Malipo Ya Kugeuza Taarifa Za Kweli Kuwa Za Uongo

Malipo Ya Kugeuza Taarifa Za Kweli Kuwa Za Uongo

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,237
Reaction score
1,744
Mt 28:12-13 SUV
[12] Wakakusanyika pamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi, [13] wakisema, Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala.

Taarifa za kufufuka kwa YESU hazikupokelewa vizuri na watesi wa YESU, zilikuwa ni taarifa mbaya kwao.

Kutolewa kwa fungu la fedha nyingi kwa Askari waliokuwa wanalinda hilo kaburi ilikuwa ni kuwanyamazisha kwenye ukweli na kuwataka kupotosha ule ukweli.

Fedha kumwagwa kwa Askari hawa ilikuwa ni kusema kile walikitaka wao na si ule ukweli uliotendeka.

Tunajifunza kwamba wapo watu wanaweza kutoa gharama yeyote ile kuwapa watu fedha waseme habari za UONGO.

Ukweli unaweza kugeuzwa na baadhi ya watu waliolipwa pesa nyingi kwa kusema habari za UONGO.

Habari mbaya ni kwamba ukweli huwa una tabia ya kujisimamia wenyewe, unaweza kuwadanganya watu sasa hivi, atatokea mtu mzuri na kuutoa ukweli wote ulivyo.

Juhudi za kuzuia watu wasijue YESU alifufuka hazikufanya kazi sawasawa, zaidi ukweli wa kufufuka kwa YESU ulisambaa kila mahali.

Mt 28:8 SUV
[8] Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa hofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake habari.

Mambo ya kweli yanaweza kufunikwa kwa muda mchache sana, Ila baadaye kila kitu kitakuwa wazi, hasa mambo yanayohusu Mungu na wana wa Mungu.

Tuache kutumia fedha nyingi kuuficha ukweli, ukweli una tabia ya kuota sehemu yeyote ile na kila kitu kikawa wazi.

Huwezi kutengeneza habari mbaya za YESU ukafaulu, na huwezi kuwachafua walio na YESU, zaidi utaishia kujichafua mwenyewe na kuonekana hufai.

Tusimame katika kweli na haki, tusiwahofie sana wale wanaotengeneza habari mbaya za uongo dhidi yetu ili kutuchafua, wakifanikiwa basi itakuwa ni kwa muda mchache sana baada ya hapo kila kitu kitakuwa wazi.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom