Naomba msaada wa ushauri mtoto mtukutu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba msaada wa ushauri mtoto mtukutu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by moghaka, May 16, 2011.

 1. m

  moghaka JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Wakuu tafadhalini sana naomba msaada wenu, kijana mkorofi, mtukutu amemaliza f4-2010 matokeo ana D moja tu ya biology,veta hataki anataka kuunga certificate ya business, akaomba ali-sit mwaka huu 2011, shuleni fujo, walimu wanadai anakunywa pombe, sigara, kutoroka n.k wamemfukuza na malalamishi km hayo alikuwanayo akiwa f4, nimechoka sana, naomba msaada wenu wa kila hali niko tayari na ndio first born, je pana shule ya WATUKUTU kama hawa ?
   
 2. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  nionavyo mimi

  1. Maombi

  2. hiyo ni adolescence inamsumbua kaa nae chini muulize mipango yake ya maisha na usiwe mkali sana, relax muulekeze bila kumgombeza kama anataka kuwa mtu huku dunia anapaswa kuenenda vipi? kwa sababu yeye anaona anavyofanya hayo ndo maisha

  3. msome mtoto kama sio adolescence pengine ana frustration fulani na anaona hiyo ndio njia.

  4. chunguza kwa umakini makundi ya huyo mtoto na akiwa nyumbani dont let him be so loose keep him busy by different activities whether he likes them or not.

  5. usiwe na wasiwasi hilo ni jaribu tu katika familia yako litapita

  6. kama unaweza pata shule ya masista au mapadri watakusaidia pia kumnyoosha

  7. mkazanie sana kujifunza mambo ya dini ili aone hayo matendo yake si sawa hata kwa Mungu

  8. punguza kiasi cha pesa unachompa coz anapata wapi hela ya pombe.

  9. muambie hautakuwa nae milele he has to get his own life on track.

  10. usichoke kumpenda
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kwanini usijaribu kumpeleka jeshini?
   
 4. Chitemo

  Chitemo JF-Expert Member

  #4
  May 16, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,293
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  umesahau hz methali? Samaki mkunje angali mbichi..!
  ama
  Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
  Ushauri wangu ni kwamb jaribu kuongea naye na umcctize nini muhtasar wa maisha yake ya baadaye after ur decease (pole) na kama haelewi mwombe mungu ambadilishe.
  my take: analinga na hzo mali zako ama cheo chako.
   
 5. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #5
  May 16, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Aina hiyo ya mtoto na hao hapo kwenye red si kitawaka?
   
 6. c

  ccr airtel Member

  #6
  May 16, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  yah huyo mpeleke jeshini tu labda kama atagoma...lakini kule ndo kwa wakuu atafunzwa nidhamu ya ukubwani
   
 7. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #7
  May 16, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kuna wakati wenye matatizo ni wazazi katika njia za malezi, katika umri alionao NEEMA ya Mungu yahitajika katika kumrejesha katika njia iliyo sahihi au la hasha DUNIA NDIYO ITAKAYOMFUNZA. Watoto wanaelekezwa katika umri wa 0 - 12 (ndipo hapo husemwa SAMAKI MKUNJE ANGALI MBICHI) , akivuka miaka 12 hekima ya ziada yahitajika katika kumwelekeza mto njia impasayo. Hivyo basi kwa sasa jitahidi kumuomba Mungu kwa ajili yake, mshirikishe katika mambo yahusuyo familia mara kwa mara ili atambue kwamba yeye ni sehemu ya familia na anahitajika sana huku mkimkumbusha wajibu wake wa baadae katika kuchukua majukumu ya familia. Usimchukie kwa yale anayoyatenda; kama unasikia anakunywa Pombe au Kuvuta sigara mpe uhuru wa kutumia mbele yako, huku mkimkumbusha madhara ya kufanya hivyo bila ya kumhukumu. Hii itakusaidia wewe kumfahamu badala ya kusikia tu kutoka kwa walimu na watu wengineo, wakati mwingine wanaweza kuwa wanamhukumu katika mambo asiyoyatenda. Wakati nikiwa sekondari Baba yangu alikuwa anaelezwa kwamba mimi navuta bangi na yeye alikuwa anaamini hivyo, hii ilitokana na mimi kuambatana na marafiki ambao wanavuta bangi. Lakini ukweli ni kwamba kwa wakati huo nilikuwa sijawahi hata kujaribu.
   
 8. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #8
  May 16, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  POLE KWA MKASA.INGEKUWA VEMA KAMA UNGETUJUZA NANI ALIMLEA ALIPOKUWA MDOGO?JE ALIKUWA ANAADHIBIWA ALIPOKUWA ANAFANYA MAKOSA PINDI ALIPOKUWA MDOGO?ALIKWENDA SHULE AKIWA NA KIASI GANI CHA MATUMIZI?KULIKUWA KUNA UTARATIBU WA KUMSEMA ANAPOFANYA MAKOSA?NYUMBANI KUNA MALI INAYOMPA KIBURI?ANAVUTA BANGI?NIJIBU HAYO ILI NIKUPE MENGINE.TAFUTA MZEE WA HESHIMA AMBAYE ATAMPA DARASA LA KUTOSHA JUU YA MAISHA NA TARATIBU ZAKE.kuna uwezekano ujana unamsumbua!pia wakati mwingine jaribuni kutomjali ili ajue umuhimu wenu!Pia akileta utata mpelekeni mahakamani kwa makosa anayotenda,nina iman akifungwa itakuwa vizuri kidogo.Kuna mmoja alifungwa karud kanyooka.Pia ikiwezekana mbembeleze aende JKT ATARUD NA ADABU.
   
