Inahitajika Noah kwaajili ya kukodi kwenye ofisi

Zemanda

JF-Expert Member
Jan 10, 2021
5,707
11,960
Habari zenu wajumbe.

Inahitajika gari aina ya Noah, ikiwa NOAH box itakuwa poa sana kwaajiri ya matumizi ya kuzungusha wafanyakazi vituo vya kazi siku za kazi kuanzia jumatatu hadi jumamosi.

Gari inatakiwa kukidhi vigezo vifuatavyo:

1. Iwe kwenye hali nzuri kwa maana isiwe spana mkononi.

2. Iwe katika hali ya umaridadi kimuonekano isiwe chakavu hadi inakosa mvuto iwe katika rangi nzuri na isiwe na uchakavu wa bodi.

3. Iwe imekatiwa bima kubwa na kama haina then mazungumzo yapo kati ya m'miliki wa gari na kampuni ili kujua nani atawajibika na swala la bima. Isiwe na Vimeo kwa maana ya tiketi za madeni ya makosa ya barabarani kama vipo pia utaratibu wa mauzungumzo ya nani atabeba mzigo na kuwajibika nao kwa utaratibu upi yatafanyika.

4. Mwenye gari awe tayari kusign mkataba ambao utaridhia usalama wa mali yake na matumizi yake na kusimamia makubaliano bila kuleta hitilafu kwenye kazi za kampuni.

5. Gharama za service ya gari zitakuwa ni sehemu ya gharama za kampuni hivyo m'miliki atatakiwa kupewa ripoti ya service ya gari mara kwa mara.

6. Baada ya makubaliano mmiliki na kampuni watakubaliana namna ya uwasilishaji wa malipo yaani kama ni kwa siku, wiki, mwezi, robo mwaka yaani miezi mitatu mitatu, nusu mwaka yaani miezi sita sita au mwaka kamili yaani miezi 12.

Kwa maelezo zaidi naomba uje inbox kwa ufafanuzi zaidi.
 
Habari zenu wajumbe.

Inahitajika gari aina ya Noah, ikiwa NOAH box itakuwa poa sana kwaajiri ya matumizi ya kuzungusha wafanyakazi vituo vya kazi siku za kazi kuanzia jumatatu hadi jumamosi.

Gari inatakiwa kukidhi vigezo vifuatavyo:

1. Iwe kwenye hali nzuri kwa maana isiwe spana mkononi.

2. Iwe katika hali ya umaridadi kimuonekano isiwe chakavu hadi inakosa mvuto iwe katika rangi nzuri na isiwe na uchakavu wa bodi.

3. Iwe imekatiwa bima kubwa na kama haina then mazungumzo yapo kati ya m'miliki wa gari na kampuni ili kujua nani atawajibika na swala la bima. Isiwe na Vimeo kwa maana ya tiketi za madeni ya makosa ya barabarani kama vipo pia utaratibu wa mauzungumzo ya nani atabeba mzigo na kuwajibika nao kwa utaratibu upi yatafanyika.

4. Mwenye gari awe tayari kusign mkataba ambao utaridhia usalama wa mali yake na matumizi yake na kusimamia makubaliano bila kuleta hitilafu kwenye kazi za kampuni.

5. Gharama za service ya gari zitakuwa ni sehemu ya gharama za kampuni hivyo m'miliki atatakiwa kupewa ripoti ya service ya gari mara kwa mara.

6. Baada ya makubaliano m'miliki na kampuni watakubaliana namna ya uwasilishaji wa malipo yaani kama ni kwa siku, wiki, mwezi, robo mwaka yaani miezi mitatu mitatu, nusu mwaka yaani miezi sita sita au mwaka kamili yaani miezi 12.

Kwa maelezo zaidi naomba uje inbox kwa ufafanuzi zaidi.
Kwanini msinunue tu
 
Asante kwa Bandiko Mkuu.

WENYE MAGARI YA NOAH WANAKUJA KWA KASI YA 5G (USIONDOKE).

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Nipo hapa nasubiria maboss zangu wanicheki tupeane maokoto. Umasikini lazima tuupige vita.
 
Mbona ujasema kwa siku shingp unatoa au pesa unalipije
Hapo ndipo makubaliano ya mkataba wa kazi yanapoingia. Si unajua hatuwezi weka kila kitu wazi wazi hapa inakuwa haijakaa sawa.
 
Kwanini msinunue tu
Kwa baadae tutanunua ila kwa sasa inatulazimu kutumia ya kukodi. Kama kuna mtu ana gari yake haitumii imepaki tu nadhani ni busara kuikodi ili isiwe ipo idle tu imepaki.
 
  • Thanks
Reactions: BRN

Similar Discussions

Back
Top Bottom