Msaada kujua nini kinaua kuku wangu

Mtuflani Official

JF-Expert Member
Dec 31, 2019
1,938
4,354
Nimekua nikijihusisha na ufugaji wa kuku. Ila sasa naona wanakufa. Kuku wangua nawaachia wazunguke ndani ya geti. Yaani wanatoka kwenye banda na kuzurura ndani ya geti tu.

Ila cha ajabu kuna muda unawafungulia banda asubuhi lakini unaona hawatoki nje. Wanakua wametulia tu chini. Ukiwasogelea ndo wananyanyuka. Baada ya siku moja ya kuonesha hizo dalili unakuta amekufa.. Kinyesi chao ni cha kuharisha na ni rangi ya “light green”.

Maeneo ya nyuma unakuta amejiharishia na kinyesi kuganda kwenye manyoya. Sijui ni ugonjwa gani huu. Msaada tafadhali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom