john_selcius
Member
- Jul 3, 2012
- 15
- 3
Mpendwa mwana JF,
Ninaomba msaada toka mtu yeyote au taasisi yoyote wa kununuliwa gari (tipa) lenye uwezo wa kuanzia tani saba na kuendelea liwe linaweza kubinua. Nimekusanya vijana Wilayani Mpanda mkoa wa Katavi, na kuunda kikosi kazi kinaitwa WASAFI HOME CLEANERS, tumepewa kazi na Halmashauri ya kuzoa taka kwenye kata moja ya Makanyagio.
Moja ya changamoto kubwa niliyo nayo ni gari la taka kwa kuwa magari hapa yanakodishwa kwa gharama ambayo kama kikundi hatuwezi imudu. Tumejikamua angalau kwa miezi minne. Tumefika mahali hatuwezi kuendelea na kazi kama hatutapata msaada huo.
Hivyo nakuomba msomaji wa JF na watu wote wenye nia njema na ajira kwa vijana, tusaidiwe kununuliwa au kupewa gari la kutusaidia kubeba taka baada ya kuzikusanya toka kwenye makazi ya watu.
Msaada wako utakuwa wenye tija sana kwani itatusaidia kuboresha kazi yetu hivyo kuongezewa maeneo zaidi jambo ambalo litasababisha kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania tulio wengi.
Tusaidie tuweze kusimama kwa miguu yetu wenyewe.
Tafadhali unaweza kutuma sms JF/Taka/Mpanda kwenye 0768 441 304 au wasiliana nami moja kwa moja. Pia unaweza PM.