pole sana mkuu! hizi ni changamoto za kawaida ktk maisha,muombe Mungu uzivuke hizi changamoto
ila nakushauri jaribu njia mbadala ktk kutafuta kazi weka vyeti pembeni kwanza, ukiona kazi kama ambazo unaweza kufanya kama reception,sales,marketing,office assistant wewe jaribu ili mradi upate mkate wa siku ili kababy kasilale njaa
hata biashara jaribu kufanya maana sio wote tunatakiwa kuwa maofisini,nakupa mfano rahisi wa recent graduate waliothubutu na wamefanikiwa kusonga mbele
- huyu wa kwanza alimaliza sua alikaa more than two years mtaani lakini baadae alianza na mtaji wa elfu tano ananunua njegere na mbogamboga sokoni kariakoo usiku saatisa alafu asubuhi mpaka mchana analangua rejareja ikifika saa nane mchana anarudi nyumbani kupumzika ,kweli jamaa amefika mbali sana kwani mmoja ya wateja wake alimuona anahudimia kwa ueledi mkubwa alipomuuliza elimu yake akamwambia ukweli kuwa changamoto za maisha ndio zimemfanya afike hapa,milango imemfungukia maana alichukuliwa kama consultancy na kampuni fulani hivi,last year alipewa promotion yupo nje ya nchi na familia yake kama expert na bado anakampuni yake kaacha hapo bongo sometimes huwa naenda kufanya daiwaka na bwana mdogo ananilipa kiaina
- huyu wa pili sio mfano mzuri kwani jamaa ni static hataki kubadilika,huyu ni udsm political science graduate ambaye amaamua kuwa kondakta na yupo happy sana kwa kazi yake,kwa maelezo yake kila siku anapata kati ya 30000 mpaka 40000 kama posho na ana mke na vitoto viwili,japo ugomvi wake na mimi nataka habadilike asikae sehemu mmoja,lakini maisha yake yanaenda na anafanya maendeleo
kwa mifano hii michache,japo unaweza kuiona haina maana jaribu kuangalia fursa zingine,maana wengi huwa tunapenda kazi za kukaa ofisini kwenye ac lakini hakuna maslahi ya kutosha unless uwe mwizi au kuishi kwa mikopo ya bank inayotusitiri hapa mjini tusiaibike
mkuu mimi nakutakia kila la kheri kwenye kutafuta maisha na Mungu ailinde familia yako usiitelekeze maana mwenyezi anasikia kilio chako na sikio lake si zito kusikia