Naomba msaada kuhusu tatizo la Kuku wangu

wa hapa hapa

JF-Expert Member
Aug 20, 2014
281
150
Habari wadau, naomba msaada wa tiba kwa vifaranga wangu (SASSO) ambao kesho watatimiza mwezi tangu niwachukue.

Mwanzoni walikuwa wanaendelea vizuri lakini baada ya wiki mbili walianza kusumbumbuliwa na miguu(Wanapepesuka) baada ya siku kadhaa wanakufa.

Nimejaribu kuwapa dawa ya Taiphod na vitamins lakini bado tatizo linaendelea. Kuna wengine wakijisaidia kinyesi kinakuwa na rangi ya Ugoro/Kahawia.

Mwenye kujua tiba anisaidie.
 
Vipi kuhusu macho kuvimba coz nimewacheki mida ya jioni Kuna baadhi yao macho yao yamevimba.
Ungetuma picha tuone uvimbe uko vipi mara nyingi uvimbe unaweza kua ni
1.upungufu wa vitamin
2.ndui (chicken pox) -uvimbe mdogo mdogo usoni kama vipere
3.au mafua (infectious coryza) uvimbe ulojaa maji unaombatana na kutoa fluids au mafua kweny pua na kumua kwa shida

Kulegemea miguu
Pia upungufu wa madini hasa calcium phoshphorus na magnesium yanahusika
Je unatumia chakula gan? Unanunua au kutengeneza mwenyewe?
Endelea kuwapatia multivatimins na ikiwezekana wapatie antibiotcs kama OTC 20% Kupunguza hzo infections

Maintain usafi kwenye mabanda yako kwa asilimia zote

Hakikisha unawapatia maji safi na chakula kisafi (chakula kama unaacha kinachacha kinaweza kusababsha ungnjwa unaitwa aspergilosis ambao ndo miguu inapata paralysis wanashindwa kusimama na kufa )

Unaweza kuwatenga kuku waliokwsha athirika kuepusha maambukizi mapya

Mwisho mtafute mtaaram wa mifugo alie karibu yako upate ushauri zaidi
Au nenda duka la madawa ya mifugo utapata ushauri na dawa zake
 
Bila shaka umewaweka kwenye sakafu na hivyo ndio shida kama sivyo banda linabaridi kwenye floor
 
Kama unavyomuona kiongozi
IMG_20210317_163120_267.jpg
 
Mkuu wape dawa kama ulivyoshauriwa. Au watenge hao wagonjwa toa hiyo chanjo fasta. Wakipona nenda ulizia chanjo ya tatu moja wapatie.

Ila hiyo haitazuia coccidiosis. Lakini itaondoa pox, coryza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom