Naomba msaada wako tafadhali ili nipate matibabu

Mtumaini Mungu

JF-Expert Member
Aug 3, 2021
879
1,061
Naliinua na kulitukuza jina lako We Bwana, Baba Muumba wa vyote vyenye uhai na visivyo hai.

Habari zangu ndugu zangu, imekuwa karibu miezi miwili nikiwa kimya hapa jukwaani, sababu hasa za ukimya wangu ni maradhi yanayonisumbua na kunitesa kiasi kupelekea kutomudu majukumu yangu ipasavyo. Mwezi wa 11 mwanzoni nililazwa kutokana na maradhi ya vidonda vya tumbo.

Nikiwa hospital nilifanyiwa vipimo na kugundulika nina shida pia ya maambukizo kwenye sehemu ya mwisho ya utumbo ambayo imeungana na njia ya haja kubwa (Lakini madaktari wamenihakikishia sio saratani).

Ndugu zangu kwa sasa naendelea vizuri japo bado sijaruhusiwa kwasababu matibabu yanaendelea.

Lengo haswa la Mimi kufungua nyuzi hi ni kuomba MSAADA toka kwako wewe mwana JamiiForums mwenzangu, ninatakiwa kulipa gharama ya Tsh 91,200/= ili niweze kuendelea kupata matibabu na kuruhusiwa. Pesa hi ni sehemu ya gharama za matibabu (NIMESHINDWA KULIPA PESA YOTE).

NINAOMBA kwa yeyote ambaye anaweza kunikopesha pesa hii anikopeshe, NITAILIPA 30/12/2021, nipo tayari kuilipa na riba ya Tsh 15000/=.

Lakini pia endapo Mungu hajakujalia kuwa na pesa hii kwa pamoja, NINAOMBA mchango wa kiasi chohote ili nikamilishe malipo ya deni hili.

Nawasihii wapendwa msinisahau katika sala, dua na maombi yenu.

Kama una chochote na ungependa kunisaidia basi ninaomba tumia namba hii Ili kuwasiliana na Mimi mwenyewe, na pia kutuma mchango wako.

Mungu mwenyewe aliye mpaji na awabariki, awarudishie na kuwaongezea pale palipopungua.

Mtumaini Mungu
Mtwara, Tanzania.

SHUKRANI KWENU NYOTE.
Ninawashukuru kwa MSAADA wenu, nimepata MKOPO toka kwa mmoja wa wana JF.
 
Pole kwa matatizo mkuu. Mungu akutangulie kwanza kabla ata michango haijafanikiwa.

Ila kwanini usingetumia control number mtu aweze kulipia kwa control no itasaidia assurance.
 
Pole kwa matatizo mkuu. Mungu akutangulie kwanza kabla ata michango haijafanikiwa.

Ila kwanini usingetumia control number mtu aweze kulipia kwa control no itasaidia assurance.
Asante sana mkuu, Mema unayo niombea Mimi Mungu mwenyezi aliye hai akupe zaidi ya wema huo.

Hapa kwenye control number sijaelewa vizuri, je kituo ndo kinatakiwa kutengeneza hiyo number au ni Mimi?

Kama ni Mimi naomba nifahamishwe namna ya kutengeneza.
 
Pole sana.

Ila kwa ushauri, ungetuma na supporting evidence za kuumwa ili tusiwe na doubt na wewe.
 
Pole sana.

Ila kwa ushauri, ungetuma na supporting evidence za kuumwa ili tusiwe na doubt na wewe.
Asante sana kaka.

Nitumie meseji au nipigie kwenye hiyo namba yangu.

NIMESHINDWA kuweka documents za hospital kwasababu ya PRIVACY YANGU Lakini endapo mtu atahitaji basi sina budi kumtumia ili nisaidiwe.
 
Privacy gani mkuu? Wakati ushatoa namba na ni kiasi tuu cha mtu kuangalia jina lako?
Na nikishajua jina lako ni kiasi tuu cha kuuliza hospitalini hapo kama kuna mgonjwa wa namna yako kalazwa!
 
Privacy gani mkuu? Wakati ushatoa namba na ni kiasi tuu cha mtu kuangalia jina lako?
Na nikishajua jina lako ni kiasi tuu cha kuuliza hospitalini hapo kama kuna mgonjwa wa namna yako kalazwa!
Hio ni namba yangu na imesajiliwa kwa majina yangu, nimelazwa hapa Hospital ya rufaa Ligula.

Kama Kuna ushauidi utahitaji ukinitafuta kwa namba hiyo NITAKUTUMIA.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom