Naomba Msaada wa Kisheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba Msaada wa Kisheria

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Elli, May 22, 2010.

 1. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,827
  Likes Received: 10,128
  Trophy Points: 280
  Jamani wana JF,

  Kwa leo sitapenda kutoa taarifa kamili kwa jili ya interest fulani lakini naombeni sana kama kuna mtu anaweza nisaidia katika hili.

  Huku mkoanii kwetu tulipozaliwa, Baba na Mama walikuwa wafanyakazi wa serikali na tuliishi kwene nyumba ambayo ilijengwa kwa msaada wa serikali na kukabidhiwa baba, mara baada ya baba kustaafu aliachiwa nyumba mama tena kwa maandishi kwani alikuwa mtumishi wa serikali pia, cha ajabu,, afisa mmoja wa sekta fulani, alikuja na kufanya vurugu na tukatolewa kwenye nyumba na nuymba hii akamkabidhi ndugu yake. N
  imejaribu kufuatilia bila mafanikio lakini jambo zuri ni kwamba nimefanikiwa kupata baadhi ya nyaraka ambazo endapo nitapata msaada wa kisheria nitaweza kudai baadhi ya vitu.

  aliyetayari ntaaomba tuwasiliane hapa hapa then nitampa mawasiliano yangu binafsi

  Asante sana
   
 2. n

  nndondo JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Jamani pole sana, lakini japo yamepita mlitolewaje? na msaada unaotaka ni wa bure? ama ni wa contact? si unajua hii tanzania wanasheria wakumwaga ila wanasheria wanaojua sheria ni wachache sana. Kama ni contact nakupa ya Alex Mgongolwa simu labda wengine waweke kwa hapa sina ila yuko jengo la Bima mtaa wa azikiwe karibu na luther house wanatazamana na Baroda Bank upande mmoja upande wa pili kuna Sukari House yenye Stanbic chini na wao wana Tanzania standard charter chini yao gorofa ya 5 kampuni sijui jina nimesahau ila ukiuliza wakili mgongolwa utampata. Ushauri kwa watanzania wote, kwa sasa kama mnavyojua adui yetu mkubwa wananchi ni serikali yetu, watu wanajichukulia maamuzi mkononi na kutumia vyombo vya dola kuwa rubber stamp, hatuna serikali hakuna haki, kitu kama cha mwenzetu kikikukuta usikubali kutoka pigania haki yako mpaka ufe acha watoto wako waje kufaidi matokeo, mara nyingi hao wanaokufuata wanajua kwamba watanzania ukiwatishia mbwa kubweka wanatupa kila kitu na kukimbia, sasa hivi nchini hakuna sheria hakuna mwenye haki shikilia ulichonacho kesi zenyewe ni gharama wakili anataka hela, rushwa zimejaa hata kwenye mahakama, pia kesi hizi zinachukua milelel kumtoa mtu ndani ya nyumba utahitaji ubavu kweli, licha ya kukata rufaa, eviction orders zenyewe ni za kununuliwa, makarani wa mahakama kupeleka hiyo order, hela itabidi upate dalali wa kumtoa, bado kuna viongozi wa serikali za mtaa wa kushuhudia, hela dawa hapo ulipo fia hapo nchi hii viongozi wanaotakiwa kukutafrisiria sheria ndio wezi wakubwa. Pole lakini hapo ulipo dawa ni sheria tu kwa sasa wewe ni victim
   
 3. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Nipe kwanza adress yako nitangulize invoice yangu kabisa.,for lawyers it is unethical to provide a free legal service unless it ia a legal aid
   
 4. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,753
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280

  ingekuwa vema kama ukibainisha yafuatayo:

  -Je nyumba hiyo babako alipewa kama msaada moja kwa moja au ni wakati wa kipindi cha uhai wake na mke wake?
  -Je unadocuments zipi zenye kuonesha kuwa hiyo nyumba alipewa nbabako?
  -Je,umepita muda gani tangu mnyanganywe nyumba hiyo?
  -Je,nyumba hiyo imejengwa kwenye kiwanja cha nani?
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  May 26, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180

  Angalia usitende kosa la jinai liitwalo touting!

  Acting as tout prohibited:
  "Any person who, on behalf of any advocate, or for his own account, acts as a tout shall be liable to a fine not exceeding one thousand shillings and to imprisonment for a term not exceeding six months." (Section 47 of the Advocates Act, Cap. 341, R. E. 2002)
   
 6. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hivi hizi sheria huwa haziwi 'updated', hiyo shilingi elfu moja inatakiwa iwe equivalent na wakati au ndio fixed for the life time?
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  May 26, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nilimsikia Hakimu mmoja anasema kwamba ni afadhali amwachie mshtakiwa huru kuliko kumpiga faini ya fedha kidogo iliyowekwa kisheria! Alidai kwamba ni aibu kwa mshtakiwa baada ya kupigwa faini anaitoa fedha hiyo chap chap halafu "anadai arudishiwe chenji!" Anyway, Sheria kama imesema kwamba mshtakiwa alipe TSh 1,000/- hakimu hana budi kumtoza fedha hiyo hiyo iliyotajwa na sheria.
   
 8. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  touting: In British English, a tout is any person who solicits business or employment in an importune manner (generally equivalent to a solicitor
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Wenye mamlaka ya kubadili sheria Law reform Commission wanafanya nini? Si ndio ya yao ya kila siku. Ina maana wameshindwa kutekeleza majukumu yao
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  May 27, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Law Reform Commission mara nyingi huwa wako pro Government zaidi (of course ni chombo cha Serikali) kuliko kuangalia uhalisia wa mambo, ie wanafanya kile ambacho Serikali inataka, ndio maana Sheria nyingi zinabaki kama zilivyo! Kwa mfano katika kupitia Sheria 40 ambazo zilionekana kulingana na Tume ya Nyalali kuwa ni kandamizi, maoni ya LRC karibu yote yalifanana na yale ya Mwanasheria Mkuu! Siamini kama hawa jamaa wako seriously working!
   
 11. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #11
  May 27, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Touting: "The solicitation of business by highly recommending a security or product, esp. when the recommendation's basis is largely puffery (i.e. overdone praise)." [Black's Law Dictionary, 8th Edition by Bryan A. Garner, Editor in Chief].
   
Loading...