Naomba msaada wa ushauri, nini tatizo la kuwashwa mlango wa haja kubwa?

Pole inawezakuwa ni minyoo maana huwa kuna viminyoo vidogovidogo vinaitwa ascaries kama sijakosea kutamka na kuandika huwa vinatabia ya kutekenya kwenye mlango vinakuwa kama vinataka toka ila vinapopata hewa ya nje vinarudi tena ndani hivyo kwa stail hiyo vinasababisha sana muwasho.

Bora uende tena hospitali ukapime. Maana hata kama utasema umetibiwa sana minyoo lakini bado pengine na mazingira yako mwenyewe sio safi, i.e hunawi mikono unapotoka kujisadia haja kubwa na ndogo, hunawi mikono na sabuni kabla na baada ya kula chakula, vyakula vibichi hasa matunda na mbogamboga hayaoshwi vizuri na maji safi kabla ya kuliwa na kupikwa.

Kwa hiyo unakuwa unajitibu minyoo na unaingiza wengine wapya. kama usafi hauzingatiwi.
 
Huo unaitwa upeke(minyoo midogodogo hua inatekenyaga uko kwenye ndude)tafuta dawa za minyoo or umwone doc.
 
Pole sana, jitahidi pia na usafi pia tumia deto, pia usile vyakula vya pilipili.
 
pole. kwanza toa wazo la minyoo make sio minyoo

mara nyingi huwa ni fungus lakin wengi huchukua dawa pharmacy bila kupewa ushauri na daktari jinsi ya kutumia
  1. sehemu ya aja kubwa na uke pamoja pembeni ya pumbu za mwanaume au perineum yote huwa na unyevu ambao ndo mazingira mazuri ya fungus lakini pia ina uchafu ambacho ni chakula kizuri kwa bacteria
  2. jinsi ya kutumia kama ni fungus sugu inabidi utumie dawa mbili systemic antifungal yani dawa za kumeza pia na topical yani za kupaka kwa mwanamke anaweza kuongeza dawa ya kuweka ndani ya uke yani vaginal pessaries lakini kabla ya kutumia nyoa eneo lote pia mtibu na mkeo au mmeo
  3. siwezi kuandika dawa hapa maana si utaratibu mzuri ni PM ntakwandikia
  4. lakini ntakwandikia dawa kwa magonjwa mengine ya zinaa
 
a
Aksante sana mdau kwa ushauri wa kitaaluma.

Naona watu wanaleta mambo ya Chit-chat na ya Jukwaa la Wakubwa kwenye jukwaa serious la JF doctor.,this is pitty, inakuwa kama wengine hatujawahi kuugua kabisa.

Walioleta utani wa kijinga hapa wote wako kwenye pipeline ya ban. Take my word to a commercial bank.
 
Back
Top Bottom