Mhindih
JF-Expert Member
- Mar 14, 2011
- 331
- 68
Habari wanaJF ni matumaini yangu hamjambo. Tafadhali naombeni msaada wenu.Nina mdogo wangu ana umri wa miaka 11 na miezi kama 8 hivi yuko darasa la 6 ametuhumiwa kesi ya kulawiti mtoto wa jirani yetu mwenye miaka 8 akiwa na wenzake watano. Januari mwaka huu alichukuliwa kwenda polisi tulipofika ndio tukaambiwa kuwa mnamo tarehe kati ya 24-27 mwezi wa 12 mwaka jana akiwa na wenzake watano walimlawiti mtoto mwenzao.Ikabidi tuulize kwa nini mlalamikaji amechelewa kutoa taarifa polisi? Tukaambiwa kuwa taarifa ilifika ila aliekuwa amefungua jalada alichukua likizo hivo sasa ndio ametoka likizo. Tukiwa police watoto walipigwa sana hadi kufikia mdogo wangu kukubali kuwa kweli alishiriki. Hapo police mama wa mtoto (mlalamikaji) alitoa cheti kutoka kwa daktari kuonyesha kuwa ni kweli alifanyiwa vitendo vya kinyama. Baada ya uchunguzi watoto 4 waachiwa kwa vigezo kuwa walio juu ya miaka 12 kesi itaenda mahakamani na waliochini ya miaka 12 wameachiwa.Kweli kesi imeenda mahakamani na tumeambia kesi itatajwa tarehe 6/3/2012. Naombeni msaada wenu wa kisheria ili nimsaidie dogo ukizingatia yuko shule na muda wa masomo anapoteza kwa ajili ya kufuatilia kesi. Nawasilisha samahani kwa maelezo marefu