wivu sana tena sana, na roho mbaya shuti utakuta kaenda kwa waganga sasa hivi kukologa vizuri as unaonekana ka pesa kakutoa kapo.

  nasisitiza tena angalia asianze kutesa watoto akirudi, maana mapenzi sie nani kusema achana nae wakati unampenda kesho utasema upo nae kama kawa.

  Pia msome akianza mambo ya wamefanya hivi vile warudishe etc as anaweza shinda kukubadili ukadhani ni ukweli kumbe uongo mtupu.
   
 17. epson

  epson JF-Expert Member

  #17
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 1, 2012
  Messages: 508
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  kwa kifupi naweza sema huyo mke wako ni mchoyo, it doesn't make sense kwamba mdogo wake kaja and there is no problem ila kuja kwa ndugu zako anatishia kuondoka, huyo anabip tu by the way how old is she?. ua a man, ua a head of the family and u produce testosterone as well, remain calm she will be back soon. lakini pia nafikiri itakuwa vizuri ukimsaidia dada mmoja wa huyo kaka yako kwa sasa kuliko wote wawili kwa mkupuo, ni ushauri tu
   
 18. N

  Natalia JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 3,558
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mimi ndio maana wanaume wakibongo hatari.kabla ya kumuoa ulimwambia hayo ,it's not good Mkala.I do not believe mambo ya extended family at all.mama angu nae kutwaa anawakusanya akienda kijijini gari limejaa watoto.Akienda kazini tunawafukuza kwa wazazi wao na basi. Well I'm a conservatives republican I believe in personal responsibility.Ujamaa uliisha kitambo jamani kutwaa nagombana na my mom.msiba wanamsubiri yeye,mtu kamaliza shule year.mkaka put your wife kwanza ndugu wa nini ?na nishawaambia ndugu wa mother akienda mbinguni.undugu basi .wanaume wa kiafrika bwana noma
   
 19. N

  Natalia JF-Expert Member

  #19
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 3,558
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  I'm a conservative I do not believe in extended family.put your wife first .Au wapangishie na uwe na kazi mbili
   
 20. N

  Natalia JF-Expert Member

  #20
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 3,558
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Extended family nomaa .put your wife first .unawaza inheritance ya watoto wako kweli wewe .watu wanakufa ghafla .Save money for your kids and wife zikizidi pesa shopping
   
Loading...