Naomba ufafanuzi wa masuala ya uchumi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba ufafanuzi wa masuala ya uchumi

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mtazamaji, May 11, 2010.

 1. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  kwenye habari za kimatafita nimekuwa nikisikia Ugiriki ilikaribia KUFILISIKA( BANKCRUPCY). Ujerumani ikaingia kuokoa jahazi.
  Je wataalamu wanaweza kunieilewesha kwa lugha nyepesi nini sababu ya taifa kufilisika ??na na nini maana na maneno kama BUDGET DEFICiT( Nakisi ya bajet) . Uhusiano wa mambo kama govermnent spending/ borrowing na economic health ya nchi na thamani ya pesa ya nchi na masuala mengine yanyofanana na hayo ili nipate mwanga kwenye hizi termilogy za kiuchumi.


  Naamini japo kaelimu ka haya masuala kidogo kanaweza kunipa mwanga wa kuchambua bajeti yetu inayokaribia kiundani zaidi.

  Natanguliza shukrani.
   
 2. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Taifa linafilisika kutokana na kushindwa kulipa madeni yake, ndio situation iliyoikuta Greece medeni mengi kuliko uwezo wa kulipa.

  Budget deficit ni pale matumizi yanapozidi makusanyo.

  Maswali yako ya mwisho ni complex sana, sidhani kama inawezekana kuielezea kwa ukamilifu hapa. Cheki Wikipedia au google kwa ujumla.
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Aksante sana mkuu kwa maelezo yako nimecheki lakini bado sijaelwa vizuri.
  kwa maana hiyo ikija list ya mataifa maskini zaidi duniani leo hii ugiriki itakuwemo huku tuliko sisi wa 3dr world? kama sio kwa nn ugiriki isiwe ni nchi masikini zaidi duniani ?

  Hii matumizi kuzidi makusanyo (deficit) nimeshangaa kusoma na kusikia kumbe hata UK,USA, etc na wale waliondelea nao matumizi yao yanazidi makusanyo. sasa hizo hela wanazotupa misaada ku finace majeshi yao wanatoa wapi? kwa jibu langu haraka kichwani nikahisi labda wanajichapia tu noti zao kuziba hiyo deficit lakini nikajiuliza mbona thamani za hela zao ziko juuu.

  Je Buddget deficit yetu tanzania ikoje leo hii? ilikuwaje miaka sita iliyopita ? inapungua au inaongezeka? Je Inawezekana mataifa yetu yalishafilisika zamani?
   
 4. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu maswali mazuri. na mimi pia nasubiri majibu. Mtu atokee basi atuelezee.
   
 5. M

  MJM JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Budget deficit ni suala la makadirio tu hivyo inapofikia kwenye matumizi ni wakati wa kutumia akili na kuangalia cashflow. Kama hazina yao haia hela then kulingana na priorities walizoweka baadhi ya matumizi yasiyo ya lazima yanapunguzwa na hali ikiwa mbaya zaidi ndiyo wanatafuta contingent plan ili maisha yaweze kwenda mbele. Hii system siyo ya kutumia kwa nchi kama Tanzania ambako serikali yetu ni bora liende, kukuta kitu kisicho kwenye budget kimelipwa siyo jambo la ajabu na hata priorities mara nyingi zinakuwa driven kisiasa.

  Kiuchumi ni kosa kubwa sana kuchapa hela ili uweze kuziba budget deficit hadi ifikie very critical situation maana side effect ni inflation, nk. Ongezeko la fedha lazima li-match na kukua kwa uchumi siyo factor kama kupanga budget usiyoweza kuimudu.

  Lakini hili suala la ugiriki limenikumbusha kauli ya nyerere "hawa wazungu hawana dhamira ya dhati ya kuziendeleza nchi maskini" hivi angalia pledge ya Ujerumani na uangalie huo ni msaada wa Africa kwa miaka mingapi. Pamoja na kwamba sisi hatuombi msaada bali wanatakiwa kurudisha kile walichotuibia kipindi cha Ukoloni na wanachoendelea kutuibia kwa ukoloni mamboleo
   
 6. k

  kioja Member

  #6
  May 11, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  BANKRUPTCY na UGIRIKI.

