Naomba msaada napata shida kutumia ufunguo wa spear wa gari

Mnandi

Senior Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
156
Reaction score
28
Habari zenu wakuu, nina shida kidogo nahitaji ufumbuzi. Miezi miwili iliopita nilinunua gari toka Japan (2001 Land Cruiser Prado) na kwa sasa limeshafika na nimeanza kulitumia. Tatizo ni kwamba, limekuja na funguo mmoja tu ambao ni Master Key. Kwakuwa nina uzoefu wa siku nyingi wa magari, naelewa umuhimu wa kuwa na funguo wa Spare.

Niliamua kwenda kwa Lock Smith anichongee funguo wa spare. Funguo ulichongwa vizuri lakini kila ninapochomeka kwenye gari kuliwasha haliwaki. Nikiweka funguo uliokuja na gari linawaka. Sasa nimegundua kuna taa flani nyekundu kwenye dashboard huwa inawaka muda wote ila nikichomeka funguo uliokuja na gari ile taa inazima.

Nikichomeka funguo niliochongesha kwa locksmith ile taa haizimi inaendelea kuwaka. Jana niliamua kwenda Toyota na kuwaeleza shida yangu wakaniambia funguo wa Spare ni $500 ambayo ni approximately 840,000/=. Gari nililokuwa natumia mwanzo halikuwa na funguo wa spare lakini nilichonga funguo wa spare kwa shilingi 10,000/= tu na ulifanya kazi bila tatizo.

Mwenye ujuzi wa haya mambo ya funguo za magari tafadhali tushirikishane ili kama kuna namna ya kuokoa jahazi nifanye hivyo. Otherwise itanibidi tu kwenda Toyota kulipia kiasi hicho cha fedha nipate spare key.

Shukrani.
Cc: LEGE , CYBERTEQ

Ufunguo wenye logo ya Toyota ndio uliokuja na gari na huo mwingine umeandikwa JMA ndio niliochongesha.
25yy5n7.jpg
wcjllg.jpg

-> hapa hiyo taa nyekundu yenye shape kama gari ikiwa inawaka kabla ya kuchomeka funguo uliokuja na gari.

2isgu1e.jpg

-> hapa baada ya kuchomeka funguo original wa gari taa ikazima

21brv3d.jpg
 
Habari zenu wakuu, nina shida kidogo nahitaji ufumbuzi. Miezi miwili iliopita nilinunua gari toka Japan (2001 Land Cruiser Prado) na kwa sasa limeshafika na nimeanza kulitumia. Tatizo ni kwamba, limekuja na funguo mmoja tu ambao ni Master Key. Kwakuwa nina uzoefu wa siku nyingi wa magari, naelewa umuhimu wa kuwa na funguo wa Spare. Niliamua kwenda kwa Lock Smith anichongee funguo wa spare. Funguo ulichongwa vizuri lakini kila ninapochomeka kwenye gari kuliwasha haliwaki. Nikiweka funguo uliokuja na gari linawaka. Sasa nimegundua kuna taa flani nyekundu kwenye dashboard huwa inawaka muda wote ila nikichomeka funguo uliokuja na gari ile taa inazima. Nikichomeka funguo niliochongesha kwa locksmith ile taa haizimi inaendelea kuwaka. Jana niliamua kwenda Toyota na kuwaeleza shida yangu wakaniambia funguo wa Spare ni $500 ambayo ni approximately 840,000/=. Gari nililokuwa natumia mwanzo halikuwa na funguo wa spare lakini nilichonga funguo wa spare kwa shilingi 10,000/= tu na ulifanya kazi bila tatizo. Mwenye ujuzi wa haya mambo ya funguo za magari tafadhali tushirikishane ili kama kuna namna ya kuokoa jahazi nifanye hivyo. Otherwise itanibidi tu kwenda Toyota kulipia kiasi hicho cha fedha nipate spare key.
Shukrani.
Cc: LEGE , CYBERTEQ

nakushauri nenda toyota wakutengenezee kwa hiyo usd500.ukilinganisha gharama ya gari lako na ufunguo wa tsh10000 hata wewe mwenyewe unalishushia hadhi.
 
