Msaada kuhusu tatizo la koo kuhuma (persistent sore throat)

Vonzelewsk

Member
Sep 20, 2018
20
21
Habari ndugu zangu wa JF ..kama heading inavyojieleza naomba msaada wenu kwa ushauri najua JF ina kila aina ya watu nimeamua Nije apa kwakuwa nina amini hii ni nyumba ya kila kitu.

Tatizo langu la koo kuhuma lilianza takribani miezi 6 iliyopita..Nilianza kusikia maumivu ninapomeza chakula,shida kumeza mpaka nisukumie na maji hiyo condition ilienda kama siku 5 baadae ikatoweka. Nikaanza kusikia kitu kama kimekwama kooni ila nikikimeza akimezeki nayo ikaa kama wiki1 then ikaondoka iyo hali.

Nilienda hospitali nikaonana na Dokta nilivyomuelezea akaniandikia dawa za kumeza moja wapo ni Ampliclox nikatumia mpaka zikaisha lakini tatizo linaenda na kurudi mpaka muda huu ninaleta thread apa limekuja tatizo lingine ambalo ni kupaliwa yani nikiongea kama dk1 ivi lazima nipaliwe.

Koo bado linauma na nikiongea au kukaa tu hali ya kupaliwa uja ghafla naomba msaada wenu wa ushauri na mawazo nini cha kufanya ili nijue kinachonisibu ..Asanteni..naomba mnisamehe kwa thread ndefu..
 
Pole sana mkuu nilipitia hali ya kuhisi kama kuna kitu kimenasa kooni na maumivu hasa nyakati za asubuhi lakini nlikuja kugundua ni kutokana na aina ya perfume niliyokuwa naitumia. Nilivyoachana nayo tu tatizo likaisha, nilitumia tangawizi ilinisaidia kiasi.

Tatizo lako ni la muda mrefu nenda kwa wataalam wa afya
 
Shukrani kwa ushauri..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom