Naomba msaada wa Kisheria Kuifuta CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba msaada wa Kisheria Kuifuta CCM

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Kamende, Sep 2, 2008.

 1. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2008
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ni imani yangu kuwa wengi kati ya wanaotembelea hapa wana ujuzi mkubwa wa mambo ya kisiasa na kiuchumi Tanzania. Kwa hiyo sina kazi kubwa ya kuelezea hali halisi ya namna ambavyo nchi ya Tanzania inavyomasikinishwa na CCM.

  Nimesoma hoja za wengi humu jukwaani, KLHNews, magazetini kila siku ninasikiliza redioni na kuangalia katika TVs mbalimbali. Kila wakati ninajiridhisha kuwa asili ya matatizo ya Tanzania ni mfumo mbaya wa siasa ambao umewekwa na CCM na unailinda CCM isiondoke madarakani.

  Haiwezekani kupambana na rushwa na ufisadi kwani hiyo ni hirizi muhimu ya CCM.
  Haiwezekani kufanya siasa za usawa kwani CCM wanapambana na hilo kila siku.
  Haiwezekani wenye uchungu na nchi kufurukuta kwani wanawekewa mizengwe kila siku na wakubwa walioko ndani ya CCM.
  Haiwezekani watanzania wafaidi rasilimali za nchi yao kwani CCM imeamua kuwakasimisha wageni toka nje rasilimali za nchi hii.

  Kwa hiyo haiwezekani umasikini uondoke Tanzania kwani CCM imeamua kufungulia milango rasilimali zetu ziibwe bila huruma.

  Wajameni ninaomba mwenye utaratibu mwema wa kufungua kesi mahakama Kuu ya kuiomba mahakama imwamuru msajili wa vyama vya siasa aifute CCM aniletee hapa jukwaani au hata kwangu binafsi. Ninajiaminisha kuwa hii ni njia muafaka ya kuisaidia nchi yangu Tanzania kuondokana na jinamizi la mitupora.

  Please give out your technical view

  Sitanyamaza hadi CCM ifutwe
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa kuwa haja yako ni kuifuta kisheria, nakushauri nenda kaangalie mkataba ambao watanzania waliingia na watanzania kutawala. Humo naamini utaona kasoro nyingi sana na ukiukwaji mkubwa wa mkataba ambao CCM imeufanya. Utapata njia ya kuanzia
   
 3. M

  Masatu JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Simple! join Chadema...
   
 4. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2008
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,734
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  Mi naona hiyo ni njia ndefu sana. Mahakama zenyewe niza kwao sasa hiyo kesi naweza kwenda mpaka kiama? la msingi ninaloliona ni kujipanga vizuri 2010 kuimarisha vyama vyetu vya upinzani kama tukikosa urais basi angalau tuhakikishe wabunge zaidi ya 80% niwaupinzani tuweke mambo sawa 2015 tuchukue nchi jumla. na uzuri uliopo ni kwamba vyama vilivyochukua uhuru ukishavitoa madarakani ndio mwisho wao leo hii KANU iko wapi??? Tukaze buti Mola hamtupi mja wake.
   
 5. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2008
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Usipoteze muda wa kuhangaika kuifuta SISIEM, jifute wewe kwenye uanachama wao...! halafu tumia nguvu zako kuhimiza wengine wajifute kama wewe, halafu subiri 2010, tuwapigie CUF au Chadema kura.
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ikiwa kuna prufu walikwiba feza ya BOT na kuifanyia kampeni kinyume cha sheria ,hilo litakuwa kosa la jinai.
  Ikiwa ilitumia vyombo vya dola kukwiba matokeo Zanzibar hilo litakuwa kosa la jinai.
  Ikiwa ni chama pekee kinachotoa mafisadi hilo litakuwa kosa la uhaini.Hukumu yao ni kifo.
   
 7. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Inabidi utueleze zaidi CCM una maana gani?

  Wewe huoni ukiifuta ccm wale wana ccm watahamia CUF na kufanya u CCM ndani ya CUF.
  Mimi siku zote naamini na ndiyo imani yangu ya kwamba CHAMA chochote hakina ubaya ama uzuri ila wabaya ama wazuri ni BINADAMU.
  Nitarudia tena hii ndio imani yangu tatizo la umasikini wetu ni sisi wantanzania ndio tatizo.
  sisi watanzania tuna chuki binafsi sisi kwa sisi,tunapenda vitu vitukute tukiwa tunapiga stori,waoga wa ku risk,tupo kama kandoo fulani,wazee wa fitina,watu wasio penda maendeleo ya mwenzio nk.
   
 8. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mimi nitakuwa wa kwanza kuwapa hao Chadema na Caf kama wataungana tu na si vinginevyo wasije nao wakatufisadi.
   
 9. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Goodluck comes to those who do not wish for it.You are slowly digging your own grave!By the end of it all we will see what are fruits of your hardwork.
   
 10. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mpaka sasa kulingana na sheria ya vyama vya siasa nchini CCM ingetakiwa iwe iimefutwa. sheria inakataza chama caha siasa kufanya mambo yeyote ya kidini. ukisoma ilani ya CCM ya uchaguzi mwaka 2005 utakuta mambo ya Kidhis Court ambalo ni jambo la kidini. mchakato wa tanzania kujiunga na OIC umeanzishwa na CCM na ni kinyume na sheria ya vyama vya siasa pia. ukiangali kwa umakini mambo haya pia yanakiuka katiba. nipe muda nikufanyie research na niko tayari kukuandalia nyaraka zote za mahakama za kukifuta hiki chama. CCM has lost legitimacy in all fields of law in tz
   
 11. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2008
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,858
  Likes Received: 198
  Trophy Points: 160
  Itafutwa na wananchi ktk uchaguzi kwa sababu ya hali ngumu ya maisha. Hali inazidi kuwa ngumu hadi itafika mahala ukimwelewesha mjinga chanzo cha shida zake atakuelewa vizuri. Maana wakati huo atakuwa hata hajui mchana atakula nini. Na pengine hata chai atakuwa hajanywa. Patam hapo. So in election ataungana na wapenda mageuzi na hapo ndo CCM itafutika ktk siasa za Tanganyika.
   
 12. K

  Kifoi JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2008
  Joined: May 12, 2007
  Messages: 836
  Likes Received: 231
  Trophy Points: 60
  mutashidaje kwa kura wakati tume ya uchaguzi ni CCM watupu si kujidanganya tu kupiga kura.
   
 13. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #13
  Sep 3, 2008
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  hiyo sio complete soln
   
 14. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #14
  Sep 3, 2008
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  tusijedanganye na kujipotezea muda jamani hawa watu ni wezi wa kura kila mtu anajua, sis wananchi wenyewe hatuko serious na mabadiliko ya kweli huu muamko ulioko hapa ni mdogo sana kulinganisha na kura zinaotakiwa kuing'oa CCM some serious business shuold be done kama hatuta amka na kufanya mabadiliko yakiambatana na kujitolea kwa ukweli na kwa moyo tutabaki hapa hapa, hali halisi ya kushindwa na kuzidiwa mashambulizi ni baada ya ile hotuba ya kijinga ya JK, hiyo imezima kila kitu kilamtu yuko kimya hata mitaana watu hawana muda tena wa kujadili siasa, kila mtu amechka kabisa, na hapo ndio upenya mzuri wa hawa wezi

  SOMETHING SERIOUS SHOULD BE DONE
   
 15. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #15
  Sep 3, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Absalom Kibanda


  NAPENDA kuanza kutumia fursa hii ya leo kwa kueleza kwa kiapo kwamba: ‘‘Mimi Absalom Kibanda ni mwanahabari nisiyefungamana na chama chochote cha siasa kwa maana ya kiitikadi na sitarajii japo kwa wakati huu, kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa miongoni mwa hivi vilivyosajiliwa, hususan wakati nikiendelea na kazi hii ya uanahabari.”

  Nimelazimika kuanza kwa kueleza waziwazi msimamo wangu huo kutokana na ukweli kwamba, maandishi ninayotarajia kuyaandika leo yanaweza yakapotoshwa na wanasiasa, wanahabari wenzangu, au wananchi wengine wa kawaida ambao kwa hulka ni wepesi kubebwa na pepo za kusi za kisiasa ambazo aghalabu zimekuwa zikiwakumba watu wengi, miongoni mwetu.

  Mada yangu leo hii imechochewa na hoja zilizotolewa katika siku za hivi karibuni kabisa na mwanasiasa wa siku nyingi, Kingunge Ngombale-Mwiru, ambaye kimsingi yeye ndiye mtu anayeweza akasimama kifua mbele akitamba kuwa mmoja wa wanasiasa wachache waliobakia walioshiriki kikamilifu kwa miaka mingi katika harakati na mikakati mbalimbali ya kisiasa ndani ya CCM na nje, pengine kuliko mwingine yeyote.

  Watu wanaomjua Kingunge wanafahamu kwamba kwa sasa yeye ndiye mtu pekee (nasisitiza pekee) aliyepata kuwatumikia kwa namna ya kuwa msaidizi wa karibu katika nyadhifa na nafasi mbalimbali marais wote wanne waliopata kuliongoza taifa hili, ukianza na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

  Kumbukumbu zinaonyesha kwamba, zama za Mwalimu, enzi hizo Kingunge akijulikana kuwa kada mwadilifu wa TANU na baadaye CCM akivaa joho la kikomunisti zaidi kuliko alivyokuwa mjamaa, mwanasiasa huyu alikuwa akishirikiana na wanasiasa wa kariba ya kina Paul Sozigwa, Daudi Mwakawago katika kuandaa programu za chama, ilani za uchaguzi na maandiko mengine mbalimbali ya kiitikadi.

  Aliendelea kuwa mtu wa karibu na kwa mara ya kwanza akaingizwa serikalini wakati wa Serikali ya Awamu ya Pili (1985-1995), iliyokuwa ikiongozwa na mzee Ali Hassan Mwinyi, na kwa namna ya pekee yeye na Rashid Mfaume Kawawa wakawa wakionekana kuwa watu waliokuwa na jukumu la kuendeleza msingi wa kiitikadi na kiuongozi waliokuwa wameanza kuujenga wakati wa Mwalimu.

  Katika mazingira ya ajabu kabisa, Kingunge aliweza kuvaa vyema sera za ruksa zilizokwenda sambamba na kuanguka kwa mfumo dume wa kikomunisti duniani na hata yalipotokea mabadiliko ya Glasnots na Perestroika kule Urusi chini ya uongozi wa Mikhail Gorbachev, mwanasiasa huyo gwiji hapa nchini aliendelea kustawi, kinyume cha matarajio ya wengi, ambao wakati huo walidhani angeporomoka sambamba na kuporomoka kwa ukomunisti. Haikuwa hivyo.

  Kama hiyo haitoshi, Kingunge ambaye alikuwa jemedari wa mfumo wa kidikteta wa chama kimoja, akionekana juu juu kuwa mfuasi wa falsafa za Ki-Marxist na Ki-Leninist, ghafla alionekana akikubali kuingia kwa mfumo wa vyama vingi hapa nchini kwa namna ile ile walivyofanya Baba wa Taifa na Rais Mwinyi.

  Katika hali ya kustaajabisha, Kingunge alionekana kubadilika, na kitu pekee alichoonekana kuendelea kubakia nacho kilikuwa ni mavazi yake yale yale ya Chou en Lai na suti za kaunda na ngouabi, alizokuwa ameanza kuzivaa tangu zama akiwa kada mkomunisti (kimaandishi).

  Hali hiyo ya Kingunge kumudu vishindo vya mabadiliko, ilimpa fursa ya kuingia salama katika Serikali ya Awamu ya Tatu ya Benjamin Mkapa, kwanza akijenga msingi wa ushindi wa kuingia ikulu kwa kiongozi huyo na kisha akamfanya mshauri wake mkuu wa masuala ya siasa na mtu wake wa karibu kabisa katika masuala yote muhimu ya kisiasa na kisera.

  Akiwa mmoja wa wandani wa kisiasa wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Kingunge anatajwa kuwa mmoja wa watu waliopenyeza hoja ya kumhalalisha Kikwete machoni mwa Mkapa na huku akitumia uzoefu mkubwa wa propaganda za siri na za wazi, akamwezesha kupenya vihunzi vigumu kabisa vya uteuzi, akisaidiana na watu wengine kadhaa ndani ya serikali na wale wa CCM. Huyo ndiye Kingunge.

  Wakati fulani nilipokuwa nikijadili na wenzangu wawili, watatu ni siri gani hasa iliyomwezesha Kingunge akafanikiwa kupenya vishindo vyote vya kisiasa na hata kuweza kumudu kuwa kipenzi cha marais wote wanne wa nchi hii, tulijikuta tukitoa maoni tofauti kuhusu jambo hilo.

  Leo hii kwa zaidi ya miaka 35, Kingunge ndiye mtu anayetajwa kuwa mwanasiasa aliyedumu kwa muda mrefu katika mzingo unaowazunguka viongozi wakuu katika taifa hili, hali ambayo imemfanya ajijengee jeuri ya kimamlaka inayomwezesha kunyosha kidole kwa kada mwingine yeyote yule ndani ya chama chao na wakati mwingine hata kwa wale walio nje ya serikali.

  Hii ndiyo jeuri ambayo Kingunge aliitumia wiki iliyopita alipoibuka na akawashutumu waziwazi wabunge wenzake wa ndani ya CCM hususan wale waliojijengea tabia ya kukikosoa hadharani Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake. Amewashangaa viongozi wa chama hicho wanaoiponda serikali kwa madai ya kutetea masilahi ya taifa.

  Katika hali ya kujiamini, Kingunge akitumia nadharia za ‘chama kushika hatamu’ na ile ya ‘huyu si mwenzetu’ alizoshiriki kuziasisi na kuzihalalisha miaka ya 1980 na 1990, alifikia hatua ya kuwaonya kina Samuel Sitta, Anne Kilango, Aloyce Kimaro na wenzao wengine kutodhani kwamba wao wanaweza wakawa maarufu kuliko kilivyo chama chao.

  Kwa maneno yake mwenyewe alisema, ninamnukuu: ‘‘Wanaodhani umaarufu walionao umetokana na wao wenyewe, wanajidanganya, hebu wasimame peke yao tuwaone kama wataendelea kuwa maarufu. Wanapaswa kujua kuwa, umaarufu wao unatokana na chama na madaraka waliyonayo yametokana na chama.”

  Hakuishia hapo alikwenda mbele zaidi na kusema kwamba, hivi sasa kundi la wana CCM hao wanaodakia hoja za wapinzani wamejikuta pasipo wao wenyewe kujua wakiwasaidia wapinzani katika kukivuruga chama hicho tawala na serikali yake kwa kisingizio cha kusimamia masilahi ya taifa.

  Katika hili, alisema katika siku za hivi karibuni kumezuka tabia ya wabunge wa upinzani kuanzisha hoja na kudai si ya upinzani bali ya kitaifa, hali inayosababisha baadhi ya wabunge wa CCM kujiingiza katika kutetea hoja hizo bila kujua kwamba kwa kufanya hivyo, wanakidhoofisha chama chao. Huu ni ukweli mtakatifu; mpuuzeni Kingunge.

  “Umezuka mtindo hivi sasa, wapinzani wanaibua hoja, ili kuwakamata vizuri CCM, wanasema hoja hii ni ya kitaifa, kwa masilahi ya wananchi, hivyo viongozi wetu wa CCM nao wanajikuta wakiingia katika mijadala hiyo bila kujua kwamba wanachofanya ni kukidhoofisha chama.

  “Umaarufu wa magazetini haufai, ni wa kupita tu, na inapofikia kipindi fulani, hata hayo magazeti yanakusahau, wapo wengi tuliwaona, lakini wako wapi sasa?” alihoji Kingunge katika kauli ambayo kwa yakini huenda ilikuwa ikiwalenga makada wa zamani wa CCM wa aina ya Augustine Mrema, ambao umaarufu wao umekuwa ukipungua kila kukicha tangu walipojitoa katika chama hicho tawala. Huu ni ukweli mchungu kwa kila mpenda demokrasia.

  Alipoona hoja yake pengine inaweza kukosa mashiko, Kingunge aliendelea mbele na kusema; “wapinzani hawana hoja wala sera za kueleweka, ndiyo maana wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali za kuwarubuni wana CCM kwa kuwataka wachangie hoja zao baada ya kuzipa nguvu na kuziita hoja za kitaifa. Tumegundua nia ya wapinzani ni kutaka kukidhoofisha chama chetu, hawawezi na sisi tumejipanga imara, si tu kwamba wakinawa hawatakula, bali pia hawatakiwi hata kunawa.”

  Ni jambo la bahati njema kwamba, tayari wanasiasa kama Sitta, Kilango na Kimaro, kwa nyakati na sehemu tofauti wamezijibu hoja zote zilizotolewa na Kingunge na kimsingi wote wamezipinga na huku wakitoa maelezo tofauti, wameonekana kuzipuuza. Wanafanya makosa makubwa.