Last edited by a moderator:
Funguo za magari toka japani kuanzia miaka ya 2000,hivi zimewekwa Computerized module ambayo inaongeza ulizi wa gari husika.Hii Module wakati unachomeka fungua na kupiga start ya gari inacheck serial Number ya Control Box ya gari husika ECU, kama sio sawa na serial yake kwenye funguo gari itawaka hiyo taa nyekundu na aitowaka.(kuna jamaa ana unversal Module Ametengeneza mwenyewe Huwa anawasha gari yeyote ila hutumia zaidi ya dakika 5 au kumi mpaka apate frequency usika) hapa Tanzania wapo watu wachache sana tunaoweza kuprogram funguo hizi mpya.Ata kama utachonga funguo mpya still kama aina chip itakuwa ni kazi bure kuwasha gari.
Mkuu Lenge nnaona yupo katika mchakato wa kuanza hii huduma officially hapa Dar all the Best.
Ndugu Mnandi last year tulichaji 4M kwa ajiri ya fungua ya lori la SCANIA na mmliki akubisha kulipa.vwkeydis.jpg29889-main-photo.jpge88f5af2c64528a28e3627f154027bac.gif
 
Funguo za magari toka japani kuanzia miaka ya 2000,hivi zimewekwa Computerized module ambayo inaongeza ulizi wa gari husika.Hii Module wakati unachomeka fungua na kupiga start ya gari inacheck serial Number ya Control Box ya gari husika ECU, kama sio sawa na serial yake kwenye funguo gari itawaka hiyo taa nyekundu na aitowaka.(kuna jamaa ana unversal Module Ametengeneza mwenyewe Huwa anawasha gari yeyote ila hutumia zaidi ya dakika 5 au kumi mpaka apate frequency usika) hapa Tanzania wapo watu wachache sana tunaoweza kuprogram funguo hizi mpya.Ata kama utachonga funguo mpya still kama aina chip itakuwa ni kazi bure kuwasha gari.
Mkuu Lenge nnaona yupo katika mchakato wa kuanza hii huduma officially hapa Dar all the Best.
Ndugu Mnandi last year tulichaji 4M kwa ajiri ya fungua ya lori la SCANIA na mmliki akubisha kulipa.
mkuu kwahiyo gharama yenu itakuwa kiasi gani?
nakushauri nenda toyota wakutengenezee kwa hiyo usd500.ukilinganisha gharama ya gari lako na ufunguo wa tsh10000 hata wewe mwenyewe unalishushia hadhi.
nashkuru sana kwa ushauri mkuu, naamini hapa Tanzania kuna mafundi wazuri tu ambao wanaweza kulishughulikia swala hili kwa gharama nafuu bila kuharibu gari yangu. Nikikosa itanilazimu kurudi kwa dealer tu
 
mkuu kwahiyo gharama yenu itakuwa kiasi gani?
nashkuru sana kwa ushauri mkuu, naamini hapa Tanzania kuna mafundi wazuri tu ambao wanaweza kulishughulikia swala hili kwa gharama nafuu bila kuharibu gari yangu. Nikikosa itanilazimu kurudi kwa dealer tu

Mkuu nnnandi , maelezo aliyotoa Chipukizi hapo juu yako sahihi kabisa, funguo bila hiyo chip inayosomeka kwenye control unit haiwezi kuwasha. China ni chimbo la kila kitu, kuna kampuni zinatengeza blank key ambayo inakuwa na transponder kulingana na aina ya gari (number ya chip iliyoko kwenye funguo ya gari yako), inakuwa na template ya funguo kabisa unapeleka kwa fundi wa kuchonga funguo anakuchongea inakuwa kama original tu.
funguo.jpg
 
Mnandi kinachotakiwa hapo kwanza ni kuupata huo funguo wenye transponder chip iliyo compatible na gari lako alafu ndio uwe programmed kuwasha gari lako. Programming inaweza kufanyika Manually (process zinatofautiana kati ya magari) au kwa kutumia Key Programmer ya gari husika. Gari lako lina "immobilizer System". Kazi ya immobilizer system ni kuzuia wizi wa gari kwa kutumia funguo malaya au kwa kufanya 'hot wiring'. Hii system inafanya kazi kwa kuDisconnect fuel supply kwenye engine mpaka utakapoweka funguo original za gari. Kama upo Arusha nitafute kwa 0716-904626 / 0767-174757 ili nikusaidie upate funguo ya Spare..

