Naomba msaada wa kuondoa madoa na chunusi usoni

Melodia

Member
Jun 22, 2012
8
10
Habari wakuu,
Ninaomba msaada kwa mwenye uelewa wa cream nzuri(isiyochubua please)kuondoa tatizo la chunusi usoni kwangu.

Nimeshatumia vitu vingi Lakini baada ya muda tatizo hurudi.Ninaomba mwenye Tiba ya uhakika anisaidie.

Nimesikia La vista cream inasaidia na haichubui Kuna mwenye testimony na hili?

Asanteni!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Creams zinasaidia ila kama hujui kuitunza ngozi yako chunusi zinarudi pale pale

Jaribu kutumia *botouer ant acne (kama ngozi yako ni ya mafuta sana)
Botouer whitening (kama una ngozi kavu)

Pendelea kuosha uso na maji ya uvuguvugu na sabuni za herbal

Usipake mafuta mazito usoni, ukitembea kwenye jua kali sana hakikisha unakitambaa cha kujifutia uso na immediately unavyofika home osha uso

Yani uso uwe unacheza sana na maji, pia pendelea kunywa maji mengi sana, punguza vyakula vya mafuta mengi

Njia za asili

Changanya ndizi mbivu, limao na manjano paka usoni kaa nayo dkk20 osha uso na maji ya uvuguvugu

Asali, limao, manjano, liwao

Nyanya, sugulia usoni

Uteute wa alovera paka usoni, dkk 20-30 osha uso wako kwa maji ya uvuguvugu

Nb:
Usikamue chunusi (maybe zile za njano maana zinaleta muonekano wa kinyaa kwako na kwa watu unaokutana nao) usikamue ukitumia hayo maelekezo niliyotoa zitakauka na kuisha kabisa zenyewe

It depends na ngozi inareact vipi kuna inayowahi na zinazochelewa, usichoke kama majibu ni ya taratibu mno

Unapokamua chunusi ndio zinaleta black spots/dots usoni na kuongeza idadi ya chunusi (yale majimaji, maana ngozi ya uso ni laini sana na very sensitive)
 
Melodia,

Usitumie cream yoyote

Kunywa maji mengi,pata muda wa kupumzika/kulala,epuka vyakula vya mafuta mengi na osha uso/oga kabla hujalala kila siku (usilale ukiwa umepaka chochote usoni)

Mie huwa napata chunusi pia nikikasirika kasirika ama kuwa na stress so nafikiri nayo inaweza kuwa sababu
 
Hakutoka tumboni na chunusi....anataka awe kama alivoumbwa labda km angekuwa anataka kuwa kama Michael Jackson

Usidandie gari kwa mbele utagongwa nyuma mama yako...!

Hayo ndio maumbile aliyojaaliwa na MUNGU akitaka awe kama alivyotoka tumboni mbona hajirudishi utoto akawa anajinyea na kujikojolea. Jinga kabisa.

Shubhaaaaaamit.
 
Melodia,

Usitumie cream yoyote

Kunywa maji mengi,pata muda wa kupumzika/kulala,epuka vyakula vya mafuta mengi na osha uso/oga kabla hujalala kila siku (usilale ukiwa umepaka chochote usoni)

Mie huwa napata chunusi pia nikikasirika kasirika ama kuwa na stress so nafikiri nayo inaweza kuwa sababu
Hii nadhani ndiyo tiba halisi... Maji na matango yanasaidia sana kutengeneza ngozi nzuri...
 
Ukiendelea kutumia creams ndo utajiharibu kabisa...bora ukae hivyo maji ya kutosha baada ya muda utaona matokeo
 
Back
Top Bottom