Naomba msaada mahali ninakoweza kuipata hii dawa DINOPROSTONE 3MG. ni muhimu mno!

Kwani hakuna dawa nyingine za kuinduce labor tofauti na dinoprostone?Mbona oxytocin ziko nyingi tu ila zinatoka kwa prescription

Mwambie huyo daktari awasiliane na mfamasia wa hiyo hospital apewe ushauri wa dawa mbadala za kuamsha uchungu.
Mkuu Dinoprostone haitumiki kwenye labour induction, inatumika kwenye cervical ripening. Ukimpa mtu oxytocin (kuinduce uterine contractions) bila cervical ripening unaweza sababisha uterine tear.

Also zinapatikana wodi karibu zote za wakija mama hospitali kwa sababu ni Dawa muhimu.

Sababu ya mtu kuitaka hii Dawa kinyemela bila kupitia hospitali ni kama anataka ku fanya criminal abortion ndo maana ni controlled drug
 
Siku 3 mmemuweka mgonjwa hospitali?

Ikishindikana kawaida kamfanyieni operation...kama hawana iwezo pelekeni hospitali inayowezekana

Mtakuja poteza mama na mtoto bure....kuzaa kawaida sio ushujaa

Ila kama yupo hospitali ya serikali zungumza vizuri na manesi na madaktari.....uhai wa mama na mtoto muhimu
nashukuru ndugu mpaka muda huu hajafika dactar wala nesi wapo tu watu wa usafi wakifika nitaongea nao mkuu
 
wakuu nawasalimuni sana, naomba msaada kwa hili ndugu.
nimeshazunguka hii dar mpaka nimechoka kila duka halina hii dawa.
ni ya kumsaidia mama mjamzito kujifungua kwa maelekezo ya daktari ameshaitiliza siku za kujifungua kwa hio hio dawa itakuwa ni ngumu sana kujifungua. naombeni sana wa kuu.

We sema tuu unataka kutoa mimba.. Mbona Huduma unayoitaka ni rahiisi sana kwenye hospitali zetu..
 
hapana ndugu, ni mke wangu alikua ajifungue toka tar 19 lakini njia haifunguki na dactari amemuandikia dawa hio,tumeanzia kuitafuta hapa sinza mwenge manzese kariakoo hadi muhimbili hawana, muda huu nawasubiria madocta niwaambie nimeikosa sijui watashauri nini.
 
Siku 3 mmemuweka mgonjwa hospitali?

Ikishindikana kawaida kamfanyieni operation...kama hawana iwezo pelekeni hospitali inayowezekana

Mtakuja poteza mama na mtoto bure....kuzaa kawaida sio ushujaa

Ila kama yupo hospitali ya serikali zungumza vizuri na manesi na madaktari.....uhai wa mama na mtoto muhimu
ni hospitali ya serikali mkuu sinza palestina, kwa kweli hawa manesi na docters wanausika na wajawazito sipati nafasi ya kuongea nao.
 
Siku 3 mmemuweka mgonjwa hospitali?

Ikishindikana kawaida kamfanyieni operation...kama hawana iwezo pelekeni hospitali inayowezekana

Mtakuja poteza mama na mtoto bure....kuzaa kawaida sio ushujaa

Ila kama yupo hospitali ya serikali zungumza vizuri na manesi na madaktari.....uhai wa mama na mtoto muhimu
Hatari sana

Hawa jamaa wanasemaga matibabu bure kwa wajawazito,kumbe hata dawa hawana
 
hapana ndugu, ni mke wangu alikua ajifungue toka tar 19 lakini njia haifunguki na dactari amemuandikia dawa hio,tumeanzia kuitafuta hapa sinza mwenge manzese kariakoo hadi muhimbili hawana, muda huu nawasubiria madocta niwaambie nimeikosa sijui watashauri nini.
Omba kuonana na daktari mkuu,mwambie una shida ya dharura sana,
 
Sio lazima hiyo tuu..kuna altenatives nyingi km tatizo ni augmentation/induction of labour kuna dawa na tricks nyingi zinatumika mahospitalini mkuu..usiumize kichwa!
Toa ushauri mkuu wa kumsaidia mdau anaumiza kichwa
 
Haya ndo yanatokea pale unapoomba ushauri kwa mitandao ushauri kwenu
Mgonjwa mjamzito kukaa hospital siku Tatu tano bila kujifungua uchungu wa kweli ni kawaida

Hospital nyingi za Tanzania hazina sawa za aina nyingi

Tunatakiwa kuelewa majukumu ya kazi ya Dr na muuguzi

Kuna tatizo LA kupata au madr kutoa taarifa za kukidhi za tatizo LA wagonjwa wetu mahospital

Kwa Mgonjwa husika hapa Juu nashauri zungumza na wauguzi wakupe nafasi ya kupata maelezo ya Dr kama kuna uwezekano wa maelezo na nature ya matibabu

Naona watu wanatoa povu tu APA oo kuna matibabu dawa mbadala na kila kitu sawa sikatai ila kila Mgonjwa ni individual na matibabu yanakua individualised

Ukishindwa kupata sawa inabidi urudi Kwa Dr umpe maelezo ili aweze kufanya maamuzi mapya

Pole Kwa huduma ya shemeji yetu
 
Kama ni cervical ripening tu si watumie hata misoprostol zinapatikana kwa urahisi tu.
Nikupe ushauri wa bure najua una elimu ya level Fulani naheshimu hilo

Misoprostal haijaidhinishwa wala kuruhusiwa na wizara ya Afya ya Tanzania Kwa matumizi hayo so saying ukitumia ikimletea madhara Mgonjwa wizara INA uwezo wa kukusimamisha kazi

Misopr imeidhinishwa wa management ya PPH PEKEE KWA SASA
 
Hospital nyingi inatumika kwa ajili ya cervical ripening kabla ya labour induction na hatujawahi kusimamishwa kazi na huyo mgonjwa kumbuja yupo hospitali. Najua pia kuwa inatumika kwenye active management ya third stage of labour ku prevent PPH, na pi tunaitumia sana kwenye kutibu peptic ulcer disease
 
Nashukuru kama unafahamu sasa ongeza na ethics zako utagundua hicho kinachofanyika tunatumia ignorance ya tunaowahudumia so hatutumii uzoefu kwamba hospital zinatumia Basi Hata kwenye mitandaoni tuandike
 
Mkuu huyo mgonjwa yupo hospitali tayari that is the key point.
 
nashukuru sana wakuu kwa msaada wenu dawa imepatikana kwa msaada wa mhudumu wa hapa imegarimu 50000! sijajua ni halali au la maana hata risiti sijaewa.
lakini yote ya yote ajifungue tuu. uzazi umekua mgumu sana aisee unaweza kusema kuzaa njambo lisilo na maana kabisa.!
 
Hongera mkuu na pole kwa changamoto unayopitia. Ndio uanaume huo. Mgawanyo wa majukumu. Wewe unakimbia huku na kule, shem nae anaugulia maumivu kitandani.
 
nashukuru sana mkuu
Afu mara dawa kama oxytocin na dinoprostone hupatikana hospital sana kwa sababu ndipo wagonjwa (mama wajawazito) hupatikan hivyo kusababisha ziwe adimu mtaan hivyo wawez mwambia huyo daktar akwandikie prescription uende hospital utaipata
 
nashukuru sana wakuu kwa msaada wenu dawa imepatikana kwa msaada wa mhudumu wa hapa imegarimu 50000! sijajua ni halali au la maana hata risiti sijaewa.
lakini yote ya yote ajifungue tuu. uzazi umekua mgumu sana aisee unaweza kusema kuzaa njambo lisilo na maana kabisa.!
Hilo ndo LA msingi inarange 30 mpaka 50 inawezekana kachukua ya Maji ila don't care nachojua hiyo ni dawa nzuri na ndio iliyopendekezwa evidence based kuwasaidia kina mama kuanza uchungu kama amefika miezi Tisa na Haina madhara Kwa mama na Mtoto tumwombee Afya njema ya uzazi
 
Siku 3 mmemuweka mgonjwa hospitali?

Ikishindikana kawaida kamfanyieni operation...kama hawana iwezo pelekeni hospitali inayowezekana

Mtakuja poteza mama na mtoto bure....kuzaa kawaida sio ushujaa

Ila kama yupo hospitali ya serikali zungumza vizuri na manesi na madaktari.....uhai wa mama na mtoto muhimu
hyu jamaa wa nchi gani ? dokta dawa anayo kwenye mfuko wa koti .badala atoe hela anazunguka dar nzima
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom