Naomba ufafanuzi maana ya Uchumi wa Kati

Wajumbe

Senior Member
Jul 26, 2020
136
379
Wajuzi naomba mwenye utaalamu wa masuala ya uchumi atupe maana ya uchumi wa kati, maana nachanganyikiwa. Benki ya Dunia imesema tumeshaingia kwenye uchumi wa kati, Kikwete amesema uchumi wa kati uliopangwa na Mkapa wa 2025 ni kufikia wastani wa kipato cha dola 3,000 kwa kila mwananchi.

Baadaye akasema kilichofikiwa na Tanzania ni kipato cha dola 1,000. Ndugu zetu wataalam wa uchumi, hebu mtutoe tongotongo sisi Wajumbe
 
Uchumi ulipanda Wakati wa Rais Mkapa na Kikwete na ukashuka awamu ya tano! Lake ni tunaambiwa waliotupeleka kweye uchumi wa kati ni awamu hii! Unaonaje hilo?
 
Uchumi wa Kati yaani middle income ni uchumi ambao unaweza kumlipa kila mwananchi wake Pati la dola 1006 mpaka dola 3955 kwa mwaka. Sisi Tz tuko dola 1008 kwa mwaka kwa hiyo tumevuka tu kwa dola Mbili tu. Ina maana tuko bado uchumi wa chini sana kwenye daraja la pili au uchumi wa kati. Mkapa alitaka tufikie ngazi ya juu ya uchumi wa kati kabla hawajatutangaza. Kuna nchi huwa zinakataa Kuingia daraja la pili kama wako ngazi ya chini kama yetu kwa sababu misaada inapunguzwa nchi ikiingia uchumi wa pili au wa tatu. Ndiyo maana wenye kujua hawashangilii sana hilo.
 
Kasome darasani huko utaelewa, au ulisoma UDOM wewe, ninyi ndio mnajifanya waelewa kumbe kichwani zidaduye. Hazimo mweeeeeeeeee,
 
Kasome darasani huko utaelewa, au ulisoma UDOM wewe, ninyi ndio mnajifanya waelewa kumbe kichwani zidaduye. Hazimo mweeeeeeeeee,
 
Sisi bado hatujaingia kwenye nchi za uchumi wa kati bali tumetoka kwenye nchi za uchumi wa chini daraja la chini hadi nchi zenye uchumi wa chini daraja la kati( low middle income) uchumi wa kati bado safari ni ndefu sana
 
Uchumi wa Kati yaani middle income ni uchumi ambao unaweza kumlipa kila mwananchi wake Pati la dola 1006 mpaka dola 3955 kwa mwaka. Sisi Tz tuko dola 1008 kwa mwaka kwa hiyo tumevuka tu kwa dola Mbili tu. Ina maana tuko bado uchumi wa chini sana kwenye daraja la pili au uchumi wa kati. Mkapa alitaka tufikie ngazi ya juu ya uchumi wa kati kabla hawajatutangaza. Kuna nchi huwa zinakataa Kuingia daraja la pili kama wako ngazi ya chini kama yetu kwa sababu misaada inapunguzwa nchi ikiingia uchumi wa pili au wa tatu. Ndiyo maana wenye kujua hawashangilii sana hilo.
Kwahiyo kumbe Awamu hii imebembeleza tuingizwe tu huku tuko chini ili wapate ujiko wa uongo siyo ?
 
Wajuzi naomba mwenye utaalamu wa masuala ya uchumi atupe maana ya uchumi wa kati, maana nachanganyikiwa. Benki ya Dunia imesema tumeshaingia kwenye uchumi wa kati, Kikwete amesema uchumi wa kati uliopangwa na Mkapa wa 2025 ni kufikia wastani wa kipato cha dola 3,000 kwa kila mwananchi. Baadae akasema kilichofikiwa na Tanzania ni kipato cha dola 1,000. Ndugu zetu wataalam wa uchumi, hebu mtutoe tongo tongo sisi Wajumbe
nimefurahishwa sana na jina lako
 
Njoo kwetu Tz ujionee mwenyewe jinsi tunatamba kwenye "Uchumi wa kati". Havielezeki kwa keyboard bali kwa macho. Yaani hadi raha. Mireli ya umeme, mibwa mikubwa ya kuzalisha umeme hadi black out itakuwa ni historia. Midege hadi mingine inarushwa tu bila waatu na ukiingia ndani uji selfishe utakavyo. Kwa kifupi, huo ndo uchumi wa kati
 
Uchumi wakati maana yake ni KUWA NA KITAMBI KIKUBWA HALAFU MIGUU MYEMBAMBA KAMA CHELEWA.
 
Wajuzi naomba mwenye utaalamu wa masuala ya uchumi atupe maana ya uchumi wa kati, maana nachanganyikiwa. Benki ya Dunia imesema tumeshaingia kwenye uchumi wa kati, Kikwete amesema uchumi wa kati uliopangwa na Mkapa wa 2025 ni kufikia wastani wa kipato cha dola 3,000 kwa kila mwananchi. Baadae akasema kilichofikiwa na Tanzania ni kipato cha dola 1,000. Ndugu zetu wataalam wa uchumi, hebu mtutoe tongo tongo sisi Wajumbe

1.Bank ya dunia inazungumiza kuhusu sisi kuwa "lower middle income country."
2. Tanzania -sisi uongozi wa nchi yetu wanazungumzia kuhusu "middle income country" pekee.

lower middle income country maana yake sisi bado ni maskini hohehahe- yaani bado tunakinga bakuri kama the late Matonya.
Middle income country ndio hiyo ya dola 3000 aliyokuwa anazungumzia mzee wa Bagamoyo mstaafu Kikwete leo; maana yake ni kwamba, the late Matonya amebadirisha makazi, kutoka Dodoma, kwenda Mwanza na Dar- Es- salaam, lakini bakuri bado kukinga ni pale pale ...

Nafikili umepata mwangaza kidogo...
 
Back
Top Bottom