 9. H

  Heri JF-Expert Member

  #9
  May 16, 2011
  Joined: Aug 28, 2007
  Messages: 242
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hujasema status yako. ie single parent, divorced, married. Je ni mtoto nje ya ndoa au una m/watoto nje ya ndoa
  . Huwezi kupata ushauri mzuri bila vitu hivi kufahmika pamoja na mambo mengine.
   
 10. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #10
  May 16, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Eti waalimu wanadai kwa mtoto ni mlevi, anavuta bhange, anatoroka... Wazazi wengine bwana!
   
 11. A

  Aine JF-Expert Member

  #11
  May 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Pole sana; Kwanza muombee sana kwa Mungu.
  Pili hope kwenu ni kijijini, mpeleke kijijini kama kuna baba yake mkubwa au mdogo au mjomba asiende kwa bibi/babu atawasumbua, akae huko kwa muda wa zaidi ya miezi mitatu na atakayekaa naye awe anaenda naye shamba kulima tena ampe shamba lake na alime na kupanda na kupalilia kila simu kasoro siku za ibada. Na hakikisha nyumba anayokwenda haina umeme wala anasa zozote za mjini.

  Kama ulimnunulia simu mnyang'nye kipindi hiki atachokuwa kijijini
  Mpeleke mwenyewe na umuachie hela kidogo sana zisizoweza kutosha nauli ya kurudia kijijini hadi hapo utakapomfuata.
  Mpe masharti kwamba kama anapenda shule, basi akae hapo wakati unatafakari nini asome na unajipanga kifedha.
  Mwambie ndg utakayempelekea mtoto wako kwamba ahakikishe anafanya kazi na siku za ibada anaenda kusali bila kukosa

  Kama huwa anakusiliza, akikaa kijijini kwa muda huo, bila tv, umeme, simu, na kufanya kazi za shamba atabadilika ila atakayekaa naye awe strict kwa nidhamu na kazi.
  Wakati yupo jijini muombe Mungu ambadilishe na asirudi hadi utapomfuata
  All the best
   
 12. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #12
  May 16, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ushauri wako umetulia, nimeupenda. Pia umeuliza maswali ya msingi sana
   
 13. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #13
  May 16, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Pole sana kaka Moghaka, hata mimi nilipita katika kipindi cha nduguyo. Kikubwa ni kuwa anadhani ninyi mnashirikiana na walimu kumchukia, tayari ubongo wake umejijenga kwa hilo. Kuhusu balehe, NO, hakuna balehe ya 17+ siku hizi. Ushauri wangu ni kuwa, kwanza, punguza kumuonesha kuwa umemchoka, kijana kama huyo ukimhubiria kuhusu mapungufu yake mara nyingi unakuwa kama wimbo, anauzoea na haumpi tabu kabisa. Nadhani wewe ndio mlezi wake, tumia nafasi ya yeye kuomba fedha au privileji zingine kumueleza vile unakwazika na matendo yake, au mpotezee kwa muda mpaka ajistukie.
   
 14. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #14
  May 16, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  nlidhani ingekuwa busara kama ungetoa maoni yako kwa kumshauri na sii kwa kumkejeli we kama huna jibu sii ukae kimya tu.Yatakukuta na ww naona bado hujui nini maana ya uzazi.
   
 15. AlP0L0

  AlP0L0 JF-Expert Member

  #15
  May 16, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 3,473
  Likes Received: 759
  Trophy Points: 280
  Tuko pamoja mkuu! Huruma hailei mwana.
   
 16. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #16
  May 16, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  umeyasababishwa mwenyewe mzaz....kuna shule moja iko kenya huko watot wakotrofi wote wako kule
   
 17. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #17
  May 16, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mpeleke mombasa
   
 18. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #18
  May 17, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mwana umleavyo ndivyo akuavyo huyo kwa sasa ni maombi tu maana kila utakalomwambia anakuona umepitwa na wakati
   
 19. Jomse

  Jomse JF-Expert Member

  #19
  May 17, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna shule moja kenya kama utahitaji jina lake ni PM.Mtoto unamkabidhi mwalimu hapa dar na haruhusiwi kurudi mwenyewe mpaka utakabidhiwa tena na mwalimu watakapofunga shule.Akifika shule haruhusiwi kutoka nje ya eneo la shule na haruhusiwi kuwa na simu.Ukitaka kuwasiliana nae utampigia matron au patron na mtoto wako utaongea nae.
  Hii ilimsaidia jirani yangu ambaye binti yake alianza ukorofi wa ajabu alipofika form two alimpeleka huko na sasa amebadilika
  Kumbadilishia mazingira na kampani inasaidia sana kwani yawezekana ana group baya la marafiki .
   
 20. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #20
  May 17, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Pole ila hujanijibu maswali ambayo nilikuuliza mkuu.Au bado unampenda mwanao?
   
Loading...