Makampuni ya Simu yapora Watanzania kwa kuongeza gharama za Bando mara mbili ya kawaida, hakuna anayejali

jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
8,940
2,000
Tuna makampuni ya simu mengi hapa Tanzania. Kwa bahati mbaya, karibu yote ni ya kigeni baada yale ya wazawa kufilisika.

Kuanzia 30-07-2020 Mkampuni haya ya simu yameanza kidogo kidogo kupandisha gharama za vifurushi, wanapandisha alafu wansikilizia kama wanyonge watashtuka, sasa wamefika mahali haivumiliki, na kwanini watru hawapigi kelele imegundulika kuwa watumiaji wa mitandao ambao wangepiga kelele wao wanalipiwa na Ofisi zao, hawan cha kupoteza lakini tuwaonye makampuni ya simu huu uhunu mnaofanya ipo siku tutakata laini zenu ama tutanzisha movement kwenye mitandao ya kuwakataa na turudi kwenye mtandao mmoja wa serikali

1. Vodacom: wamepandisha bando za wiki mwezi na mwaka, kama Tigo walivyofanya.

2. Tigo (Mic) : imepandisha bando la 1500 kuwa 3000 na kuondoa mb kabisa, yani ukitaka mb unanunua separate.

3. Airtel: Hawaeleweki, mara wanakupa bando ila litumike kuanzia sa nne usiku

4. Zantel: hamna kitu

5. TTCL: walau hawa wapo wapo na wanaeleweka,

MAKAPUNI YALIYOKUFA/FILISIKA

1. TRITEL
2. MOBITEL :- Kampuni ya kwanza kabisa ilikuwa ni Mobitel iliyopewa liseni Novemba 1993 na ilikuwa inatumia mfumo wa analojia kwa ajili ya kutoa huduma kwa wateja waliokuwa Dar es Salaam na Zanzibar. Makao makuu na mitambo ya kampuni hiyo ilikuwa pale maeneo ya Gerezani – Mtaa wa Lugoda.

Kampuni hii ilikuwa inamilikiwa na MIC Tanzania Limited na wenye hisa walikuwa ni pamoja na kampuni ya Millicom International Cellular ya Luxembourg, Ultimate Communications Limited ya Tanzania na Tanzania Telecommunications Corporation – yaani TTCL.

Mapema mwaka 2006 kampuni ya Millicom International Cellular ya Luxembourg ilinunua hisa zote za makampuni yake yaliyo Barani Afrika ikiwemo MIC Tanzania na hivyo kubadilisha jina la utanbulisho wa kampuni hiyo maarufu ya simu za mkononi kuwa TIGO.

Hapo mwanzo – kabla ya ujio wa mfumo wa digitali (GSM) ni wachache sana waliweza kuwa na simu za aina hii kwani awali ilikuwa ni kwamba unachajiwa hata pale unapopigiwa simu. Hizo simu awali zilikuwa zinauzwa na kampuni hiyo lakini iwapo mteja atakuwa na simu yake mwenyewe basi huipeleka pale kwa ajili ya kusanidiwa (configured) na pia kulipiwa gharama za kuongea – yaani kuwekewa salio.

Mwaka uliofuata – 1994 – kampuni nyingine – TRITEL ilisajiliwa. Kampuni hii – ambayo ndiyo chimbuko la kampuni ya Airtel ya sasa – ndiyo ilikuwa ya mwanzo kabisa kuwa na mfumo wa dijitali GSM. Baadaye shughuli za kampuni hii zilichukuliwa na Celtel ya Mohamed Ibrahim – bilionea wa Sudan ambaye naye aliuza shughuli zake kwa kampuni ya Kuwait – Zain – mwaka 2007.

Mwaka 2010 kampuni ya Bharti Airtel ya India ilinunua hisa zote za kampouni ya Zain Africa kwa dola za Kimarekani 10.7 bilioni na hivyo jina la kampuni hii ya simu za mkononi hapa Tanzania likavadilishwa na kuwa Airtel.

Mwaka 1999 kampuni ya simu ya Vodacom yenye makao makuu Afrika ya Kusini nayo ilipata usajili hapa Tanzania na ni kampuni ambayo ilikua kwa haraka sana – kwa maana ya kuchota wateja wengi katika muda mfupi. Hi ilitokana na uwezo wake wa kuingia katika maeneo ya ndani ya nchi kutokana na kujengwa minara mingi ya kusambaza mawasiliano (communication towers).

Aidha kampuni hii ilikuwa ya kwanza kuingiza huduma za kutuma pesa katika simu (MPesa) huduma ambayo ilikua kwa haraka sana na kuigwa na makampuni mengine ya simu za mkononi.

Kwa ujumla ukuaji wa kasi wa huduma za simu za mkononi nchini Tanzania kulisaidiwa na kuwepo kwa huduma ndogo na duni sana za huduma za simu za kawaida yaani landlines zilizokuwa zinatolewa na TTCL.

Hii ilichangiwa na unafuu wa huduma za simu za mkononi hasa katika ile huduma ya malipo kabla (prepaid services). Aidha gharama za kuunganisha simu za mkononi (installation charges) ni rahisi sana ikilinganishwa na gharama za kuweka huduma za simu za landline.
 
screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
9,562
2,000
Na hizo bando ndogo walizotuachia zinaisha fasta, sijui kuna jini mnyonya bando. Juzi nimejiunga GB 4 za Tigo leo wananiambia zimebaki MB 400 wakati sijaitumia kivile
 
Santos06

JF-Expert Member
Mar 11, 2019
727
500

wanakuja
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom