Naomba ushauri, hivi huyu ananipenda kweli?

Naomba ushauri, hivi huyu ananipenda kweli?

Joined
Jul 25, 2014
Posts
83
Reaction score
36
Habari zenu wana jamvi,

Naombeni ushuri juu ya huyu boyfriend wangu sijui ananipenda au la? Tumekuwa kwenye uhusiano kwa miaka mitatu sasa, ana miaka 33,hajanitambulisha kwa mtu yeyote kwao hata rafiki pia,haoneshi dalili ya kutaka kuoa.

Sasa japo nikimwambia ananiambia ndio anafanya mipango,nyumbani kwake nimeshaenda na kulala pia hakuna dalili ya mchepko,ila ukitaka ugomvi shika simu yake.

Aliwahi kuibamiza na kuivunja simu yake samsung galaxy s5 kisa niliishika nikawa naangalia nikimuuliza anasema ananipenda, nimemdanganya nina mimba kama tatu zote ananipa hela anasema nikatoe sasa simuelewi anasema ananipenda , eti jamani hapo kuna mapenzi kweli.

Naomba ushauri wenu
 
Hapo subiria maumivu ya moyo....Kama huna moyo wenye kusukuma damu vyema tafadhali sepa faster.
 
Dah mimba tatu(3) zote zake then anakupa hela ukachomoe???? Kazi kweli kweli
 
Pole lakini hapo andaa plan B. kila la kheri.
 
kimbia fasta wakati bado mapema..usisubiri giza liingie..
 
Kweli NEW AGE mna mapepo, yaani unatoa mimba tena 3 alafu unakuja kujisifu hapa 👮, haki ya nani do!!

Unavua chupi ovyo na kijana anaendelea kufaidi wewe unashindwa kufanya maamuzi course of your future. Eeh!!!!!!!!!!!!!!!
 
Yawezekana usiwe type yake ya kuona ila kwa eat and run unafaa...
 
Habari zenu wana jamvi,

Naombeni ushuri juu ya huyu boyfriend wangu sijui ananipenda au la? Tumekuwa kwenye uhusiano kwa miaka mitatu sasa, ana miaka 33,hajanitambulisha kwa mtu yeyote kwao hata rafiki pia,haoneshi dalili ya kutaka kuoa.

Sasa japo nikimwambia ananiambia ndio anafanya mipango,nyumbani kwake nimeshaenda na kulala pia hakuna dalili ya mchepko,ila ukitaka ugomvi shika simu yake.

Aliwahi kuibamiza na kuivunja simu yake samsung galaxy s5 kisa niliishika nikawa naangalia nikimuuliza anasema ananipenda, nimemdanganya nina mimba kama tatu zote ananipa hela anasema nikatoe sasa simuelewi anasema ananipenda , eti jamani hapo kuna mapenzi kweli.

Naomba ushauri wenu

Miaka mi3 hajakutambulisha kwa yeyote,haoneshi dalili ya kutaka kukuoa,hataki ushike simu yake,umedanganya una mimba anakupa hela utoe,bado unataka tukuthibitie kama kuna mapenz hapo!!!
Ok!Huyo ANAKUPENDA sana,tena usimuache!
Umefurahi ee???
 
Mimba tatu umedanganya na akakupa hela ya kutoa aiseee Kimbiaa mbio ndefu dear hafai na hakupendi
 
Ukipendwa huihitaji kuuliza watu
unajua tu we mwenyewe
kama ukila na kushiba
unauliza watu wakwambie kama umeshiba au bado?
 
Kimbia, hamna kitu hapo. He is playing you, nini mnachofanya pamoja? Kama hakuna kinachowaunganisha basi huyo anatarajia kujiengua mda wowote, mtu anayekuambia utoe mimba mara zote hizo hakuwazii mema na hatakuoa kwa kisingizio hicho hicho kwamba ulitoa
 
Back
Top Bottom