Naomba msaada kujitoa kwenye huduma ya Vodacom Simu TV

Bloodmen

Member
Aug 7, 2014
39
9
Nilidownload App ya Vodacom inayoitwa Vodacom simu tv. Muda nilikuwa na download sikujua gharama zake. Baada ya kuanza matumizi nikaona gharama ni kubwa mno, kwa siku tsh. 299.

Nikaona ni vema nijitoe, nilivyowapigia wanielekeze namna ya kujitoa wakanielekeza lakini sikufanikiwa kujitoa. Nikiweka salio tu wanakata hiyo 299 kwa siku. Nikaenda Vodashop bado wakasema tumekutoa lakini nikiweka salio nakatwa hiyo 299 kwa siku.

Sasa nimejiuliza hela inakatwa kwenye system inashindikanaje kunitoa? Naomba mnisaidie kimawazo, nifanye nini ili nijitoe? Maana hiyo vodacom simu tv chanel zake ni zile zile ambazo ziko kwenye simu tv ambayo unatumia MB peke yake wakati hiyo vodacom simu tv unakatwa na vodacom tsh 299 pia uwe na MB.

Nisaidieni wadau kimawazo maana maisha haya tulionayo siyo ya gharama zisizokuwa na ulazima.
 
Ziko app za aina mbili za vodacom simu tv kwahyo kama wanapiga pesa utakuwa umewrong kupakua apps we ungepakua ya kwanza uachane na ya pili coz hiyo ni PRO na siyo free. Mimi ninayo hiyo ya kwanza na haileti njenje kwahiyo uninstall Hiyo app baadaye pakua nyingine.
 
Back
Top Bottom