naomba ufafanuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

naomba ufafanuzi

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Ngambo Ngali, Feb 13, 2011.

 1. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Nimekuwa nikisia redioni hasa matangazo ya vifo yanayosomwa na redio One ambapo wanatumia neno "mama wake" wakiwa na maana "mama yake fulani".

  Je hayo ni matumizi mazuri ya kiswahili? Zamani tulizoea kusema mama yake....,
  baba yake......................... Je Bakita wamebadili matumizi.
   
 2. C

  Choveki JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2011
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Unajua siku hizi ni unamjua nani si kuwa unafahamu kiswahili vizuri au la ndiyo uwe mtangazaji au mwandishi wa habari.

  Zamani watangazaji walikuwa wanachaguliwa na kuchujwa kweli kweli, siku hizi ni bora liende tu! Wengi wao sidhani hata kama wamefauli hicho kiswahili wanachodhania wanakitangaza! Wakati mwingine wanatia hata kinyaa kuwasikiliza, lakini ndo tufanyeje? Ndo soko "huria" la kazi la ki-Tanzania lilivyo!

  Bakita nao utadhania wanafanya kazi ya kulazimishwa, kimyaaaa! Kitivo cha kiswahili chuo kikuu Dar wengi wao hata hawawezi kutamka au kuandika Ng'ombe au hata nzi! sasa hapo utategemea nini? Wengi wao hawajui tofauti ya mazingira na mazingara, siku na masiku etc! na unaambiwa ndo mabingwa wa lugha!
   
 3. b

  bakarikazinja Senior Member

  #3
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 179
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  jamani mimi roho inaniuma sana kusikia mtu anaharibu hii lugha ya kiswahili wakati mimi navyo jua ndio utamaduni wetu sisi waswhili yaani weacha tu lazima babu kifimbo cheza arudi
   
 4. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Je wanaosema naniliu badala ya nanihii, 'baada' badala ya 'badala', wapo hata wantangazaji redioni wanaotamka thatha badala ya sasa, wale wenye kithembe.(Ni sawa kuajiriwa kwenye tasnia hii) kuna wale wliobobea kwa kusema lisaa limoja badala ya saa moja, au masaa 24 badala ya saa 24. Hebu fikiria hii ni mpaka kwenye matangazo ya kampuni kubwa tu za simu hapa tz, utajiuliza hivi wahusika wanapoidhinisha tangazo huwa wanazingatia usahihi wa lugha? SOMEBODY HELP PLEASE!!!!!!
   
 5. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2011
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,126
  Likes Received: 23,735
  Trophy Points: 280
  Mmh ota mwozowe!.
   
 6. z

  zuri Member

  #6
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 59
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unasema redioni ama kwenye Radio? It is a genuine question?
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Kuna tangazo fulani la biashara mara baada ya kutangazwa wanamalizia tangazo hili " limesababishwa na ...." . Ajabu na kweli tangazo limisababishwa na ........au limeletwa kwetu na .........

  BAKITA waamke na kuchukua hatua
   
 8. De Javu

  De Javu JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2011
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 266
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa uono wangu matatizo yanaanzia kwenye hivyo vyuo wanavyosomea hawa waandishi/watangazaji halafu kuna huku kuajiriana kwa kujuana. Mtangazaji/mwandishi lazima awe amehitimu na kufikia kiwango kinachokubalika, wengi wao wanaonekana wanafanya hizi kazi wakiwa hawana sifa za kua watangazaji/waandishi; lugha zao wanazotumia ni zile za mitaani tu. Hapa inatakiwa wizara husika/Baraza la kiswahili pamoja vyombo vinavyohusika kuwa "serious" na hili.
   
 9. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Kuna mjomba hapo juu(nimeshindwa kumnukuu) amegusia suala la Kitivo cha Kiswahili cha Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Jamani, tusiwe tunadandia vitu bila kujua undani wake. Pale Chuo Kikuu kuna Taasisi ya Taaluma za Kiswahili(iliyokuwa TUKI) ambayo moja ya kazi zake ni kufanya tafiti za Kiswahili pamoja na kufundisha Kiswahili kwa wanafunzi wa UDSM. Nina mashaka kama Mkuu Choveki anamfahamu hata mhusika mmoja wa TATAKI, hata akafikia hitimisho kuwa wataalam wetu hawajui lugha. Wataalam hao ndio walioaminiwa na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo(kupitia BAKITA) na kupewa dhamana ya kuandika Kamusi ya Kiswahili Sanifu(toleo la kwanza:1984), ambayo ndio inayotumika kokote duniani kunakofundishwa Kiswahili, achilia mbali machapisho zaidi mengi ambayo yamekuwa yakichapwa na TUKI tangu 1930(ikijulikana kama East Africa Language Commitee). Kwa hiyo watu kama Prof. Hursklainen(Ujerumani), F. Topan(Uingereza), Prof. Peter Massamba(Kenya) na wengine wengi walikosea sana kuleta miswada yao kuhakikiwa TUKI na wasiojua tofauti ya mazingara na mazingira. Uwe ukifikiri kabla ya kuhusisha watu wasiohusika na pumba zako!
   
Loading...