Naomba Msaada wa Haraka, Possibly From Christians!!

Naomba Msaada wa Haraka, Possibly From Christians!!

Chige

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2008
Posts
13,493
Reaction score
29,888
Guys,

Naomba msaada wa haraka kuhusu neno "VILASI."

Nadhani hili neno linahusiana na masuala ya ubatizo; sasa kuna kifungu cha maneno nimekutana nacho ambacho natakiwa kukitafsiri kwenda Kiingereza! Sentensi zenyewe zinasema:
  • Tarehe ya kufunga vilasi vya usomaji
  • Tarehe ya kufunga vilasi vya watu.
So, hiyo vilasi ni nini? Na nini tafsiri yake in English?
 
Inaweza kuwa "lessons?"

Baada ya ku-Google nikakutana na hii habari:
Kim kwa sasa ameanza kuchukua vilasi vya kujifunza nyimbo na ameshajitokeza katika video moja na Kanye ambayo alionyeshwa akiwa nusu uchi juu ya pikipiki.

Nikatafuta English article inayokaribiana na hiyo habari:
Kim has been taking singing lessons, because Kanye has a ton of faith in her career!


Kama ni lessons, hiyo vilasi vya usomaji ni "studying lessons" au "reading lessons?"
 
Duh! Hapa unaweza kufiwa na mgonjwa mikononi!!!
 
Mkuu, nimejaribu kutafuta vyanzo mbalimbali ambavyo vina neno VILASI... Nahisi lina maana ya nyumba fulani hivi, mithili ya sehemu ya kujisomea au bweni (sina uhakika). Kama sivyo basi litakuwa ni neno tata (lina maana zaidi ya moja). Tiririka nazo halafu uhusianishe na muktadha wa makala yako...

Bw. Kakol alimuuliza Waziri wa Nyumba na Huduma za Starehe kuna VILASI vingapi vya elimu ya watu wazima katika tarafa ya Yatta na Wizara inao mpango gani wa kuinua elimu ya watu wazima katika sehemu hiyo.

Wizara yangu ya Elimu inafahamu sana matatizo ambayo wazazi wanapata wakati wanajaribu kujenga VILASI vya kusomea watoto wa shule za msingi, yaani primary, na pia nyumba za kulala waalimu. Lakini kwa vile, Bw. Spika, Wizara yangu haina pesa za kutosha za kujaribu kusaidia katika mipango hiyo ya kujenga MAJUMBA, kwa wakati huu hatuna njia ambayo tunaweza kusaidia katika ujenzi wa nyumba za kulala za waalimu katika shule za msingi na VILASI vya kusomea watoto. Kitu ambacho tunatumainia, Bw. Spika, ni kwamba wananchi pamoja na viongozi kama Wanabunge watashirikiana katika mwito wa kufanya kazi pamoja ili wajaribu kuondoa tatizo hilo katika nchi yetu ya Kenya.

Pesa tulizonazo kwa wakati huu tunajaribu kutengeneza nyumba za kulala waalimu, na VILASI katika shule za secondary pamoja na colleges ambazo waalimu hufundishwa, na huo ni mzigo ambao Serikali inajaribu kuuondoa. Lakini kwa wakati huu hatuna njia ya kusaidia isipokuwa katika shule ambazo WATOTO WANALALA NDANI, katika sehemu ambazo watu hawawezi kujimudu kama Turkana, Mandera, na penginepo.

Nb: Hizo ni aya ambazo zimetoka katika vyanzo viwili tofauti ila nahisi vinaendana.
 
Nahisi tu kwa sababu sijakuta neno hili bado (au sikumbuki?). Kutokana mifano hapo juu inaonekana asili yake ni Kiingereza
"class" = klasi = kilasi, halafu kwa njia ya kuiswahilisha zaidi ungepata uwingi "vilasi".
Inawezakana, je?
 
Back
Top Bottom