Queenever1
JF-Expert Member
- Jul 30, 2019
- 422
- 815
Habari za usiku,,jamani nisaidieni nifanyaje. Juzi nilikua kkoo nikatoa Pesa kwa Crdb wakala, mtandao ulisumbua sana badae ikatoka akanipa. Nikaondoka. Sasa Leo nafsi ikaniambia angalia salio,,naangalia nakuta ile Pesa niliyotoa ,,imetoka na nyingine kiasi kile kile ,,nikapanic kurudi kwenye msg zipo mbili zinaonesha hela ilitoka Mara mbili ( laki 2 ×2=400000/=) nimepanic sijui naanzia wapi ,,nataka kesho niende kwa Yule wakala je atakubali ndo kinachonipa headache ,,nifanyaje nipate Pesa yangu??? Mwenye wazo wapendwa,Ahsanteni. Nilikua na Mr alinizuia kabisa kutoa pesa kwa wakala kwa vile niliona ATM ziko mbali nikalazimisha,,sasa nahaha mwenyewe kitandani naogopa hata kusema😤
