Naomba ufafanuzi katika hili kuhusu vifaranga vya Bata

Raia Mtata

JF-Expert Member
Feb 4, 2017
315
592
Habari zenu humu ndani.

Kutokana na changamoto za ufugaji wa hawa bata wadogo na matokeo ya vifo vya mara kwa mara, kuna kitu nahitaji kufahamu.

Je ni muda gani ambao hawa vifaranga wa bata watakuwa wamekomaa na kupona kwenye umauti? Wiki 2 au 3 au mwezi au miezi miwili baada ya kuzaliwa?
 
Dhana ya kwamba vifaranga wa Bata lazima wafe sio ya kweli, walishe vifaranga wa Bata chakula cha vifaranga(starter).Kwenye maji yao ya kunywa wawekee dawa za malt vitamin zinauzwa kwenye maduka ya mifugo.Achana na habari za kuwanyonga shingo unawaumiza bure kinachowauwa viranga wa bata ni ukosefu wa madini na vitamini
 
Hivi nikifuga bata wa kawaida lazima niwatengenezee sehemu yao ya kucheza maji?maana huwa naina huku mtaani bata wanapenda sana kucheza kwenye maji
 
Mwezi lakini kuna kitu nilijifunza. Mara nyingi vifaranga hufa kwa kujinyonga nyonga shingo hadi kufa. Kama hufa kwa shida hiyo badilisha uzazi. Yaani mfano bata waliototolewa litoe dume na libadili weka dume lingine kabisa lisilozaliwa kwenye uzao huo utaona matokeo hiyo shida haitakuwepo
 
Hivi nikifuga bata wa kawaida lazima niwatengenezee sehemu yao ya kucheza maji?maana huwa naina huku mtaani bata wanapenda sana kucheza kwenye maji
Huwa na muhimu kwasababu huwa ni moja ya tabia yake ya kupunguza joto kupitia kuoga kwenye maji pia hata kama kuna wadudu baadhi mwilini huwatoa kupitia njia hiyo. Cha muhimu ni kumbadilishia maji kila siku na kumuwekea maji safi.
 
Sawa
 
Dhana ya kwamba vifaranga wa Bata lazima wafe sio ya kweli, walishe vifaranga wa Bata chakula cha vifaranga(starter).Kwenye maji yao ya kunywa wawekee dawa za malt vitamin zinauzwa kwenye maduka ya mifugo.Achana na habari za kuwanyonga shingo unawaumiza bure kinachowauwa viranga wa bata ni ukosefu wa madini na vitamini
Well said. Vifaranga vya bata vilelewe kwa kupewa chick starter (hasa broiler starter) kwa mwezi mmoja au miwili. Kuna jirani yangu yeye huwachanganya na vifaranga wa kuku (japo anakosea) tangu day one wanaanguliwa na wanakua wote. Kipe wanachokula wale kuku ndiyo na bata wanakula pia. Pia huwapa huduma zingine sanjari na vifaranga wa kuku. Mf. Vitamin, etc
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom