Naomba ufafanunuzi juu ya kisa cha tajiri na yesu(luka 18:18-27)

Ukisoma katika luka 18:18-27 kuna kisa cha kijana tajiri na yesu. Kijana anataka kuingia katika ufalme wa mungu na kazishika amri zote tangu utoto wake. Lakini yesu anamwambia ili aupate ufalme wa mungu basi auze mali zake zote na kuwagawia maskini kisha amfuate. Kijana anaondoka kwa masikitiko kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

maswali yangu,
je, matajiri hawataurithi ufalme wa mungu kwa sababu ya mali zao?

definition ya utajiri hapo ni ipi??
Kwa sababu kila mtu kuna kitu kamzidi mtu mwingine, je na mimi niuze nyumba,gari au hata hii simu niliyonayo ili nikamsaidie asiye na vitu hivyo ili niingie kwenye ufalme wa mungu??

mwishoni yesu aliposema kwa mwanadamu hayawezekani bali kwa mungu yanawezekana alikuwa na maana gani?,
Matajiri wako ambazo wataurithi ufalme wa Mungu ,sababu ya Yesu kumwambia vile sio kwamba Yesu hapendi matajiri Wanafunzi waYesu walikuwa matajiri Sana,sababu ni kiroho alimuona mtu Yule anapenda Mali zake kuliko kumpenda Mungu ndio mana alisema vile ila watu waMungu ni matajiri, kumpenda Mungu kunatakiwa kuzid kumpenda malizako au chochote ulicho nacho, soma Ibrahim alivyomtoa isaka kuonyesha mwana si kitu Zaid ya Mungu utajiri wake ukizid Sana alikuwa tajiri Sana Kwa Yesu kuna utajiri Sana
 
Ukisoma katika luka 18:18-27 kuna kisa cha kijana tajiri na yesu. Kijana anataka kuingia katika ufalme wa mungu na kazishika amri zote tangu utoto wake. Lakini yesu anamwambia ili aupate ufalme wa mungu basi auze mali zake zote na kuwagawia maskini kisha amfuate. Kijana anaondoka kwa masikitiko kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

maswali yangu,
je, matajiri hawataurithi ufalme wa mungu kwa sababu ya mali zao?

definition ya utajiri hapo ni ipi??
Kwa sababu kila mtu kuna kitu kamzidi mtu mwingine, je na mimi niuze nyumba,gari au hata hii simu niliyonayo ili nikamsaidie asiye na vitu hivyo ili niingie kwenye ufalme wa mungu??

mwishoni yesu aliposema kwa mwanadamu hayawezekani bali kwa mungu yanawezekana alikuwa na maana gani?,
Hapo Yesu alimwambia hivyo ili kupima moyo wake upo wapi?Kuwa tajiri sio shida shida ni kuufanya utajiri ukae moyoni na sio Mungu.

Kumbuka Mungu anataka yeye pekee ndio ake moyoni mwako

Mithali 23
26 Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu.

Kwahio Yesu alijua kabisa huyu ana mali nyingi na ndipo moyo wake ulipo na hivyo alimpa jaribu ambalo angeshinda basi angekuwa na vigezo vya kuurithi ufalme wa mbinguni.

Mathayo 6
20 bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;

21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.

Kuna mdau katoa mfano wa Ibrahim pale juu,Mungu alimjaribu Ibrahim kwamba amtolee mwanawe wa Pekee Isaka, Kumbuka Ibrahim amempata Isaka Uzeeni tena ni Mungu huyohuyo ndiye aliyempa kwahio sio kwamba Mungu alikuwa na shida na Isaka hapana ila alitaka aone Je Ibrahim moyo wake wote bado uko kwake au kuna sehemu ya moyo amehamishia kwa Isaka baada ya kumpata? aliposhinda jaribu hilo ndio Mungu akajua kuwa huyu moyo wake wote uko kwangu ndio ukaona akatokea kondoo wa sadaka.

Hata wanafunzi wake, akina Petro waliposikia yale majibu nao walishtuka maana hata wao waliacha yote wakamfuata yeye ikabidi waulize watafaidika nini ndipo akawajibu kwamba watapokea mara nyingi zaidi ya vitu walivyoacha katika ulimwengu huu wanaoishi na ule ujao(ufalme wa mbinguni).

Luka 18
28 Petro akasema, Tazama, sisi tumeviacha vitu vyetu vyote na kukufuata.

29 Akawaambia, Hakika nawaambia, hakuna mtu aliyeacha nyumba, au mke, au ndugu, au wazazi, au wana, kwa ajili ya ufalme wa Mungu,

30 asiyepokea zaidi mara nyingi katika zamani hizi, na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.

Kwahio kuwa na mali sio tatizo ila chunga sana mali zisitawale moyo wako bali Mungu pekee,maana Biblia inasema kwamba huwezi kutumikia mabwana wawili yaani mali na Mungu kuna mmoja utamdharau tu.

Mathayo 6
24 Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.

Kwahiyo hata huyu mtu baada ya kuambiwa kauze mali zako uwagawie masikini yeye aliishia kusononeka na kuondoka kwa sababu mali kwake ndio kila kitu,kama angemjibu Yesu kwamba ngoja nikauze kwa moyo mmoja huenda angeuza lakini akapata mara nyingi zaidi au wakati anaanza tu mchakato wa kuuza huenda Yesu angemwambia nifuate maana angeona utayari wa moyo wake.

Kwahio hata katika maisha ya kawaida usipende kuweka watu au vitu moyoni kwa sababu moyoni ndipo zitokako chemchem za uzima,hicho kitu ulichoweka moyoni kikipata tatizo mfano gari nyumba ikiungua au mtu kakusaliti au kakuacha ndio unasikia mtu kapata presha ya moyo,kisukari,stroke au kufa kabisa.

Mithali 4
23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

Aliposema kwa binadamu hayawezekani ila kwa Mungu yote yanawezakana ni baada ya watu wa pembeni kusikia hayo majibu ya Yesu aliyomjibu huyo kijana.

Luka 18
26 Nao waliosikia walisema, Ni nani basi awezaye kuokoka?

Kwamba kama imani yako na moyo wako wote vyote viko kwa Mungu basi kupitia yeye hata ukiwa tajiri kuokoka kunawezekana tu.
 
Kama ni hivyo ni kwa nini wakristo leo wasiuze mali zao zote wamfuate yesu kama agizo la yesu lilivyomtaka yule tajiri ili kuonesha hawatumainii mali zao?

Wauze Mali zao ili waishije?

Kile alichoambiwa huyo Tajiri ni Mtihani tuu.
Ni Kama Ibrahim alivyoambiwa amtoe kafara mwanaye wa pekee.
Ulikuwa ni mtihani.

Elewa shabaha ya mtihani,
Ukisoma mtihani lazima ufikiri beyond
 
... wanameza na kutenda neno kwa neno wakijisahaulisha kwamba, pasi na mifano Bwana hakufundisha.
 
Binadamu tuna ishi kwenye dunia mbili ya kwanza Dunia ya Kimwili ya pili Dunia ya Kiroho.
Katika Dunia hizi Mbili Utajiri unatakiwa hili kuweza ishu na kutumikia Mungu na Jirani zetu.
Hapa kijana alikuwa anaambiwa kuuza mali zake zote zile za Kiroho kama vile majivuno, Uchoyo, Roho mbaya ili aweze mtumikia Mungu wake kikamilifu. Aingii akili kuwa auze Mifugo, Mashamba n.k ili aweze mtumikia Mungu wakati Mungu uwabariki watu wake kwa Utajiri wa mali mbalimbali zikiwemo Mifugo mashamba na mengineyo
Alikuwa auze hivyo vyote agawie maskini!?
 
kumbe hata ukizishika amri zote upo uwezekano mbinguni usiingie.

mimi nilijua ndani ya amri kumi ndio zimebeba vigezo vyote vya kuingia mbinguni"

na jamaa alimhakikishia YESU' kua amezishika tokea utotoni ndio maana alijibu kwa uhakika .

kama ingekuwepo kuna hata amri moja aliyoivunja toka utotoni hadi muda ule anahojiana na YESU" angeambiwa amri fulani bado"

lakini akajibiwa kitu kingine kabisa.
 
Ukisoma katika luka 18:18-27 kuna kisa cha kijana tajiri na yesu. Kijana anataka kuingia katika ufalme wa mungu na kazishika amri zote tangu utoto wake. Lakini yesu anamwambia ili aupate ufalme wa mungu basi auze mali zake zote na kuwagawia maskini kisha amfuate. Kijana anaondoka kwa masikitiko kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

maswali yangu,
je, matajiri hawataurithi ufalme wa mungu kwa sababu ya mali zao?

definition ya utajiri hapo ni ipi??
Kwa sababu kila mtu kuna kitu kamzidi mtu mwingine, je na mimi niuze nyumba,gari au hata hii simu niliyonayo ili nikamsaidie asiye na vitu hivyo ili niingie kwenye ufalme wa mungu??

mwishoni yesu aliposema kwa mwanadamu hayawezekani bali kwa mungu yanawezekana alikuwa na maana gani?,
Tajiri aliuliza afanye nini apate kuurithi ufalme wa Mungu . Kwa kuwa alikua kashika amri zote Yesu anamwambia kapungukiwa kitu kimoja??? Ni nini hichi??

Nadhani point ya msingi haikuwa kuhusu utajiri au umaskini . Tunaona tajiri alipewa choice achague kati ya ufalme wa Mungu na Mali zake na akachagua mali zake japo kwa huzuni.

Nadhani kuuza mali na kugawia maskini halikua jambo la msingi katika hii story ila ni jee ukipewa uchague kati ya mali na ufalme wa Mungu ni nini ungechagua?

Kwa hiyo naona alichopungukiwa tajiri sio kuwa alikua na mali nyingi na hakuuza kuwapa maskini ila ni kwamba alipenda mali kuliko Mungu na akachagua Mali kuliko ufalme wa Mungu.
 
kumbe hata ukizishika amri zote upo uwezekano mbinguni usiingie.

mimi nilijua ndani ya amri kumi ndio zimebeba vigezo vyote vya kuingia mbinguni"

na jamaa alimhakikishia YESU' kua amezishika tokea utotoni ndio maana alijibu kwa uhakika .

kama ingekuwepo kuna hata amri moja aliyoivunja toka utotoni hadi muda ule anahojiana na YESU" angeambiwa amri fulani bado"

lakini akajibiwa kitu kingine kabisa.
Mpende Bwana Mungu wako kwa roho yako yote na kwa nguvu zako zote. Mpende jirani yako kama unavyojioenda wewe mwenyewe. UPENDO ndio amri kuu; yule kijana tajiri hakuujua hilo ambalo ndio hasa mission ya Yesu duniani.
 
Back
Top Bottom