  Mmh. Ninavyojua unafilisika baada ya kushindwa kulipa madeni uliyokopa. Nadhani hawa Wagiriki walikopa sana na mapato ya serikali pamoja na akiba zake zilishindwa kulipa madeni ya nchi.

  Kumbuka pia Ugiriki imo ndani ya 'euro' na ni mwanachama wa EEC. Kwamfano hawawezi kuamuru kuchapwa kwa pesa zaidi kama vile nchi nyingine zinazotumia sarafu zao wenyewe. Kufilisika kwao kungewavuta wanachama wengine wa euro kuathirika kiuchumi. That's why EEC finance ministers came up with a rescue package announced recently.

  Kama ni mtu binafsi au Kampuni la kibiashara, unapofilisika utaratibu ni kuuzwa mali zako zilizobaki kulipia madeni. Kampuni hufa au hununuliwa. Kivumbi inakuwaje nchi inapofilisika?
   
 7. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu nimejiuliza haya maswali sana nikahisi inawezekana taifa kama tanzania kwenye accout za kimataifa linahesabika lilishafilisika siku nyingi.

  Vile Na hivi bajeti yetu Tanzania inakaribi tutasikia terminology nyingi za BOT wiazara fedha na mipango lakini nadhani knowlenge ya uchumi na mambo ya finace japo kidogo ingeingizwa kwenye masomo ya URAIA.
   
 8. b

  bnhai JF-Expert Member

  #8
  May 12, 2010
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Taifa la Tanzania haliwezi kufilisika maana halijawahi kuwa taifa tajiri yanayofilisika ni mataifa tajiri. Ukifikiria kwenye micro level utaona kwamba watu matajiri ndio hufilisika na si masikini.
  Labda na mie niongeze kidogo kwa hali ya Ugiriki. Mwishoni mwa miaka ya 1990, Ugiriki ilikuwa ni miongoni mwa mataifa tajiri 30 kutokana na takwimu za vyanzo mbalimbali. Lakini kilichotokea Taifa liliingia kwenye masuala ya rushwa na misukosuko ya kiasiasa. Lakini haya wakati yanatokea, taifa halikuwa na uwezo wa kucontrol hali hii. Maana Ugiriki kama miongoni mwa nchi zinazotumia sarafu ya ulaya haikuwa na uwezo wowote wa kuweka hali sawa. Lakini sasa, walichokuwa wanafanya ni kutoa taarifa za uongo za uchumi juu ya hali ya hiyo wakitumai wangeweza kuikabili kimyakimya. Lakini pia kumbuka kuwa ni wakati huo huo, Taifa lilikuwa kwenye mpito wa uchaguzi kwa hiyo hali ikazidi kuwa tete na ndipo hapo sasa wakajikuta wakivuka baadhi ya tergets za jumuiya ya Ulaya. Jumuia ya Ulaya huwa inatarget kwenye issue mbalimbali km inflation, uwiano wa deni la Taifa na GDP na pia nakisi ya bajet.
  Baada ya kukumbwa na hali hiyo, inamaana mahitaji ya nchi yakawa makubwa tayari wananakisi sasa watafanyaje? Wakienda kwenye masoko ya fedha, dhamana zao zikawa haziattract wateja kutokana na possibility ya kudefault kwa maana hiyo inabidi wauze kwa interest kubwa. Lakini pamoja na hiyo investors walikuwa cautious na hali hiyo.
  Baya zaidi liliwamaliza ni baada ya credit argents kudowngrade uwezo wa kulipa madeni kwa hiyo ikawa signal kwamba nchi inadondoka. Lakini lingine zaidi ni kuwa Umoja wa Ulaya ulisuasua mno kuchukua hatua kutokana na uchaguzi uliokuwepo Ujerumani (Kumbuka hili ndiyo Taifa lenye nguvu) na misukosuko ya siku nyingi ya kisiasa kati ya Ujerumani na Ugiriki.
  Kifupi sasa kwenye swali lako ni kuwa Ugiriki ilikuwa na matatizo makubwa ya nakisi ya bajeti na uwiano mkubwa kulinganisha na target ya EU pamoja na wanachama wengine wa Taifa hilo. Pia trend ya Ugiriki ilikuwa inaonyesha ni taifa linalodidimia kila asubuhi.
   
 9. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #9
  May 12, 2010
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Kwa kuongezea tu kama wasingekuwa katika sarafu ya pamoja Wagiriki uwezekano wa wagiriki kuwa katika matatizo haya ungekuwa ni mdogo mno maana kihistoria wamekuwa na matatizo makubwa ya kuweka matumizi na mapato katika uwiano na huko nyuma wao hawakuwa na hiyana katika kuchapisha pesa zaidi ili kufidia mapungufu ila sarafu ya pamoja imemaanisha wameiachia Banki Kuu ya Umoja wa Ulaya sera zote za kifedha hivyo kuwawia vigumu wao wenyewe kutumia zana hii kujinasua kipindi hiki.

  Matatizo kama haya huzikumba nchi nyingi ambazo hazina mifumo imara ya uchumi kama washirika wake katika muungano wa sarafu na ndio maana ECB wametenga kabisa fungu la kusaidia nchi nyingine kama Uhispania, Ureno na Jamnhuri ya Ireland ambazo zinaonyesha dalili ya kufuata mkondo wa Ugiriki.
   
 10. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuuu am not a mchumi lakini kwa logic ya kawaida hata msikini anafilisika. therwse kuflisika kwa ugirikii isingewua issue sababu ndani ya EU ugiriki nadhani ni chovu kuchumi.
   
 11. Kitope

  Kitope JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Dah Mkuu vumilia tu! hayo maswali yako yanahitaji mtu awe na muda wa kuchanganua 1 mpaka 100 kabla hajakuelewesha a-z. kwa ufupi mgiriki kuna mambo alichanganya hasa katika mikopo aliyokuwa nayo! na kuungua kwake ilikuwa sio mgiriki tu kutumbukia shimoni, bali mataifa mengi yaliyomo katika EU yangeathirika ama yameathirika kwa kiwango flani mpaka sasa. na ndio maana ya mataifa mengine kuingilia kati greece na kujaribu kuzima moto kabla haujasambaa. kuhusu misaada wanayotuma pia, hiyo kwa watu kama sisi tunachekelea sana tunapigwa jeki lakini kiuchumi wao hawawezi ku survive either kama hiyo misaada haiji huku. unaweza kutoa macho kwa hili lakini kama nilivyosema hapo juu 1 mpaka 100 ili kupata A-Z.
  Ntarudi.....
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tajiri hufilisika kutokana na mali alizo nazo kutowiana katika matumizi na mapato, yaana matumizi kuwa juu zaidi kuliko mapato, na tena uzalishaji kuwa chini ya matumizi, matokeo yake kuwa na madeni makubwa yasiyoweza kulipika, gape hiyo humfikisha tajiri kiwango cha kuwa bankrupt, yaani kufilisika. Maskini hana hali hiyo kwani anachochuma ndicho anachokula, hapa hata uwiano wake kiuchumi huwa mgumu kupima ndio maana anawekwa tu kwenye jedwali la umaskini.

  Mfano mfanyakazi vigumu kumwambia anafilisika kwa kuwa pato lake ni lilelike kila siku na hata atumie asitumia inahesabika pato lake linaeleweka, ingawa kwa nchi zilizoendelea hupimwa pia fixed asserts na hata bank asserts jambo ambalo kwa nchi maskini kama Tanzania hatuna system kama hiyo. Kwa utaratibu huu vigumu kumwona mtu wa kiwango cha kati na chini hasa watumishi au wakulima kuona kama wanafilisika,hali kadhalika kwa mwono kama huo nchi maskini hupimwa tu ukuaji wa uchumi wake na hueleweka tu kama nchi maskini.

  Tajiri au mfanya biashara ana capital na asserts, kwa mfumo wa kiuchumi kuna kupima uwiano wa mapato na matumizi yake, na ili awe na uchumi mzuri wenye kuimarika anatakiwa mapato yawe juu kuliko matumizi. Lakini matumizi yanapopita mapato ni kuanguka kwa uchumi wake na ndiyo safari ya kufilisika. Huo ni mchanganuo wa tofauti aliyojaribu kusema mdau hapo juu kwamba maskini vigumu kusema amefilisika tofauti na tajiri.

  Mimi si mchumi ila ni mtazamo wangu tu kutokana na uzoefu wa maisha na uchunguzi wangu katika maisha ya kila siku.
   
Loading...