  Nasema hivyo kwa sababu, alichokisema Kingunge siyo chake, ni maoni binafsi ya viongozi wenzake wa juu kabisa serikalini, na kwa hakika yanaweza yakawa ndiyo maoni binafsi ya Rais Kikwete kwa wana CCM wenzake wa aina ya kina Sitta, Kilango na wenzao.

  Historia ya Kingunge iliyomwezesha kudumu katika akili za marais wote wanne wa Tanzania, akiimba nyimbo za kila mmoja wao kwa wakati wake, akicheza nao muziki kwa kufuatisha midundo ile ile kwa kila rais na sasa hivi akiwa miongoni mwa waasisi na watekelezaji wa mirindimo ya kasi mpya, ari mpya na nguvu mpya, ni ushahidi wa wazi kwamba alichokisema ndicho anachokiwaza Kikwete.

  Lakini pengine kikubwa zaidi ni kwamba, alichokisema Kingunge si tu kwamba ni mawazo ya wakuu wake ndani ya CCM na serikalini, bali ndiyo taswira halisi ya aina ya CCM ambayo yeye na makada wenzake waliijenga kwa miaka mingi na ambayo wamekuwa wakijaribu kuiendeleza hata katika zama hizi za mabadiliko makubwa ya kidemokrasia.

  Watu wanaoijua CCM ya awamu ya kwanza hadi hii ya nne, wanafahamu kwamba, chama hiki tawala katika kipindi chote cha uhai wake kimeendelea kubakia na sura yake ile ile ya chama dola cha kisiasa na ambacho kinatumia mamlaka zake na historia zake kuendeleza udikteta wa kifikra na kimaamuzi kikitawala mawazo ya mtu mmoja mmoja.

  Watu wanaoijua vyema CCM na historia yake wanatambua kwamba, chama hiki hadi hivi leo kimeendelea kuwa na fikra zile zile za Zidumu Fikra Sahihi za Mwenyekiti (Nyerere, Mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete), hata kama fikra hizo zinakinzana na ukweli wa sasa wa mambo na hali halisi ya wakati.

  Watu wanaoijua vyema CCM na historia yake, wanatambua fika kwamba, chama hiki kimekuwa na desturi ya kuwaliza na kuwatisha kisiasa makada wake wote wanaojiinua na kujaribu kupingana nacho, wakigusa msingi wa kuwapo kwake na kuendelea kutawala kwake kwa namna ile ile kilivyopata kufanya kwa kina Maalim Seif Sharif Hamad, Horace Kolimba, Augustine Mrema na wengine wengi.

  Kwa nini basi tusiamini kuwa chama hicho kinajaribu kufanya hivyo hivyo sasa kwa akina Sitta, Kilango, Kimaro, Mwakyembe, Ole Sendeka na wenzao wengine wengi!

  Watu wanaoijua CCM vyema na historia yake ni mashahidi wazuri wa namna chama hicho kilivyo tayari kutumia nguvu zake zote, halali au batili za kuua upinzani wowote makini kikijenga hoja za kuwachonganisha wanasiasa wa upinzani na wananchi kwa namna kinavyofanya sasa dhidi ya CUF Zanzibar, kilivyofanya kwa NCCR- Mageuzi miaka 10 na ushei iliyopita na sasa kinafanya hivyo tena kwa CHADEMA.

  Kwa kutambua ukweli huo basi, Watanzania wapenda demokrasia wanao wajibu wa kuukubali ukweli kwamba wakati wa CCM na akina Kingunge kuendeleza hali hii inayokifanya chama hiki kuwa na nguvu kubwa mno kinapolinganishwa na vyama vingine vya upinzani umepita na siri iliyo nyuma ya kuondokana na hali hiyo ni rahisi kabisa; kukiua chama hicho kwa kukimega vipande viwili.

  Ajenda ya kukimega chama hicho ambacho muasisi wake Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alipata kusema ‘upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM’ inapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania anayeitakia mema nchi hii huko tuendako, na ambaye kwa hakika na kwa dhati kabisa atakuwa akipingana na mawazo na maoni ya watu wa aina ya Kingunge, Kikwete na wenzao ambao ndoto yao ni kukiona chama hicho kikiendelea kustawi kama chama kimoja chenye nguvu kubwa.

  Tufanye vipi basi kutimiza ndoto hiyo njema ya Baba wa Taifa? Njia ni rahisi japo itahitaji watu wenye uwezo wa kujitoa mhanga walio ndani ya chama hicho tawala. Ni ndoto inayohitaji kuwaona wana CCM wazito kimamlaka ndani ya chama hicho na serikalini wakiungana na kujitoa ndani ya chama hicho kwa kishindo, wakipinga ufisadi, uzushi, kufitinishana, kusingiziana, kumalizana kisiasa, kugombea madaraka kwa kiwango cha kuwa tayari kufanya lolote la heri au la shari ili kulinusuru taifa hili changa. Huko ndiko tunakopaswa kwenda. Tuonane wiki ijayo Mungu akipenda.
   
 16. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #16
  Sep 3, 2008
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  kwanza lzm CUF na CHADEMA waungane if we are really serious into it
   
 17. K

  Kjnne46 Member

  #17
  Sep 3, 2008
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Namuunga mkono Ochu lakini amekosea kutaja suala la Kadhi na OIC kwani "havipo" kwa sasa. Lakini angezungumzia CCM imeidhinisha UBALOZI WA VATICAN ambao ni wa KIDINI (TZ sio ya Wakatoliki pekee) na baya zaidi WANANCHI WOTE WANALAZIMISHWA KUPUMZIKA JUMAPILI Serikalini, Asisi zake, mashuleni, ma-SU, n.k. hata ukiwa Sabato, Hindu, Mwislamu au huna dini. Huo ni ukiukwaji wa Ibara nyingi tu za Katiba ya Nchi.

  Pili, katika mikakati ya kuing'oa CCM wananchi wanaweza kusaini petition kwa wingi ama kwa lengo ya kukishitaki Chama au hata kuwaondoa uwakilishi Wabunge wake, yaani "vote of NO CONFIDENCE". Sijasikia TZ Mbunge ye yote ameondolewa na Wananchi ingawa wengi wao hawawatumikii walala-hoi na huwa wanawatembelea vijijini wakati wa kampeni tu lakini wakishachaguliwa mashangingi yao hayaonekani tena.

  Tatu, ufumbuzi wa uhakika ni Vyama vingine viungane kuipiku CCM katika Uchaguzi kama walivyofanya Kenya ila matatizo ni: a) havitaki kuongozwa na CUF ingawa ndicho tishio la CCM eti kwa sababu ni cha Waislamu, b) viongozi wa upinzani kila mmoja nataka awe Rais yeye. Wakiafikiana haya mawili mimi naona CCM itango'ka kupitia upigaji kura.
   
 18. M

  Mama JF-Expert Member

  #18
  Sep 3, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  haitatokea labda karne ijayo,
   
 19. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #19
  Sep 3, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,648
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Implication ya ombi lako ni kwamba umeng'amua CCM haiwezi kuondolewa madarakani kupitia ushindani wa kura kwenye uchaguzi mkuu, kwa hiyo unataka eti CCM ifutwe kupitia mahakama?! Hiyo ni nonsense kwani mtu yeyote ikiwemo wewe mwenyewe unajua fika kuwa kitu kama hicho hakiwezi kutokea hata siku moja. Kwa maana hiyo swali lako ni batili na isitoshe sababu ulizoandika hazitoshi kama kudai eti chama cha siasa kifutwe. Wapiga kura ndiyo waamuzi wa suala la kuendelea kuiweka madarakani CCM au kutaka mabadiliko ya utawala.
   
 20. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #20
  Sep 3, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mnataka kuiua CCM, simple chukua formula hii,

  Opposition parties waende vijijini ambako ndiko watanzania wengi walipo na ambao ndiyo wanaitambua CCM na kuipigia kura. Wafungue matawi na wahakikishe wanapata wanachama ambao wataweza kuwaunganisha nchi nzima.

  Hapo mtaweza kuiua CCM, lakini kama ni maneno tu na kufikiria kwenda Ikulu (Kukamata executive power) bila ya kuongeza wabunge (Kukamata legislative power), mtabakia na maneno hivihivi miaka nenda miaka rudi.

  Mnapoteza muda wenu kumjadili Kingunge, laiti kama mngeamua kujadili maneno yake nadhani mngekuwa mmepata tuition ya bure kutoka kwa yule babu.
  Lakini hata hivyo mnahiyari ya kuchukua kile ambacho mnadhani ni kizuri kwenu hata kama hakiwasaidii.
   
Loading...