images
10hr9ee.jpg
images
images
 
Habari zenu wakuu, nina shida kidogo nahitaji ufumbuzi. Miezi miwili iliopita nilinunua gari toka Japan (2001 Land Cruiser Prado) na kwa sasa limeshafika na nimeanza kulitumia. Tatizo ni kwamba, limekuja na funguo mmoja tu ambao ni Master Key. Kwakuwa nina uzoefu wa siku nyingi wa magari, naelewa umuhimu wa kuwa na funguo wa Spare. Niliamua kwenda kwa Lock Smith anichongee funguo wa spare. Funguo ulichongwa vizuri lakini kila ninapochomeka kwenye gari kuliwasha haliwaki. Nikiweka funguo uliokuja na gari linawaka. Sasa nimegundua kuna taa flani nyekundu kwenye dashboard huwa inawaka muda wote ila nikichomeka funguo uliokuja na gari ile taa inazima. Nikichomeka funguo niliochongesha kwa locksmith ile taa haizimi inaendelea kuwaka. Jana niliamua kwenda Toyota na kuwaeleza shida yangu wakaniambia funguo wa Spare ni $500 ambayo ni approximately 840,000/=. Gari nililokuwa natumia mwanzo halikuwa na funguo wa spare lakini nilichonga funguo wa spare kwa shilingi 10,000/= tu na ulifanya kazi bila tatizo. Mwenye ujuzi wa haya mambo ya funguo za magari tafadhali tushirikishane ili kama kuna namna ya kuokoa jahazi nifanye hivyo. Otherwise itanibidi tu kwenda Toyota kulipia kiasi hicho cha fedha nipate spare key.
Shukrani.
Cc: LEGE , CYBERTEQ

Ufunguo wenye logo ya Toyota ndio uliokuja na gari na huo mwingine umeandikwa JMA ndio niliochongesha.
25yy5n7.jpg
wcjllg.jpg

-> hapa hiyo taa nyekundu yenye shape kama gari ikiwa inawaka kabla ya kuchomeka funguo uliokuja na gari.
2isgu1e.jpg

-> hapa baada ya kuchomeka funguo original wa gari taa ikazima
21brv3d.jpg

Pole Mkuu hayo yalishanitokea Mimi kwa gari kama yako Nikaelekezwa kwa mzungu fulani anaitwa Felix ilitumia kama dk. 10 au 15 akaja na fungua akasema kachongeshe tu kilichobaki ila bei yake ilikuwa ni 250,000/= ila hapa mjini ukitaka kuja kwangu andaa 50 yangu nikupe namba yake
 
Kuna watu mna njaa na pesa
 
Kuna watu mna njaa na pesa

Na bila kusahau kuna watu wanapenda vya Bure.... utatiwa kidole....................................cha Kichwa sinki

Wenye shida zao huwa hawaoni Shiidah ila Mpembe ndio Nuksi... kijiba cha roho... Huyo Marekani tu hakupi kitu bure.. katika Dunia hii hakuna Free lunch tambua hilo...
 
Mnandi kinachotakiwa hapo kwanza ni kuupata huo funguo wenye transponder chip iliyo compatible na gari lako alafu ndio uwe programmed kuwasha gari lako. Programming inaweza kufanyika Manually (process zinatofautiana kati ya magari) au kwa kutumia Key Programmer ya gari husika. Gari lako lina "immobilizer System". Kazi ya immobilizer system ni kuzuia wizi wa gari kwa kutumia funguo malaya au kwa kufanya 'hot wiring'. Hii system inafanya kazi kwa kuDisconnect fuel supply kwenye engine mpaka utakapoweka funguo original za gari. Kama upo Arusha nitafute kwa 0716-904626 / 0767-174757 ili nikusaidie upate funguo ya Spare..

