Innocenthezron
JF-Expert Member
- Oct 13, 2016
- 393
- 472
Mimi ni mwanafunzi mwaka wa kwanza wa udaktari hapa Hubert Kairuki memorial University HKMU. Sijawahi panga kusoma katika hiki chuo kutokana na ada yake kuwa kubwa lakini kutokana na passion yangu ya kuwa daktari na upungufu wa vyuo vya udaktari hapa nchini nikalazimika kuja kusoma hapa nikijipa moyo kwa kuwa sijawahi soma private school labda nitapewa mkopo asilimia mia lakini mambo hayajawa kama nilivyodhania.
Naomba kama kuna mashirika au watu binafsi wanaoweza kunifadhili masomo yangu kwa mkataba wowote ambao hautaingilia utu wangu niko tayari hata kama kuwafanyia kazi pindi nitakapomaliza masomo yangu hata kua daktari binafsi pia nipo tayari.
Natanguliza shukrani wana JF natamani ninachokiandika sasa kitimie. Namtanguliza Mungu pia katika haya maombi yangu.