Naomba msaada simu bora

Naomba msaada simu bora

Sim za sasa hivi watu wengi wanalia network. Simu unanunua vizuri iko safi lakini baada ya miezi kadhaa utakuta unashindwa kuingia internet hata km uko karibu na mnara
99% ni setting za wap ambazo huletwa automatic ukibadili line au kureset au simu mpya
 
Pls mkuu na mm cm yngu ni huawei ascending 630 inasumbua SNA upande wa network cjui ni kwnn hta nkitumia line ya Halotel wkt cm nyngne ni za kaida SNA wakitumia Halotel zinakamata hadi H plus ila kwngu ni tofaut.msada wako chief-mkwawa
network ya kupiga simu au internet?
 
mkuu siku nyengine usiandike jina langu kwenye kichwa cha habari kama ni message yangu tu tafadhali nitumie kama private msg sababu unazuia watu wengine kuchangia uzi huu.

kati ya hizo simu kuna hata moja unayo? haswa haswa hio galaxy s6 na A8 maana kwa muono wangu simu nyingi za around budget hio zinafanana na hizo, badala ya kukimbilia kununua simu mpya tunaweza tukazirekebisha hizo hizo. na zilipopata matatizo ulizipeleka samsung shop?

pia kuna jambo jengine muhimu unatakiwa ulijue, simu za maduka yetu kibongo bongo asilimia 90 sio mpya ni refurbished wanazitoa masoko ya korea, china na marekani kuja kuzitupa huku hivyo unaponunua simu Tanzania double check ni version ya Kimataifa ambayo huuzwa kwetu na pia utume imei yake kwenda namba ya samsung ili kuhakiki zaidi. mfano unakuta simu kainunua mzungu marekani huko ina tatizo kairudisha kwenye kampuni then inaenda kurekebishwa na kuja kuuzwa kwa bei nafuu, wafanya biashara wa bongo huzinunua zile simu nafuu na kuja kuziuza huku, kama unataka kuspend hela nyingi kama hivyo hakikisha ni version ya kimataifa, kuwa safe zaidi kanunue duka la samsung official.

kuhusu network, ikiwa ni simu ya nje ambayo wameunlock na sio iliotengenezwa kwa ajili ya Tanzania unaweza kupata Tatizo la network sababu modem yake ni Tofauti, pia simu za Alluminium hazishiki vizuri Network kutokana na material yake compare na za plastic, hivyo kama eneo lako lina shida ya network pendelea zaidi simu za plastic au kama zinakuwa na alluminium iwe ni frame tu na sio full body.

kuhusu ku overheart almost simu yoyote yenye perfomance kubwa itapata moto, unachotakiwa ni kufunga apps usipotumia au kuweka battery server ili kudownclock processor simu isipate moto.

kama hizo simu hapo juu huna tena unaweza subiri miezi kadhaa ikitoka s8 basi s7 zitashuka sana bei, samsung kuacha utengenezaji wa note 7 kumefanya thamani ya s7 isishuke hivyo itakuwa ngumu kuipata budget hio (japo inawezekana kuipata), sababu umeshatumia s6 sioni simu nyengine ya kukushauri zaidi ya s7 na flagship za mwaka 2016. sema kutokana na warranty za samsung Tanzania sioni maana ya kununua kampuni za brand nyengine ambazo hata service centre hawana, labda Huawei kidogo na simu kama Honor 8 kama wataileta itamake sense budget hio.
Kaka unacho zungumza nichakweli kabisa mimi mwenyewe nilikuwa nanunu sim kwenye maduka ya kitaa ukiitumiq ikimaliza mwozi itaqnza kuzinguwa ila tangu nilipo anza kununuwa sim ha kwenye maduka ya samsung sijaona matatizo kabisa hata kama sim inapata tatizo huwa nawaperekea kama inatatizo dogo wanatengeza bure hata mia sitow
 
1. angalia kama huna setting za wap fanya hivi

nenda setting then more network then mobile networks then acess point name, hapo utaona list ya setting za simu na kama huna setting kutakua kweupe

bonyeza dots tatu za juu au click menu button utaona create new apn click hapo au unaweza ona neno add au kijumlisha
-connection name andika neno lolote
-apn andika internet (kama ni halotel b-internet)

bonyeza menu key click save kama hakuna just back then utaiona setting yako mpya, iekee dot kwa mbele kuiactivate

2. sometime mtandao fulani eneo lako hivyo jaribu pia kubadili line
 
mkuu siku nyengine usiandike jina langu kwenye kichwa cha habari kama ni message yangu tu tafadhali nitumie kama private msg sababu unazuia watu wengine kuchangia uzi huu.

kati ya hizo simu kuna hata moja unayo? haswa haswa hio galaxy s6 na A8 maana kwa muono wangu simu nyingi za around budget hio zinafanana na hizo, badala ya kukimbilia kununua simu mpya tunaweza tukazirekebisha hizo hizo. na zilipopata matatizo ulizipeleka samsung shop?

pia kuna jambo jengine muhimu unatakiwa ulijue, simu za maduka yetu kibongo bongo asilimia 90 sio mpya ni refurbished wanazitoa masoko ya korea, china na marekani kuja kuzitupa huku hivyo unaponunua simu Tanzania double check ni version ya Kimataifa ambayo huuzwa kwetu na pia utume imei yake kwenda namba ya samsung ili kuhakiki zaidi. mfano unakuta simu kainunua mzungu marekani huko ina tatizo kairudisha kwenye kampuni then inaenda kurekebishwa na kuja kuuzwa kwa bei nafuu, wafanya biashara wa bongo huzinunua zile simu nafuu na kuja kuziuza huku, kama unataka kuspend hela nyingi kama hivyo hakikisha ni version ya kimataifa, kuwa safe zaidi kanunue duka la samsung official.

kuhusu network, ikiwa ni simu ya nje ambayo wameunlock na sio iliotengenezwa kwa ajili ya Tanzania unaweza kupata Tatizo la network sababu modem yake ni Tofauti, pia simu za Alluminium hazishiki vizuri Network kutokana na material yake compare na za plastic, hivyo kama eneo lako lina shida ya network pendelea zaidi simu za plastic au kama zinakuwa na alluminium iwe ni frame tu na sio full body.

kuhusu ku overheart almost simu yoyote yenye perfomance kubwa itapata moto, unachotakiwa ni kufunga apps usipotumia au kuweka battery server ili kudownclock processor simu isipate moto.

kama hizo simu hapo juu huna tena unaweza subiri miezi kadhaa ikitoka s8 basi s7 zitashuka sana bei, samsung kuacha utengenezaji wa note 7 kumefanya thamani ya s7 isishuke hivyo itakuwa ngumu kuipata budget hio (japo inawezekana kuipata), sababu umeshatumia s6 sioni simu nyengine ya kukushauri zaidi ya s7 na flagship za mwaka 2016. sema kutokana na warranty za samsung Tanzania sioni maana ya kununua kampuni za brand nyengine ambazo hata service centre hawana, labda Huawei kidogo na simu kama Honor 8 kama wataileta itamake sense budget hio.
Shukran sana , pia nimekuelewa kwa ushauri wako. A8 bado ninayo naomba unielekeze ni wapi ntakupata kwa marekebisho meanwhile tukisubiri hiyo version mpya
 
mimi sio fundi mkuu, cha muhimu kwanza hapo ni kuhakikisha ni international version na ina warranty hapa Tanzania ili uipeleke samsung shop wakaitengeneze bure.

nenda setting halafu about nisomee model yake. itakuwa mfumo kama huu sm-A800F au sm-A800S etc
 
SM-A800F,,,,version..A800FXXU1AOJ1
 
tuma imei yake kwenda 15685 kwa mfumo huu
REG*IMEI# badili hilo neno imei eka imei yako ya simu
unsuccessful "Phone is Possibly a grey Import"

Lakini wakati wa zoezi la kuhakiki feki jibu lilikuwa simu ni genuine inakuwaje ?
 
inamaanisha simu ni original lakini haikutengenezwa kwa ajili ya soko letu. ndio hapo unapopata conflict ya modem na band.

maana ya grey import ni vitu ambazo vinaingizwa kwenye soko na watu ambao hawatambuliki na wahusika waliotengeneza hivyo vitu.

soko letu ndio limejaa hizi bidhaa, na nyingi zao ni bidhaa mbovu zilizokataliwa huko duniani.
 
Asante sana , kuna namna yeyote ya ku set ili iweze ku match na modem na band zetu ?
 
Iphone kuanzia 4 kwenda juu ziko poa sana lkn kwa budget yako iphone 6 unapata na n simu poa sana
 
Asante sana , kuna namna yeyote ya ku set ili iweze ku match na modem na band zetu ?
hakuna mkuu sababu antenna ni hardware,

japo kuna baadhi ya simu unaweza kutweak modem ukazipata ila hizi zinakuwa tayari zilikuwemo kwenye simu zilikuwa disabled tu.

jaribu kutafuta mtandao wenye signal nzuri za internet utumie huo na line yako ya kupiga na kupokea iwe line 2 sababu 2g haizingui kwenye mtandao.
 
Ok shukran sana nimekuelewa
 
Back
Top Bottom