Naomba msaada wanaJF; Masikio yangu yanaunguruma kwa ndani

Faithful girl

Member
Feb 2, 2016
55
18
Habari za jioni,

Mimi ni binti wa miaka (20), kwa muda wa kama wiki sasa masikio yangu yamekuwa yakiunguruma kwa ndani kama sauti za magari hivi,mpaka kuna wakati nashindwa kusikia vizuri. Nakosa raha jamani, naombeni msaada wenu jamani.

ASANTENIII
 
Pole sana kwa shida uliyo nayo lkn msaada zaidi ni kuchukua hatua ya kwenda hospital kuwaona watalaam ili wajue shida nini then watakupa msaada zaidi
 
Aisee tafuta ushauri wa daktari wa masikio haraka sana aisee.

Siku maumivu ya sikio yakianza halafu yakaungana na mishipa ya kichwa, utajuta kuzaliwa kwenye hii dunia.

Sikio we lisikie tu, maumivu yake hata jino wala jicho hayafuati........
 
Kwanza ingefaa upeleke jukwaa la JF Doctors na ushauri muhimu zaidi ni kuwahi hospitali waliosomea kwa miaka zaidi ya mitano na kupata uzoefu wa miaka kadhaa wakusaidie.
 
Asante kwa ushaur mkuu
 
Vyema ungetaja mkoa/wilaya unayoishi watu wakupe ushauri wa Hospital ipi au Daktari yupi wa kumwona.
 
Kwanza ingefaa upeleke jukwaa la JF Doctors na ushauri muhimu zaidi ni kuwahi hospitali waliosomea kwa miaka zaidi ya mitano na kupata uzoefu wa miaka kadhaa wakusaidie.
Asante mkuu.daktar specialist was masikio ntampata wap
 
Pole sana binti wa miaka 20,wahi hospital mara moja.Labda haujayasafisha kwa muda mrefu
Naomba pia nikuswalike haka kaswali
Vipi haujaanza kuwaruhusu watu waanze kupitisha ndimi zao kwenye hayo masikio?
Sidhani kama usiposafisha masikio kwa muda mrefu kunaweza kupunguza usikivu.
 
Habari za jioni,

Mimi ni binti wa miaka (20), kwa muda wa kama wiki sasa masikio yangu yamekuwa yakiunguruma kwa ndani kama sauti za magari hivi,mpaka kuna wakati nashindwa kusikia vizuri. Nakosa raha jamani, naombeni msaada wenu jamani.

ASANTENIII
What is buzzing in ears?
The sound of buzzing or ringing in your ears in
the absence of audible noise can be annoying.
The symptom caused by a medical condition
called tinnitus, which produces a sound that
may resemble ringing, buzzing, clicking, hissing,
clanging or wheezing. They can be present in one
or both ears, constant or intermittent. It is a
common condition that can range in severity
from being a nuisance to a symptom of a
medical emergency that should be evaluated
immediately.

Tinnitus has no known direct cause, but it can
be symptomatic of ear infections, foreign
objects in the ear, earwax buildup, allergies,
high blood pressure, anemia, or a condition
known as Meniere’s disease (swelling in part of
the inner ear canal, causing dizziness and
hearing loss). Alcohol, caffeine, and certain
drugs are also contributing factors in some cases
of tinnitus.

Faithful girl tatizo lako ni hilo hapo kwenye maelezo ya bluu, kama hujaelewa hapo niambie nikusaidie ufahamu.
 
Chukuwa punje 3 za kitunguu saumi kijiko kimoja cha mafuta ya nazi au haba soda chemsha kwa mafuta hayo kama dakika moja na nusu ivi alafu yaache ya poe yatie masikioni inshallah inshallah utapoa
 
of tinnitus
.

Faithful girl tatizo lako ni hilo hapo kwenye maelezo ya bluu, kama hujaelewa hapo niambie nikusaidie ufahamu.
Ungefafanua Kwa kiswahili itapendeza sijakuelewa kabisa
 
Chukuwa punje 3 za kitunguu saumi kijiko kimoja cha mafuta ya nazi au haba soda chemsha kwa mafuta hayo kama dakika moja na nusu ivi alafu yaache ya poe yatie masikioni inshallah inshallah utapoa
Sasa habat soda inawezaje kumfanya asikie vizuri wakati hiyo ni dawa ya kuondoa maumivu tu.
 
Ungefafanua Kwa kiswahili itapendeza sijakuelewa kabisa
Mkuu hapo anamaanisha kwamba, mivumo, kelele au sauti ya kengere masikioni wakati haupo kwenye eneo lenye kelele linajulikana kitaalam kama tinnitus ambalo ni tatizo linaloweza kutokana na sababu mbalimbali kama vile kujazana kwa nta(ear wax)kupita kawaida, uchafu masikioni, maambukizi ya bakteria kwenye sikio, mzio(allergy)nk. Hivyo ni vigumu kubainisha tatizo lake hapa Jf bila kupitia kwa daktari.

Nasikia asilimia kubwa ya watu wanalalamika usikivu wao kupungua(hearing loss)ni kutokana na uchafu na takataka zilizoziba mfereji wa kuchuja sauti kabla ya kupelekwa kwenye sikio la ndani, ikibainika masikio ni machafu utasafishwa kwa kupigwa bomba la maji ya moto sikioni na kunyonya uchafu utoke nje.
 
Back
Top Bottom