images
10hr9ee.jpg
images
images
Ningedshangaa sana kama watu wa Arusha hawana ufumbuzi wa hilo tatizo. Arusha ni kila kitu mpaka mjapan aliwavulia kofia alipotembelea Arusha akakuta magari ya Toyota na Nissan yanayotumika kupeleka watalii yameongezwa chasis. Arusha kwa magari ni kila kitu

Na bila kusahau kuna watu wanapenda vya Bure.... utatiwa kidole....................................cha Kichwa sinki

Wenye shida zao huwa hawaoni Shiidah ila Mpembe ndio Nuksi... kijiba cha roho... Huyo Marekani tu hakupi kitu bure.. katika Dunia hii hakuna Free lunch tambua hilo...

Tatizo huo umaskini wako ndo unakusumbua...
 
Pole mimi sio Masikini ni mtu mwenye kipato cha kati... Na inakuwaje unione mimi tu ndio nina njaa.... huku mtu akihitaji huduma? Nadhani katika Maisha yako njia moja tu ambayo wewe unaifahamu ya mtu kupata kipato ambacho hakiwezi kuitwa Njaa ni kuajiliwa kazi sehemu fulani...

Jambo nililofanya mimi ni kama Udalali na udalali si kazi ya njaa... ndio maana huwa Haiishi hata kwenye Mambo ya Dini udalali upo ila una jina lingine tu ila ufanyaji wake kazi ni mmoja tu ambao ni ule ule wa kuwasaidia watu kupata kitu au ujumbe n.k kinachohusiana na jambo lililo mbele au kazi husika... Watu wa makanisa huita watu kwa mikutano na kuwaelewesha kuhusu Mungu wa Kweli na hao watu wakipatikana huingia Makanisani na Hutoa Sadaka... je na hiy ni Njaa?

Kuna makampuni ya Kuuza Vocha za Simu za Makampuni kadhaa huziuza hizo vocha na huwa wanapata chao je na hao ni Njaa?

Kuna watu kazi yao ni Minada wao hawana mali ila kazi yao ni kutafuta wanunuzi kwa kutumia Adress yao na hupata fungu lao baada ya mali kuuzwa je na hao ni Njaa???

Hata waajiliwa huwa hawana kitu wakiajiliwa mwisho wa mwezi hupata Mishahara je na hiyo tuiite ni Njaa?

Mimi nimetoa angalizo kama akitaka anipe kiasi nilichotaka ni udalali nimefanya kama unaona Njaa na wewe Mpe hiyo Namba ila kuna siku utakutana navyo na pesa Utaitoa tu... ndio utajua kuwa ni Njaa au lah...

Jaribu kuwa Mtu wa Kuelewa sio kila kitu ukiletee ushindani.... Siku Njema na Kumbuka Ukiishi Dar lazima Utumie Ubongo kuishi...
 
Kuna jamaa wako mwenge ngoja nitafute namba yao watakufanyia programming ya funguo yako mkuu
 
Pole Mkuu hayo yalishanitokea Mimi kwa gari kama yako Nikaelekezwa kwa mzungu fulani anaitwa Felix ilitumia kama dk. 10 au 15 akaja na fungua akasema kachongeshe tu kilichobaki ila bei yake ilikuwa ni 250,000/= ila hapa mjini ukitaka kuja kwangu andaa 50 yangu nikupe namba yake

Hahahaaa, si mchezo! Hiyo funguo yenyewe tu haifiki elfu 50, kuiprogram anaweza kufanya hata mwenyewe kama ana akili timamu ya kuelewa maelekezo, na uvumilivu!
 
Mkuu usiwe unapinga kila kitu kilicho mbele yako... hata Madaktari kwenye Mahospital hutibu watu kwa kuwaelekeza tu watumia dawa gani na kwa timing fulani kisha wanakunja mkwaja mwingi zaidi ya hiyo elfu hamsini.... Sasa hayo maelezo unayotaka kuyatoa jinsi ya kuiprogram hiyo funguo na je hao waliotengeneza hiyo program ni wasamaria wema na wametengeneza kwa ajili ya watu wanaopata shida? hivi wewe hufahamu kuwa hakuna free lunch? na hizo prosess tu za kufanya hiyo program lazima pesa zitumike... mimi pia nilitoa hiy Hamsini na maisha yakaenda tu Funguo niliuziwa elfu 15 ukachongwa kwa elfu 8 na aliyenieleza nilimpa cha juu na ukawekewa hiyo program kwa 250,000/= na nilitumia usafiri na nikasubiri na simu nilitumia vyote hivyo nilitumia pesa...kama laki 3 na ushee... mnaongea nini humu jamani au ndio watu kwa kujifanya bab kubwa sana kumbe unaongea pumba...

JF asilimia kubwa ni wajinga wa kuiga akili za kijinga za watu wachache humu...
 
Kwani mimi nimepinga? Sijapinga kitu mkuu, hata kuuliza njia au ofisi fulani ilipo kuna watu wanatoza pesa, lakini hilo halimzuii mtu mwingine kukuelekeza bure! Mimi nimeweka senti zangu mbili tu hapo, kufanya programming ya hiyo funguo siyo sayansi ya maroketi, inaweza kufanyika manually kirahisi tu (hakuna software inayoingizwa hapo mpaka useme "aliyetengeza hiyo programme"), ni function ambayo mtengenezaji wa gari aliiweka kwa ajili hiyo, haina haja ya kulipia chochote, labda kama hauna muda wa kufanya hivyo na unaamua mtu akufanyie, either kwa kutumia kifaa maalum au kwa kutumia miguu tu!

Ujinga ni kuendekeza njaa hata kwa vitu vidogo, unadalalia mpaka namba ya "fundi"?!
 
ni kweli kama unavyosema CYBERTEQ , key programming inaweza kufanyika manually na kila gari ina process/steps zake. Lakini hizi immobilizer systems huwa zinatunza kumbukumbu kwenye ECU kila unapoongeza funguo mpya. Uwezo wa memory ya kutunza funguo unatofautiana kwenye magari. Gari la huyu mdau lina uwezo wa kuweka Maximum funguo 12. Baada ya hapo ni lazima uzifute zote na uanze moja. Sasa kama memory itakuwa imejaa ni lazima atumie Key Programmer kufuta hizo funguo zingi otherwise kwa manual process hataweza.
 
Last edited by a moderator:
mkuu nunua ufunguo wenye chip au njoo nikuuzie then mashine mm ninayo nitakufanyia program buleeee kabisaa maana naona watu wanapigana vikumboo.

harafu kufanya program some times sio rahisi kama wasemavyo wadau..na funguo haiwezi zidi laki 1.
 
Funguo za magari toka japani kuanzia miaka ya 2000,hivi zimewekwa Computerized module ambayo inaongeza ulizi wa gari husika.Hii Module wakati unachomeka fungua na kupiga start ya gari inacheck serial Number ya Control Box ya gari husika ECU, kama sio sawa na serial yake kwenye funguo gari itawaka hiyo taa nyekundu na aitowaka.(kuna jamaa ana unversal Module Ametengeneza mwenyewe Huwa anawasha gari yeyote ila hutumia zaidi ya dakika 5 au kumi mpaka apate frequency usika) hapa Tanzania wapo watu wachache sana tunaoweza kuprogram funguo hizi mpya.Ata kama utachonga funguo mpya still kama aina chip itakuwa ni kazi bure kuwasha gari.
Mkuu Lenge nnaona yupo katika mchakato wa kuanza hii huduma officially hapa Dar all the Best.
Ndugu Mnandi last year tulichaji 4M kwa ajiri ya fungua ya lori la SCANIA na mmliki akubisha kulipa.View attachment 195440View attachment 195442View attachment 195445

pamoja sana mkuu Chipukizi sema ndio hivyo mashine zake ni garama sana aisee kama DIGIMASTER 3 bei yake imesimama sana mdogo mdogo tutafikaa tuu. nitakutafuta mkuu kuna ishu flani naifukuzia ndio maana nikawa kimya kidogo.but hata ile mashine nyingine kwa ishu ndogo ndogo kama hizi inapiga flesh.
nilii update now kiulain kdg
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom