Naomba msaada kwenye suala hili la passport

Naomba msaada kwenye suala hili la passport

Siku Naipata Nilitembea mkono Mfukoni Isije Kuyeyuka Maana Adi Naipata Ni Balaaa
Yangu niliipata kwa mbinde sitosahau nilipiga sana round pale mpaka leo nikisikia kale kamsemo kwamba ni haki ya kila mtanzania nabaki tu nashangaa
 
Habari za saa,

Nimejaza online form ya kuomba passport, lakini kuna kipengele sijakielewa.

Kuna sehemu ya kujaza nchi unayokwenda. Je, Ina maana kila nchi nitayotaka kwenda nitaomba passport nyingine?

Kingine ni kuwa, kwa wale tunaoapply scholarship mbalimbali kuna viambatanisho ambavyo educational institutions wanataka tuwe navyo ikiwemo passport. Wakati huohuo nikitaka kuomba passport naambiwa nipeleke barua ya mwaliko. Sasa hapa nafanyaje?

Wakuu msaada wenu tafadhali.
Mkuu usipate taabu kuanza kuomba invitation later, hapo kwenye nchi gani unaenda andika Kenya,Uganda n.k,.
Kwani mfano kama utaandika Norway,China,Australia n.k watakuomba mwaliko hasa kama utasema unaenda matembezi, au kama huna mwaliko watahitaji kuchungulia acc yako in sufficient? Una mpunga was kutosha?
Lakin ukijaza za E.A hutapata usumbufu was maswali ,kwani wanajua Kenya ukiwa hata na 300k unaenda na utarud
 
msaada katika tuta, naanzaje kupata hati ya kusafiri(passport) ukiachana na gharama ya laki na nusu je kuna gharama nyingine zozote ambazo pia ningependa kujua
 
msaada katika tuta, naanzaje kupata hati ya kusafiri(passport) ukiachana na gharama ya laki na nusu je kuna gharama nyingine zozote ambazo pia ningependa kujua
Gharam ni laki na nusu kiserikal ila itategemeena na njia utakayopita
 
very simple ukiwa na vigezo na ukajaza fomu yako vizuri ni wastan wa wiki 3 mpk mwezi mmoja ila kama unataka shortcut jipange
 
Zipo kama huna
Ushahidi wa shughuli unayoemda kufanya
cheti cha kuzaliwa kama huna katafute
Kitambulisho cha NIDA/namba ya kitambulisho katafute
Cheti/Kiapo cha Kuzaliwa Mzazi wa Mwombaji kama huna katafute
Picha yako iwe na background ya blue mpauko kama huna katafue

Kama unavyo hivyo vyote na kuna pesa inakuwasha tafuta watoto yatima kawanunulie unga na mchele wakuombee uzidi kufanikiwa
 
HAHAAAAA NIMEKUSOMA SANA CHIEF
 
Back
Top Bottom