Naomba tujadili kwa undani kuhusu 'ukweli'

WAKUONDOKA

Member
Oct 8, 2014
46
24
Habari zenu waungwana,
Naomba mchango wa mawazo yenu kwanza mnisaidie kujua
1.UKWELI ni nn?
2.Tunajuaje kwamba hili jambo ni kweli kbsa?
3.Je tuna uhakika gani kinachozungumzwa ni kweli na..
•vyombo vya habari,
•vitabu vya dini,
•wale tunaowaamini
•Wale wanaosema wanakupenda ?
Mtume Paulo(kwa wale wakristo) alipata kusema 'Imani ni bayana ya mambo yasioonekana ni hakika ya mambo yatarajiwayo' kauli iyo bado inasadiki ukweli ni yy mwenyewe anaeujua.
Yesu pia alipata kusema 'mimi ndio njia ya uzima na kweli' hata kwa kauli bado inabeba madhila ya ukweli juu ya mzungumzaji mwenyewe.
Naomba mchango wenu wa mawazo hapo ili nipate kupata afya ya maarifa zaidi.
••••••••••••••nawasilisha hoja•••••••••••
 
kuna Truth na fact
hivi vitu lazima uvitofautishe kabla haujaanza kuchambua.

ndio maana wacommunist wanamsemo seek truth from facts.

ukimaliza hapo liingie suala la IMANI/FAITH na sio BELIEF.

Ukweli kwa maana Ya TRUTH, kila mtu huwa ni mkweli,
Ila kwa maana ya FACT hapo ni evidence based. Na vitu hivi viwili vinakuwa processed sehemu mbili tofauti kabisa katika Ubongo(Subconcious na concious mind)
Tuanzie hapo kwanza
 
Pata habari,gather info n facts then drop the conclusion ili kung'amua ukweli.

Yawezekana ukaambiwa "mtoto uliyenae sio damu yako"

Gather facts;

Utaanza na kuangalia tabia za mwanao ukilinganisha na zako na mama yake

Then utamuuliza mkeo juu ya ilo swala.

Mwisho kabisa utachukua vipimo vya DNA ambavyo vitakusaidia kudrop the conclusion.
 
kuna Truth na fact
hivi vitu lazima uvitofautishe kabla haujaanza kuchambua.

ndio maana wasocialist wanamsemo seek truth from facts.

ukimaliza hapo liingie suala la IMANI/FAITH na sio BELIEF.

Ukweli kwa maana Ya TRUTH, kila mtu huwa ni mkweli,
Ila kwa maana ya FACT hapo ni evidence based. Na vitu hivi viwili vinakuwa processed sehemu mbili tofauti kabisa katika Ubongo(Subconcious na concious mind)
Mkuu apo umenitoa tongotongo kwa kiasi kikubwa tuu thanx
 
ukweli hutafutwa kwa kuangalia ama kuhusianisha au kulinganisha nadharia na mazingira halisi
namna ya kutambua jambo au hoja au kitu fulani kuwa ni kweli kadri ya nadharia yake ni pamoja na :

kutumia vipimo vya kimaabara sawa na utafiti wa kisayansi.
kulinganisha na mazingira halisi kwa kuyachunguza
kutumia takwimu na tafiti za kihistoria kuhusu jambo au kitu fulani katika mazingira na nyakati mbali mbali.
 
Habari zenu waungwana,
Naomba mchango wa mawazo yenu kwanza mnisaidie kujua
1.UKWELI ni nn?
2.Tunajuaje kwamba hili jambo ni kweli kbsa?
3.Je tuna uhakika gani kinachozungumzwa ni kweli na..
•vyombo vya habari,
•vitabu vya dini,
•wale tunaowaamini
•Wale wanaosema wanakupenda ?
Mtume Paulo(kwa wale wakristo) alipata kusema 'Imani ni bayana ya mambo yasioonekana ni hakika ya mambo yatarajiwayo' kauli iyo bado inasadiki ukweli ni yy mwenyewe anaeujua.
Yesu pia alipata kusema 'mimi ndio njia ya uzima na kweli' hata kwa kauli bado inabeba madhila ya ukweli juu ya mzungumzaji mwenyewe.
Naomba mchango wenu wa mawazo hapo ili nipate kupata afya ya maarifa zaidi.
••••••••••••••nawasilisha hoja•••••••••••

Ukweli ni Ukweli na ukiwa mkweli kweli itakuweka huru! Kuwa mkweli na utayafurahia maisha japo ukweli unauma ila Ukweli utabaki kuwa Ukweli.
 
Pata habari,gather info n facts then drop the conclusion ili kung'amua ukweli.

Yawezekana ukaambiwa "mtoto uliyenae sio damu yako"

Gather facts;

Utaanza na kuangalia tabia za mwanao ukilinganisha na zako na mama yake

Then utamuuliza mkeo juu ya ilo swala.

Mwisho kabisa utachukua vipimo vya DNA ambavyo vitakusaidia kudrop the conclusion.

Mh!
 
Ukweli (truth) ni hakika ya jambo fulani ambalo linaweza kuwa sahihi au la,
Ikumbukwe kuwa ukweli(truth) umegawanyika sehemu kuu mbili:-
1. Ukweli kama ulivyo (objective truth), hii ni aina ya ukweli ambayo huwakilisha uhalisia wa jambo husika bila kuhusisha mitazamo (opinions) na hisia za watu, mara nyingi huu ukweli ndio hubeba maana halisi na thamani ya kitu kilivyo hivyo "ukweli kama ulivyo" uko katika vipimo vya kiasi na idadi (quantitative measurements) mfano watu 20, kalamu moja n.k

2. Ukweli kama unavyoonekana (subjective truth) huu ni ukweli ambao huwasilishwa na mtu kwa kuzingatia hisia na maoni bonafsi (opinions). Ukweli huu huwakilisha viwango vya ubora (qualitative measurements), mfano uzuri (beauty and aesthetics) uko machoni pa mtazamaji na hauwezi ukapimwa kwa vizio vyovyote vya kiasi.
Pia jiulize kuwa je kila uzungumzacho ni kile unachokiwaza? Na kama sivyo basi ukweli ni vigumu kuufikia. Ikumbukwe kuwa binadam huwasilisha taarifa kwa kutumia lugha iliyoundwa na maneno, hivyo wazo lililo akilini ndio MWAKILISHWA, lakini lugha au maneno ndio MWAKILISHI, je, mwakilishi anaweza kuwa sawa na mwakilishwa?

Dhana ya ukweli ni tata sana ndio maana hata taarifa au tukio moja linaweza kuripotiwa tofauti na hatimae kuondoa maana halisi hivyo ukweli kupotea,
Mfano, wewe uko Dar es salaam na una marafiki zako wako Singida (eneo moja) ukawapigia simu, mmoja akasema ni baridi sana lakini mwingine akasema kuna joto sana, je yupi ndio atakuwa anasema ukweli?
**Nawasilisha hii itakupa taswira na mwanga juu ya dhana ya ukweli**
 
Kuna YOUR truth, MY truth and THE TRUTH. kwetu sisi wakristo JESUS CHRIST is THE TRUTH........pia ni NJIA na UZIMA
 
Wakati tunasoma tuambiwa Objective truth kuwa sayari ziko 9. Sasa hivi tunaambiwa ziko more than 9. Hivyo objective or scientific truth sio THE TRUTH. Ukweli anaujua yule aiyeuumba. Kuna vitu ambavyo tulijidanganya with some current 'facts' ndio tukauita absolute truth.
 
Pata habari,gather info n facts then drop the conclusion ili kung'amua ukweli.

Yawezekana ukaambiwa "mtoto uliyenae sio damu yako"

Gather facts;

Utaanza na kuangalia tabia za mwanao ukilinganisha na zako na mama yake

Then utamuuliza mkeo juu ya ilo swala.

Mwisho kabisa utachukua vipimo vya DNA ambavyo vitakusaidia kudrop the conclusion.

mkuu embe cheki hy video kwa hzo fact ulizozitoa unfkr hyo jamaa hata akisema ukwel kma ulivyoona wanawez kumuani
Mi naona ukwel uliokamilka anaujuA mtu mwenyw
 
hahahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa ukweli wa miaka kumi unabadilika kuwa uwongo ndani ya dakika moja na unaweza kurudia tena hali yake ya ukweli pindi ikihitjika iwe hivyo
maaana naona hata hii historia tuisomayo ni itofauti na ile hali ilvyokuwa enz hizo ila kutokana na iman historia ya uwongo inakuja kuwa ukweli kwa wanajamii nahakuna ukweli utakuja kusemwa ukaja kuonekana ni ukweli
ajabu ni kua tofauti kati ya uwingo na ukwli ni ndogo mno ni kama tofauti kati ya mashariki na magharibi
mfano chukua dunia alafu igawe vipande vili kimoja kiwe mashariki nakingine kiwe magharibi itabaki hivyo maana hakutakuwa na kipnde cha kati ambacho kitaku neutral inamaana kama kungekuaa na hali ya kati na kati basi ingekua afadhali na ukiunganisha dunia kama kitu hakipo mashariki basi kiopo magharibi
na hii inamaana kuwa kama hautakua mouongo basi wewe ni mkweli
wecha nimquote mtu adhim alisema inatosha mtu kuwa muongo kwa kuongea kila anachokisikia
 
Back
Top Bottom