Naomba orodha ya viwanda vilivyoanza kujengwa

Naomba orodha ya viwanda vilivyoanza kujengwa

Niende moja kwa moja kwenye swali la msingi tumeambiwa tuko kwenye Tanzania ya viwanda mi naomba tu list au hata picha tu ya kiwanda kilicho kwenye hatua ya ujenzi au hata tu eneo lililofyekwa ili kiwanda kijengwe. Maana huu wimbo wa Tanzania ya viwanda nimeshindwa kuuimba.
Je kiwanda huwa kinaota Kama uyoga???
Mkiambiwa wekezeni hamtaki bali mnataka nyumba ya 200m, serikali ikiamua kutumia pensheni funds kuwekeza , oh serikali inaturudisha kwenye ujamaa, sasa sijui mnataka nini
 
Je kiwanda huwa kinaota Kama uyoga???
Mkiambiwa wekezeni hamtaki bali mnataka nyumba ya 200m, serikali ikiamua kutumia pensheni funds kuwekeza , oh serikali inaturudisha kwenye ujamaa, sasa sijui mnataka nini
Hivi ile safari city dege eco morroco square ni sisi tumewekeza au serikali?
 
Mimi nnavifahamu walau viwanda vitatu vilivyopo katika hatua za mwisho kabla ya kufunguliwa... Kimoja kipo Kibaha Maili Moja ni cha kutengeza sabuni aina ya Kleesoft, shampoo za aina mbalimbali na 'detergents'; kingine kipo kilomita tano kabla ya kufika Chalinze kutokea Dar es Salaam ni cha kutengeneza tiles na kingine kipo eneo la Mboga, Chalinze. Hini ni cha kusindika matunda.

Kwa ujumla vyote vitakapoanza kazi vitatoa ajira za moja kwa moja takriban 10,000
Vilianza kipindi cha kikwete hivyo kwahiyo usidanganye umma
 
Viko vingi wewe tu ndio hujavijua..... kuna biko tatu mzuka soka bet meridian mbet viko vingi aisee
Hivi huitwa viwanda muflisi!!! Huanzishwa ili wanaoficha fedha kwenye vibubu waziibue na kufanya uwekezaji kwenye "betting".
 
makala-pic.jpg

Hiki hapa mkuu.
Tutavaa nguo mpya halafu tuvue tuwapelekee ulaya wakavae mitumba yetu
images

Hapa wachezaji wa mpira wakiwa wanazindua kiwanda kimoja maeneo ya jiji la dar
 
Kwani rais anavyosema tanzania ya viwanda yeye ni mama ntilie muuza supu?
Km nchi zilizoendelea km Marekani na Uingereza zilichukua zaid ya miaka 50 kufika nchi ya kiwanda. Leo hii Tanzania inataka kuwa nchi ya viwanda kwa miaka 2 tu? Hicho kitu hakiwezekani ndiyo maana ukiwa na cherehan 4 ni kiwanda. Hapa hapa hata gereji ni kiwanda
 
Kiwanda cha burudani kinanzishwa leo!

Ova
 
Vilianza kipindi cha kikwete hivyo kwahiyo usidanganye umma
Hapana, havikuanza kipindi cha Kikwete... Ukweli ni kwamba wawekezaji hao walipewa certificate na TIC Juni mwaka jana.

Desemba mwaka huo huo wakafanya site clearing na mimi nilikuwapo. Kisha wakaanza ujenzi Januari mwaka huu. Uzinduzi (jiwe la msingi) wa ujenzi ulifanywa na Mwijage. Hiki si kipindi cha Kikwete na wala huku si kudanganya umma!

Viwanda hivyo nilivyovitaja vinatarajiwa kuanza uzalishaji wakati wowote kuanzia sasa...
 
Baadhi ya watanzania ni watu wa ajabu sana badala ya kuwa na positive thinking nyie mnakuwa on the negative side,nchi hii tutaijenga sisi wenyewe
 
Back
Top Bottom