Naomba msaada kuhusu msemo

Kingeke Mavoya

JF-Expert Member
Jan 27, 2017
619
598
Habari zenu wakuu nina msemo ambao kwangu nimgumu kidogo hivyo nilikua naomba msaada nifahamu kwamba:-

Nini maana ya msemo "MWENDA TEZI NA OMO, MAREJEO NGAMANI"
 
Kijana, hili halitakuja kwenye mtihani uelezee.
By the way, hujui TEZI, OMO, MAREJEO, NGAMA (NI)????
 
Utaenda/utazunguka kila mahali ila utarudi nyumbani(nyumbani ni sehemu nzuri/salama) ni sawa na ule msemo wa Kiingereza go east,go west home is the best.
 
Utaenda/utazunguka kila mahali ila utarudi nyumbani(nyumbani ni sehemu nzuri/salama) ni sawa na ule msemo wa Kiingereza go east,go west home is the best.
ina maana rahisi tu,
mwenda tezi(sehemu ya nyuma ya chombo=shetri)na omo(sehemu ya mbele ya chombo) marejeo ni ngamani(sehemu iliyoko katikati ya chombo ambamo shehena huwekwa)yaani,waweza ukazunguka huku na huku ila mwishowe utarejea nyumbani...kwa kiingereza;east or west,home ia thw best...
 
Habari zenu wakuu nina msemo ambao kwangu nimgumu kidogo hivyo nilikua naomba msaada nifahamu kwamba:-

Nini maana ya msemo "MWENDA TEZI NA OMO, MAREJEO NGAMANI"
Tezi ni mbele kwa jahazi na omo ni nyuma. Ngamani ni katikati. Hutumiwa kama kumpasha mtembezi, waruwaru asiyetulia. Kwa hiyo, maana yake ni kuwa: nenda uendako lakini utarudi tu hapa, kwa mfano nyumbani.
 
Back
Top Bottom