Siri ya sifuri
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 2,018
- 1,508
Habari zenu wakuu,
Naomba msaada wa kidaktari, mimi mwana Jf mwenzenu ninatatizo la kiafya linalonipelekea kuhisi kwamba mwili wangu hauko timilifu kiutendaji, yaani mfumo wa fahamu unafanyakazi chini ya kiwango.
Ni hivi nimezaliwa nikiwa mzima wa afya sina tatizo lolote, ila baada ya kufikia umri kati ya miaka ishirini na ishirini na tano kuna tatizo la afya lilianza kujitokeza. Mwili wangu ulianza kupoteza nguvu na kunisababishia ulegevu wa viungo, nilishindwa kufanyakazi ngumu kwasababu nilikuwa nachoka mapema baadae maskio nayo yalianza kuwa mazito kusikia na sauti kupotea, yaani sauti ilikua inatoka kwa chini sana hata nikiongea kwa nguvu kiasi kwamba watu wengine wakawa wanapata tabu kusikia lakini sikuwa nikipata maumivu yoyote ya maskio wala kifua.
Baada ya kupata matibabu ya muda mrefu mahospitalini tatizo la mwili kukosa nguvu lilianza kupungua na baadae kuonekana kama limekwisha kabisa ,hata hivyo kwa upande wa maskio na sauti hali iliendela kuwa mbaya. Mpaka hivi sasa miaka karibia kumi toka nianze kuumwa na kupatiwa matibabu ya mara kwa mara bado sisikii vizuri na sauti inatoka kwa chini sana, yaani nikiongea kwa sauti ya kawaida naonekana kama ninaehema kwa nguvu bila kusema kitu lakini siumwi.
Nilishakwenda hospitali ya taifa Muhimbili, KCMC Moshi, Mnazimmoja Zanzibar na vituo kadhaa vya afya vya tiba mbadala na kote huko nimefeli kurekebisha hali ya maskio na Sauti.
Hata hivyo mara nyingi nilipokwenda hospitalini nimekuwa nikifuatilia huduma ya maskio na sauti ila sasa nataka nirudi tena mahospitalini kwa ajili ya vipimo ili niwezekujua chanzo cha tatizo, naamini likijulikana tatizo lilipoanzia kama ni kwenye Ubongo au Mishipa ya fahamu nawezakupata mafanikio na maeneo mengine.
Sasa naombe kujua ni aina gani ya vipimo ninavyoweza kupima na kujua hitilafu ilipoanzia ili nianze kutibu eneo hilo badala ya kupambana na maskio na sauti ambavyo huenda matatizo yake yanasababishwa na kiungo kingine ambacho ndicho kinachopasa kutibiwa.
(Natanguliza shukrani)